Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

Shukrani, nashukuru kwa kweli na najivunia kwa haya malezi wazazi wangu wamenipatia ndio nayaishi kwangu

Nashukuru umeelewa sasa kwamba binadam hatufanani
 
Kwani hapa tunaongelea kumpanda kichwani au kumtia moyo? Mimi binafsi mume awe na pesa asiwe na pesa unyenyekevu wangu kwake uko pale pale mimi siwezi kushindana na mwanaume ila kama wakati ana pesa alikuwa hanisaidii chochote na alikuwa ananisaliti siku zikimuishia kwanini ndo anikumbuke mimi?

Wanaume bwana yaani mnahangaikaga na michepuko huko nje mnasingizia kwamba sisi wake zenu ndo tunawafanya mchepuke ila yakitokea ya kutokea hiyo michepuko yenu ikiwakimbia ndo mnajifanya kurudi kwa wake zenu wawatie moyo kwanini na kipindi mambo yakiwa magumu msiende kwa hiyo michepuko yenu mliyokuwa mnaihonga kuliko wake zenu?
 
Mbona hata wanaume mna tabia ya kutulinganisha wanawake? Tofauti ni kwamba ninyi hamsemagi mnafanyaga tu vitendo ila sisi tunasemaga tu na hatufanyi vitendo mfano unakuta mwanamke wako labda mpole na mnyenyekevu lakini ni mbaya kisura na siyo mvumilivu ila unakutana na mwanamke mwingine mpole, mnyenyekevu, mzuri na mvumilivu

Sema tu ukweli kutoka moyoni mwako wewe hautamuacha huyo wa kwako ukaenda kwa huyo mwingine? Sasa ndo muone changamoto tunazokutana nazo sisi wanawake yaani mfano mwanaume wangu anajua kujali lakini hana pesa halafu ninakutana na mwanaume mwingine anayejua kujali na ana pesa wewe unadhani sitamtaka huyo mwanaume mwingine?

Nitamtaka ila tu sitahitaji kuwa naye na nitabaki nakwambia tu ufanye kama yeye na mara nyingi hizo zinakuwaga ni kauli tu lakini huwa hatumaanishi kutoka moyoni nimesema mara nyingi siyo mara zote na sisi ni binadamu kama ninyi yaani wanaume ninashindwaga kuwaelewa mnapotakaga wanawake wakamilifu

Yaani hamtakagi wanawake wenye kasoro hata moja sijui aliyewadanganya kuwa dunia hii kuna mkamilifu ni nani basi waumbeni ninyi wenyewe hao wanawake mnaowataka maana hata Mungu aliyetuumba anatuelewa na mapungufu yetu sasa sijui ninyi wanaume ni akina nani mnaolazimisha wanawake tuwe wakamilifu
"Tatizo umezubaa sana, kuwa kama James huoni mwenzio atafika mbali sana yule"
 
Ndiyo wanawake wa kibongo tumeumbwa kuhudumiwa tu kwa sababu majukumu yetu hamtaki kutusaidia hao wanawake wa kizungu ambao wanahudumiana sawa na waume zao hata hao waume zao wanawasaidia majukumu yao yaani hapo ni mgawanyo tu wa majukumu sasa ni kuchagua moja kati ya hayo mawili tu

Ni either tuwaige wazungu completely na siyo partially eti kutaka wanawake tu ndo tuanze kuhudumia wanaume ila wanaume wasitake kusaidia kazi za nyumbani au tuendelee na mila na desturi za kiafrika ambazo mwanaume ndo anatafuta pesa na kuhudumia mke na watoto na mwanamke ndo anafanya kazi za nyumbani na kulea mume na watoto
kmmmae yani balaa sana. Wanawake wa kibongo wameumbwa kuhudumiwa tu. Wakikosa huduma ni vita kali ya taarabu!
 
Kimila za kiafrika itapendeza zaidi..😂😂😂
 
Sasa ukiwa na Reception Jau Jau kwanini usumbue watu😃😃😃 ukiwa na sura ya Ndali~yours inabidi uwe mpole sio kiherehere kama mfukobwa shati
 
Dah kiukweli uliyo yasema hapa kama ni kweli basi nimpe hongera zake huyo jamaa kwamba kapata mwanamke mwenye sifa za kuitwa mke.
Lakini ukweli ni kwamba ni wanaume wengi sana wamajikuta wakikimbiwa na wake zao ama wapenzi wao kwasababu ya kuteteleka kiuchumi, mara nyingi sana wanawake wamekuwa si watu wavumilivu katika suala la ugumu wa maisha unapowakuta wenza wao.
Hili la kusema maisha ni kupanda na kushuka wanao lijua ni wachache sana.
Hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa ama mahusiano kwa lengo la kulelewa au kuhudumiwa na si kujenga familia, yaani familia kwao ni jambo la pili lakini kubwa kwake ni kupata huduma.
Siwalaumu kwasababu ni jukumu la mume kulea familia yake lakini wanawake wanapaswa kutambua kwamba maisha hayawezi kuwa sawa siku zote. Usimdharau masikini unae muona leo huwezi jua kesho atakuwaje.
 
Nakuamini sana lakini kwa hili nadhani uliangalie upya, kama ni hivi basi kuna uwezekano mkubwa wa mke kufanya hata hila za kumuangusha mumewe ili amkomoe.
Kwahiyo mume alikukosea kipindi akiwa na pesa ukamvumilia ila umeshindwa kumvumilia wakati hana pesa, hii inamaana kwamba unachokitaka kwake ni pesa na si vingine kama si hivyo basi ungemvumilia pia kipindi ambacho hana pesa.

Alafu ikitokea akapata tena pesa je arudie tena kukunyanyasa kwasababu ulimdharau wakati wa hali ngumu?.
Huoni kwamba huu ni wakati pekee wa kumbadilisha mumeo ajifunze kuijua thamani yako kwa khwa naye karibu ili asije rudia yale mabaya badala ya kumkomoa.
 
Kwahiyo kumbe wanaume wengi wanapooa wanakuwa hawajui thamani ya mwanamke bali wanaoa ili wake zao wakawafundishe huko huko ndoani? Aise kuna wanawake wana huruma jamani yaani wanakubali kuolewa na wanaume wasiojua thamani ya mwanamke?

Hivi ninyi wanaume mnaweza kuoa wanawake ambao hawajui thamani ya mwanaume na mkwafundisha huko huko ndoani? Siyo ninyi mnaotakaga wanawake ambao ni ready-made kitabia? Sasa mbona sisi tukitaka wanaume ambao ni ready-made kiuchumi mnatuona kama vile hatuna mapenzi ya dhati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…