Mtume wa Mkuranga Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtume wa Mkuranga Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Asalaam/Alaikum,

  Rehma na Amani ziwashukie Waislam wote popote walipo. Amin.

  Ndugu

  Waislam, Nimeona cd inayoonyesha mtu mmoja tena anae jiita Muislam anadai kuwa yeye ni MTUME wa Mwenye ez Mungu na anaowafuasi huko Mkuranga nje kidogo ya Jiji la Dar.

  Kwa mujibu wa Wafuasi wake Kiongozi wao amepewa UTUME kwa njia ya Miujiza na wanamkubali na kumtii kuwa ni Mtume wa Kweli, na wanapokea amri kutoka kwake kama Nabii.

  Sasa sijui kama vyombo vya Kiislamu wanalijuwa hilo au hawajui, Naomba kwa wanaohusika kama Bakwata ,Mwamsho, Jumuia zote za ki Islamu na Serikali kufuatilia suala hili ili kujuwa ukweli wake kabla mtu huyu hajawakufurisha watu wengi zaidi.

  Jina lake anaitwa Mtume ABDALLA SAIDI ,yuko Mkulanga na anao Msikiti wake na watu wake anao waita Masahaba.

  Kwa taarifa zaidi wako Masheikh wenye kuumizwa na unafiki huu walimtembelea mtu huyo na kujionea kufuru zao hizo na jinsi wanavyo wapotosha jamii ya Waislamu.kwa taarifa za kweli kabisa waone sheikh NURDIN KISH KISH wa Msikiti ulopo Vetenary, au sheikh,ABDUL WAKATI,wa Msikiti ulipo Mtaa wa Bungoni Ilala dsm. Vile vile unaweza kuzipata cassete na cd za hao Masheikh niliowataja ambao ndio walitoka kwenda kuwaona siku ya Ijumaa pamoja na Maustadh wa Masjid Tungi ulipo Temeke,Dsm pia walikwenda kushuhudia unafiki wa mtu huyo, casete zinapatikana Msikiti wa Mtoro Kariakoo Dsm.

  OMBI

  Naomba kwa wale watakao bahatika kuzipata cds zao watuwekee kwenye huu mtandao wetu wa zanzinet, https://www.jamiiforums.com na kwenye YOU TUBE ili Dunia iwafahamu na ikiwezekana wakamatwe na waadhibiwe kwa mujibu wa Sheria.

  NAKUTAKIENI RAMADHANI KAREEM , AMIN
   
 2. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,657
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Huyu ni Ayatollah tu kama alivyokuwa Khomeini na wafuasi wake. Au labda hadi awe Mmanga ndiyo mtamkubali? :rolleyes:
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nini maana ya mtume?

  Kwani mtu kujiita mtume kuna kosa Gani?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyo bwana ajisajili tu ktk vyombo husika..lakini baada ya hapo hana hatia..inabidi tu mkubali kuwa kila mtu ana imani yake na hakuna kushurutishana ktk dini.

  "Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua."
  Al Baqarah – 256


  "Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?."
  Yunus – 99
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mh Ayatollah si mtume. Ni kiongozi wa dini. Tafsiri ya mtume inatofautiana kati ya tamaduni na tamaduni au waumini na waumini. Ndio maana kuna mtume Mwingira na huyu tunayemsikia. Nadhani la kufuatilia hapo ni kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama yale ya Chibiliti (sorry kama nimekosea) aliyewachoma waumini wake, maana watu hawa huwepo muda mchache na wanauwezo mkubwa wa kuwashawishi wananchi waliokata tamaa
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  mimi hapo sioni ni tatizo hata kidogo, binadamu hana mamlaka ya kuhukumu mwingine kwa masuala haya ya dini, ni mungu mwenyewe tu,
  sasa yeye akisema ni mtume Waislamu wengine wataathirika vipi, mbona kwa Wakristo kuna Mitume mengi tu, mwacheni aanzishe dhehebu lake watakao mkubali basi watamfuata, na yeye sio wa kwanza yupo Ghulam wa Amahydia, yupo Kharifa wa USA nk
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Duh kaaz kwer kwer
   
 8. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yes mtu akiona na roho wa Mungu ndani yake na anamuongoza vyema na anaweza kufuata nyayo za mitume waliotangulia muacheni.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  huyu anahaki ya kujiita mtume kama mitume wengine akina muhamad ili mradi tu hatoi mafundisho yanayowapeleka watu kwa shetani.....
   
 10. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mtume ni mtu aliyetumwa, kwa hiyo sio lazima awe ametumwa na Mungu, inawezekana katumwa na Shetani
   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kuna Mtume frednand, mtume kakobe, mtume mzee wa upako!
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Shida hapa watu tunachanganya maana ya neno "mtume" kama linavyotumika ktk Ukristo na neno hilo linavyotumika katika Uislamu. Katika Ukristo wengi wamejiita au wameitwa mitume (apostolos - mjumbe wa Mungu/mtumishi wa Mungu/aliyekabidhiwa ujumbe mahususi wa kuwapelekea wanadamu). Katika Uislamu nadhani neno "mtume" linatumika kwa Wajumbe wachache wa Mwenyezi Mungu wanaotajwa katika Qurani (mtanikosoa nikikosea). Hii ina maana kwamba nje ya hao mtu mwingine hata akiwa mwislamu safi hawezi kujivika tilte hiyo.

  Kama ni hivyo basi yule bwana atakuwa na makosa kadiri ya Uislamu. Na adhabu ya kumpa nadhani ni kumtenga na jumuiya ya Kiislamu au kuongea naye ili ajirudi na kuacha kujiita hivyo. Vinginevyo kama kaandikisha dhehebu lake serikalini jumuiya ya Kiislamu haina adhabu nyingine mbadala kwani nchi yetu inaamini katika Uhuru wa Kuabudu. Mtu ana uhuru wa kuamini au kufuata imani au chochote anachoamini alimradi havunji sheria za nchi.
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Muhammadi na yeye si alijipa utume bandia? Sasa kuna kosa gani na Wabongo tukawa na mtume wetu ambaye si mmanga?

  Mimi nataka namba yake ya simu, huyu mtume wetu mpya.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hao uliyo wataja wana jiita watume au wewe ndiyo ume waita mitume?
   
 15. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kuna mtume na nabii Josephat Mwingira pia, huyu yupo maeneo ya Mwenge.
  Bongo siku hizi watume wako wengi tu. Hivyo huyo sioni ajabu huyo kujiita mtume.
   
 16. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  umewasingizia sijawahi kumsikia kakobe anajiita mtume, kafanye homework yako vizuri
   
Loading...