Mtulia Awapigia magoti CCM, Awaomba Radhi kwa Kuwashinda 2015 Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni (CCM)

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Kutoka Dar es Salaam.
Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amewaomba radhi wanachama wa chama hicho tawala kwa ushindi wa kishindo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiwa CUF.

Mtulia ametoa kauli hiyo leo Januari 21, mwaka 2018 wakati akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2015, Mtulia alishinda ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, lakini Desemba 2 mwaka jana alijivua uanachama wa chama hicho na kuhamia CCM, hivyo kupoteza sifa ya ubunge. Hata hivyo CCM kilimpitisha kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Huku akiviponda vyama vya upinzani Mtulia amesema, “Nawaomba msamaha kwa yote niliyowakwaza wakati wa kampeni na kushinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi 2015.”

"Mnisamehe mtoto wenu nimerudi nyumbani kwenye chama kubwa. Niliwapa kadi lakini mmeamua kunipa ubunge."

Amesema vyama vyote vya upinzani ni sawa na asasi za kiraia, kwamba ni tofauti na ilivyo CCM kwa madai kuwa wapinzani wanasaka pesa na si kusaidia wananchi
Alitaja sababu iliyomfanya kuhama CUF kwamba ni baada ya kuona viongozi wake wakuu hawaelewani, huku akisisitiza kuwa nje ya CCM ni sawa na kujenga ukuta.Mtulia aliambatana na wanachama wa CUF walioamua kujiunga na CCM na kukabidhiwa kadi.

Chanzo: Mwananchi
 
Mtulia amenikumbusha story za kile kitabu cha fasihi "Things fall apart "Naona amekumbwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, Muda huu sio wa kuomba msamaha ni muda wa kupambana jukwaani, Alishavunja mkataba na wanakinondoni

Kuna misingi ya mgawanyo wa madaraka yeye haujui Bunge na Serikali vitu viwili tofauti, Yeye aliamua kuunga mkono sio kuirekebisha na kuikosoa hana mamlaka ya kulia lia ovyo jukwaani

Akapambane na Salim mwalim au pesa za manunuzi alishahonga au?
 
Eti anaomba radhi kwa kuwashinda kwa kishindo!!!!!! Hizo ni kejeli aisee....manaake wao si chochote si lolote kwake....baada ya kushinda kwa kishindo akawacheka tena maana aliwapa kadi tu wao wamempa nafasi ya kugombea ubunge na pesa....ha ha haa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwani 2015 alichaguliwa na masisiemu?
Hakika njaa haijawahi kumwacha mtu salama hasa mtulila.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naam Mkuu na hapa kutakuwa na wizi wa hali ya juu kuhakikisha anashinda kwa gharama zozote zile vinginevyo lawama zote kwa uchwara na sera zake za kuwapa rushwa wachumia tumbo kisha kuwarusha juu ya wafia chama ili wawe wagombea.

Huyu ndie Kiongozi wa Mazwazwa Mkuu..
Yote anayoyasema hayatoki kwenye moyo wake..
Msukumo wa tumbo zaidi.
 
Kwa siasa za Tanzania lolote laweza kutokea.
Ikiwa tunaambiwa chama ni cha 'masikini' na 'wanyonge' sitegemei jipya toka kwa masikini na wanyonge
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huyo Mtulia ngoja asubiri kipigo cha aibu atakachopata tarehe 13 February.......

Ndipo hapo atakapoona ubaya wa usaliti, kwa kuwa ubunge atakosa na pesa alizokabidhiwa na CCM nazo zitakuwa zimeanza kwisha.....

Yatamkuta yanayoitwa majuto ni mjukuu.
 
Anatakiwa kuwaomba radhi wananchi wa kinondoni. Walimuamini lakini yeye kaliamini tumbo zaidi kuliko maslahi ya wapigakura wake.
 
Kutoka Dar es Salaam.
Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amewaomba radhi wanachama wa chama hicho tawala kwa ushindi wa kishindo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiwa CUF
Mtulia ametoa kauli hiyo leo Januari 21, mwaka 2018 wakati akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2015, Mtulia alishinda ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, lakini Desemba 2 mwaka jana alijivua uanachama wa chama hicho na kuhamia CCM, hivyo kupoteza sifa ya ubunge. Hata hivyo CCM kilimpitisha kugombea ubunge katika jimbo hilo
Huku akiviponda vyama vya upinzani Mtulia amesema, “Nawaomba msamaha kwa yote niliyowakwaza wakati wa kampeni na kushinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi 2015.”
"Mnisamehe mtoto wenu nimerudi nyumbani kwenye chama kubwa. Niliwapa kadi lakini mmeamua kunipa ubunge."
Amesema vyama vyote vya upinzani ni sawa na asasi za kiraia, kwamba ni tofauti na ilivyo CCM kwa madai kuwa wapinzani wanasaka pesa na si kusaidia wananchi
Alitaja sababu iliyomfanya kuhama CUF kwamba ni baada ya kuona viongozi wake wakuu hawaelewani, huku akisisitiza kuwa nje ya CCM ni sawa na kujenga ukuta.Mtulia aliambatana na wanachama wa CUF walioamua kujiunga na CCM na kukabidhiwa kadi.
Chanzo: Mwananchi
shithole!!!!!!
 
Back
Top Bottom