Mtume apigwa faini kwa uongo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mwanaume mmoja wa nchini Taiwan ambaye hujitambulisha yeye mwenyewe kama mtume wa mungu, amepigwa faini ya dola 1380 kwa kusababisha mtafaruku kWang Chao-hung au maarufu kama Mwalimu Wang ambaye hujitambulisha kwa watu kuwa yeye ni mtume, ameponzwa na maono yake ya utabiri wa tetemeko la ardhi na tsunami ambalo halikutokea.

Mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka huu, "Mtume" Wang aliandika kwenye blogu yake utabiri wa kutokea tetemeko kubwa la ardhi litakaloambatana na Tsunami mnamo mei 11 mwaka huu.

Mtume huyo feki pia aliwataka watu wazikimbie nyumba zao kwani hazitaweza kuhimili tetemeko hilo la ardhi na kuwashauri waishi kwenye nyumba zilizotengenezwa kwa makontena ya mizigo.

Wito wake ulipokolewa na watu wengi ambao kweli waliziacha starehe za nyumba zao na kwenda kujibanza kwenye makontena ya mizigo.

Mei 11 ilikuja na iliondoka na hakuna tetemeko la ardhi wala tsunami lililotokea nchini Taiwan na hivyo kuifanya serikali ya Taiwan iamue kumpandisha kizimbani Wang kwa kujidai mtume na kueneza habari za kizushi zilizosababisha mtafaruku kwenye jamii.

Akisomewa hukumu yake jana kwenye mahakama ya mji wa Nantou, Wang alihukuiwa kulipa faini ya dola za Taiwan 40,000 ambazo ni sawa na Tsh Milioni 2.13.

Wakati huo huo, Uchunguzi umeanza kujua kama Wang alikuwa amekula dili na watu wanaouza au kukodisha makontena

Iwapo ataonekana alikula dili, huenda akahukumiwa adhabu zaidi kwa kosa la utapeli.wa jamii kwa kutabiri tetemeko kubwa la ardhi ambalo halikutokea.
 
Back
Top Bottom