NA HUU NAZANI UTAKUWA NI UONGO AU NI PHOTO SHOP
Naanza kuamini watanzania tunaweza tukawa tumelaaniwa, hivi ulichokifanya hapo umekielewa lakini? Mhe. Rais ajasema kwamba amemaliza matatizo yote yanayohusu elimu, kuanzia madarasa, vifaa vya kufundishia na uhaba wa walimu.
Wala hakusema amekausha na kumaliza kero na matatizo mbalimbali yanayokabili taifa, kama vile huduma za afya, ulinzi na usalama, upatikanaji na ugawaji wa maji safi na salama, upatikanaji wa chakula cha kutosha na ziada ya kushangaza, huduma za usafiri na mambo mengine mengi yanayokwaza maendeleo.
Uongo aliouongelea ni kitendo cha baadhi ya wana-siasa kutumia majukwaa vibaya, kwa kuishiwa kwao sera na kwa kuwa na sera nzee zilizo choka na kufubaa, zisizo sikilizika wala kutekelezeka, kuanza kutumia uongo kujipamba kisiasa.
Hii imekuwa desturi na tamaduni ya CHADEMA kudanganya umma katika mambo mbalimbali ili kujenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.
Hapa ningetoa RAI yangu kwa umma wa watanzania kuwa, kila wanapoambiwa jambo na hawa wazushi wa mambo wawe wanaomba uthibitisho. Hii ndio dawa na mwarubaini wa waropokaji kama walivyo CHADEMA.
Rai yangu kwa CHADEMA ni kutaka kuwasisitiza ya kwamba, muda, umaarufu na rasilimali walizonazo wao kwa sasa walikuwa nazo NCCR-MAGEUZI, UDP na CUF. VISIWATIE JEURI.