Lindi: Aliyepokea hongo ya Tsh. 600,000 apigwa faini ya 500,000

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Mahakama ya Wilaya ya Liwale imemhukumu Bw. Khalidi Rashid Mingoli, aliyekuwa. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Kikulyungu na Mkazi wa Kijiji hicho, baada ya kukiri kosa na kuamriwa kulipa faini ya Shilingi 500,000/= au kwenda jela miaka mitatu, kwa kosa la kupokea hongo ya Shilingi 600,000/=.

Hukumu hiyo dhidi ya Khalidi Rashid Mingoli katika Shauri la Jinai Na. 1062/2024, imetolewa chini ya Mhe. Christopher Makwaya - Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Liwale Januari 15, 2024.

Mshtakiwa huyo alipokea hongo jumla ya Shilingi 600,000/= kutoka kwa wafugaji watatu waliokuwa wameingiza mifugo kwenye ardhi ya Kijiji cha Kikulyungu kinyume na utaratibu ili asiwachukulie hatua za kisheria.

Mshtakiwa amelipa faini Tshs. 500,000/ = na kuachiwa huru.

Kesi hii imeendeshwa na Wakili Salum Bhoki wa TAKUKURU Lindi.

Chanzo: TAKUKURU
 
Vi rushwa vidogo dogo wanakomalia
Walewanaokula mamilion kwa mabilion kimyaa

Ova

Jemedari Heri ya mwaka mpya.

Nipe mwanga kidogo, inamaana anarudisha kwanza pesa aliyochukua rushwa Kisha anatoa lakini Tano kama faini au anatoa lakini Tano kwenye Ile laki sita aliyochukua rushwa anabakiwa na kilo ya kwenda kujipooza machungu?
 
Back
Top Bottom