Mtukufu rais wetu na huu ni uongo?

Katiba mpya itamke wazi kwamba watoto wote wa viongozi wote wasome shule za serikali na si vinginevyo,wajinga hawa maana wanaweka watoto wetu kama katuni vile ili baadaye watutawale.
 
Ni picha za kusikitisha, ni vema viongozi wetu wakaacha siasa na kuelekeza nguvu ili kufikisha huduma muhimu kwa wananchi wa kawaida. Si ajabu huko kwenye shule hizo zahanati hakuna na kama ipo haina dawa au wataalam.
 
Bila shaka hii story na picha nazo zinatoka kiwandani kwa Jk (mtanzania mwenzetu) mmoja wa wamiliki wa viwanda tajwa.
 
Jamaa unanongwa wewe! yaani hutaki tu kukubali,nashauri JK awe anamualika mpika uongo mashughuli katika uzinduzi wa miradi.
Miradi gani wanayozindua ya maana au kama ule wa Mwanza ambapo Pinda katumia zaidi ya magari 50 kwenda kuzindua mradi wa ufugaji nyuki miznga 20?............ Useless!!!
 
Unapodharau elimu kwa wananchi ndipo unapoishiwa na hawa air head..aibu kwa nchi yenye utajiri mkubwa ikiendelea kuwasomesha wanafunzi katika majengo primitive kama haya. Waziri hujisikiaje anapowatembelea na gari lake la millions huku wadau wa sekta yenyewe hali hiyo.
 
Nchi yetu imebarikiwa sana. Hakika viongozi wake watalipwa kwa uongozi wao mbovu
 
Miradi gani wanayozindua ya maana au kama ule wa Mwanza ambapo Pinda katumia zaidi ya magari 50 kwenda kuzindua mradi wa ufugaji nyuki miznga 20?............ Useless!!!

wewe umeifanyia nini nchi hii tangu uzaliwe zaidi ya kujaza tu choo
 
Ni picha za kusikitisha, ni vema viongozi wetu wakaacha siasa na kuelekeza nguvu ili kufikisha huduma muhimu kwa wananchi wa kawaida. Si ajabu huko kwenye shule hizo zahanati hakuna na kama ipo haina dawa au wataalam.

badala ya kuchangisha wananchi pesa kwa ajili ya maandamano,tusiwanyanganye hizo pesa wachangie miradi ya maendeleo kama ujenzi wa madarasa na kununulia madawati
 
dah ... sasa naanza kuamini kwamba EL ndiyo kichwa cha ccm kwa kauli yake ya "elimu kwanza"
 
Hayo madarasa ya makuti na miti yalijengwa kwa muda ili kukabiliana na tishio la kimbunga na kama unavyojua tena ndugu yangu watoto wote wangekufa iwapo wangeangukiwa na matofali
 
wewe umeifanyia nini nchi hii tangu uzaliwe zaidi ya kujaza tu choo
huwezi kujua ni kitu gani nilichoifanyia nchi hii kwa kutazama haya maandishi dogo!!.................hata hivyo ujifunze kutumia maneno mazuri, wengine humu ni wazazi wako ila muda mwingine akina Mama huwa wanafanya makosa kutowaambieni ukweli nyie watoto.
 
Duu hakujua analosema, Bora Mkapa alikuwa anajisifu kwa kutumia kodi za wananchi kujenga barabara...akalipa madeni mpaka akasamehewa...mkate ulikuwa sh 250, cement sh 5000, dah alafu ****** anajisifu kwa mikopo ya world bank na Nssf. Kiufupi anaturudisha tulikotoka....

Fedha Uswiss, EPA, Richmond, na mengineyo ni uongo??? Acha siasa ****** watu wanauelewa...
 
Jk kaka kweli una huruma na watoto wa taifa hili kweli leo hii miaka hamsini ya uhuru bado tunaishi katika hali nhii kweli vijana wetu hawana mahali pa kusomea wanasomea kwenye mahema ya miti na bado wanasoma wakiwa wamekaa chini kweli this is too much harafu ukukosolewa unasema ya kuwa watu wana vyuo vya uongo sasa unataka wasiseme ubovu ulionao. kiukweli nimeangalia picha za wadogo zetu wa shule za msingi hali inatisha siyo nzuri hata kidogo kama unavyounda kikosi kazi basi pia unda kwa ajili ya kushughulikia suala la elimu ya watoto wa maskini
 
Unamwambia nani? Kichwa cha nazi hiki? Wewe unafikiri hajui kinachoendelea kwa watoto wa shule za walazwahoi? Tena sio vijijini tu, hii hali hadi shule za Dar es salaam. Anajua sana, waziri wake wa elimu anajua sana, kabineti nzima inajua, wabunge wanaowakilisha majimbo hayo wanajua sana lakini ndio hivyo tena - ama 'tuingie msituni' (tujiunge M4C) au tusubiri hadi siku ya Kiama! Hawa watoto wakielimishwa vizuri kuwa huu ni uvunjifu wa haki za kibinadamu achilia mbali Katiba ya nchi, wataelewa na wakifikia umri wa kupiga kura watajiunga na wale wanaopigania haki za binadamu!!
 
Back
Top Bottom