Hivi karibuni kuna mtumishi kahama kutoka Serikali Kuu kwa cheo cha mhasibu mwandamizi (Senior accountant-SA) akiwa ametumikia miaka 10 kwenye utumishi wa umma, baada ya miaka mitatu alikuwa anapanda kuwa Mhasibu Mkuu (Principle Accountant). je ni kanuni gani ya utumishi inatoa mwongozo wa kule anakohamia kwamba atapewa cheo gani? ukizingatia kuwa anakohamia cheo cha Mhasibu mwandamizi kina madaraja mawili, SA-I na SA-II.
Mtiririko wa upandaji wa Serikali za Mitaa ni : Accountant-II (yr-0), Accountant-I (yr-4), Senior Accountant-SA (yr-7), Principle Accountant-II (yr-10), Principle Accountant-I (yr-13).
Wakati ule wa taasisi ni Accountant II(yr 0), Accountant-I (yr-3), Senior Accountant-I (yr-6), Senior Accountant-II (yr-9), Principle Accountant (yr-12)
Mungu akubariki unapochukua muda wako kunielimisha.