Mtulia Awapigia magoti CCM, Awaomba Radhi kwa Kuwashinda 2015 Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni (CCM)

Arekebishe tu mitaro, usombaji wa takataka na utupaji wake, bomoa bomoa ya waliokando ya mitaro na kulinda mitaro..yawezekana..
 
Kutoka Dar es Salaam.
Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amewaomba radhi wanachama wa chama hicho tawala kwa ushindi wa kishindo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiwa CUF
Mtulia ametoa kauli hiyo leo Januari 21, mwaka 2018 wakati akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2015, Mtulia alishinda ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, lakini Desemba 2 mwaka jana alijivua uanachama wa chama hicho na kuhamia CCM, hivyo kupoteza sifa ya ubunge. Hata hivyo CCM kilimpitisha kugombea ubunge katika jimbo hilo
Huku akiviponda vyama vya upinzani Mtulia amesema, “Nawaomba msamaha kwa yote niliyowakwaza wakati wa kampeni na kushinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi 2015.”
"Mnisamehe mtoto wenu nimerudi nyumbani kwenye chama kubwa. Niliwapa kadi lakini mmeamua kunipa ubunge."
Amesema vyama vyote vya upinzani ni sawa na asasi za kiraia, kwamba ni tofauti na ilivyo CCM kwa madai kuwa wapinzani wanasaka pesa na si kusaidia wananchi
Alitaja sababu iliyomfanya kuhama CUF kwamba ni baada ya kuona viongozi wake wakuu hawaelewani, huku akisisitiza kuwa nje ya CCM ni sawa na kujenga ukuta.Mtulia aliambatana na wanachama wa CUF walioamua kujiunga na CCM na kukabidhiwa kadi.
Chanzo: Mwananchi
aaa51581fbc8a9b7f173b8b36affe29c.jpg
 
Hahaha uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana, ikiwa alishinda akiwa CUF leo atashinda vipi akiwa CCM?! Hoja ya viongozi CUF kutokuelewana inawasaidia nini wananchi?! Yeye alikuwa mbunge wa jimbo kwa ticket ya CUF, yeye hakuwa kiongozi wa CUF, na kutokuelewana kwa uongozi ndani ya CUF kuliathiri vipi ubunge wake. Yeye alikuwa akiwawakilisha wananchi wa jimbo la kinindoni bungeni, hakuwa akiwakilisha makundi ya uongozi ndani ya CUF.
Yeye aliwashinda ccm kwasababu hawakukubalika sio mtu. Leo yeye anadhani walimchagua yeye na sio chama hahaha.
Kwa hoja yake ni kwamba wanakinondoni hawakuchagua muwakilishi kwa kigezo cha chama gani katoka, anatuambia na kutuaminisha alichaguliwa yeye Mtulia siyo Mtulia mwanachama wa CUF. Lakini alipaswa kuelewa siasa za sasa chama kina uzito sanaaa.
Alipaswa atuambie alishindwa kuwa muwakilishi asisingizie chama na uongozi wake.
Hapaswi kuwa muwakilishi popote ikiwa anawakilisha chama badala ya wananchi.kama anawakilisha chama alipaswa akagombee nafasi za kichama huko ccm alikohamia.
Ubunge wa kuchaguliwa ni uwakilishi wa wananchi.
Isipokuwa wa viti maalum ule unawakilisha chama.
 
Back
Top Bottom