Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

IKWETA KONZO M

IKWETA KONZO M

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Messages
305
Points
1,000
IKWETA KONZO M

IKWETA KONZO M

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2013
305 1,000
Stephen King ,mtu maarufu kwa uandishi wa Vitabu duniani aliwahi kukataliwa Kazi zake Mara nyingi.

Aliwahi kwenda kwa wachapishaji (Publishers) wa Vitabu 30 wakikataa Kazi zake kwamba hazikuwa na ubora .

Hali hii ilimfanya aanze kukata tamaa na mafanikio.

Akiwa katika hali ya kukata tamaa aliambiwa neno kubwa na mke wake " *Mume wangu ,tusikate tamaa tuendelee kutafuta wachapishaji wengi ipo Siku tutafanikiwa tu* "

Kutokana na hilo neno la mke wake lililomtia nguvu na ujasiri aliendelea kutafuta hatimaye akapata.

Stephen King ameandika vitabu 58 na stori fupi zaidi ya 200 .

Stephen King ameshauza nakala za vitabu milioni 350 duniani mpaka sasa .

Tafiti zinaonesha kwamba Stephen King ni tajiri wa 5 katika waandishi wa vitabu duniani mwaka 2019 , akiwa na dolla million 400.


Hakika hakuna safari isiyo na changamoto katika maisha isipokuwa lazima uangalie aina ya mtu unayesafiri naye.

Mke wa Stephen King alimwambia mume wake hivi akafanikiwa


*Mume wangu ,tusikate tamaa tuendelee kutafuta wachapishaji wengi ipo siku tutafanikiwa tu*

Je, mke wako anakwambiaje unapokwama , mume wako anakwambiaje ukikwama ? Ndugu, jamaa na rafiki zako wanakwambiaje ukikwama?

Hakikisha unasafiri na mtu anayeona matatizo kwa jicho la mafanikio.

*You're the Sperm that won the race*

#Nanauka
 
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
38,335
Points
2,000
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
38,335 2,000
Muangalie fulani ana biashara nzuri, yule binti amewajengea wazazi wake nyumba, yule mliyesoma nae ana watoto wawili, kijana yule kawawekea wazazi wake mashine ya kusaga, wewe unakwama wapi? Hayo ndio maneno tunaambiana
 
BradFord93

BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Messages
429
Points
1,000
BradFord93

BradFord93

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2017
429 1,000
Wanawake wa kibongo wanajua kulinganisha na watu wengne....utakachoambiwa n kuwa "siwezi kuishi na mwanaume asyeweza kunihudumia"

Hpo itafuata dharau...kejeli....michepuko na mwsho kibuti ndiii

Wanawake wa kibongo hasa kipindi hiki cha magu co watu wa kupanga nao maisha...!!atakuchuna pesa mpk ngozi kabsaaaa
 
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
38,335
Points
2,000
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
38,335 2,000
Wanawake wa kibongo wanajua kulinganisha na watu wengne....utakachoambiwa n kuwa "siwezi kuishi na mwanaume asyeweza kunihudumia"

Hpo itafuata dharau...kejeli....michepuko na mwsho kibuti ndiii

Wanawake wa kibongo hasa kipindi hiki cha magu co watu wa kupanga nao maisha...!!atakuchuna pesa mpk ngozi kabsaaaa
Saa kama huwezi kuhudumia mke kwa nini uoe?
 

Forum statistics

Threads 1,315,270
Members 505,171
Posts 31,851,972
Top