'Mtuhumiwa,wenzake walisheherekea kuvunja kanisa' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Mtuhumiwa,wenzake walisheherekea kuvunja kanisa'

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  SHAHIDI wa tatu katika kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya mfanyabiashara wa zamani wa Rwanda, Gaspard Kanyarukiga (64), amedai katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwamba mtuhumiwa huyo na washirika wake, walisherehekea kwa kunywa bia na mvinyo, baada ya kubomolewa kwa Kanisa la Parokia ya Nyange, wilayani Kivumo, Kibuye Aprili 16, 1994.

  Shahidi huyo aliyetambuliwa kwa jina bandia la CBK alidai jana kuwa, alishuhudia Kanyarukiga akishauriana na viongozi katika Kanisa la Nyange akiwamo Paroko wa Kanisa hilo Padri Athanase Seromba (yuko jela), Inspekta wa Polisi Fulgence Kayishema na viongozi wengine na kisha kuamuru kubomolewa kwa kanisa lililokuwa linahifadhi wakimbizi wa kitutsi wapatao 2000.

  “Baada ya kumaliza kubomoa kanisa, walikwenda kupumzika na viongozi waliingia ndani ya nyumba ya mapadri kusherehekea kwa kunywa bia na mvinyo,’’ CBK ambaye alikuwa anaongozwa katika ushahidi wake na mwendesha mashtaka, Arthia Alexis aliliambia jopo la majaji watatu waliokuwa wanamsikiliza.

  Kwa mujibu wa shahidi huyo, miongoni mwa viongozi waliokuwa wanasherehekea ni pamoja na mtuhumiwa Kanyarukiga, Padri Seromba, Kayishema na viongozi wengine ambao hakuweza kuwakumbuka majina.

  Upande wa utetezi ulianza kumhoji shahidi huyo mara baada ya mwendesha mashtaka kuhitimisha mahojiano naye.

  Mwendesha mashtaka anatarajia kuita mashahidi 10 kuunga mkono hoja zake.

  Kanyarukiga alitiwa mbaroni Afrika Kusini Julai 2004, anatuhumiwa kushiriki mauaji ya kimbari katika mkoa wa Kibuye, Magharibi mwa Rwanda . Alikana mashtaka yanayomkabili.

  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3506
   
Loading...