Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

Shukrani, nashukuru kwa kweli na najivunia kwa haya malezi wazazi wangu wamenipatia ndio nayaishi kwangu

Nashukuru umeelewa sasa kwamba binadam hatufanani
bila shaka umelelewa kwenye malezi mazuri ya kiislamu na walezi wako waliishi kama mfano wa kuigwa na wewe. Niombe radhi kwa kuku group pamoja na wenzako wengi humu ambao wanafanana kimtazamo kutokana na comments zao ninazozionaga mara kwa mara humu inapokuja mada kama hii.
Kama kweli unafanya haya uliyoyaandika hapa katika maisha halisi basi big up sana kwa huyo kidume uliyenaye, ameokota dodo chini ya mkaratusi.
Maisha hayako uniform hata kidogo lazima kuna kukwama mahali, sasa kwenye kukwama ndio tunaona maana ya vile viapo vya siku ya ndoa. Bahati mbaya sana wenzako wengi ukicheki mitazamo yao unagundua kuwa hivi viapo hawawezi kuviishi. Ila kwako wewe unaonekana unajua maana halisi ya companionship kwa mujibu ya maelezo yako.
Endelea hivyo hivyo kutofungamana na upande wowote usiokuwa sahihi nimekupenda ghafla.
 
Kwani hapa tunaongelea kumpanda kichwani au kumtia moyo? Mimi binafsi mume awe na pesa asiwe na pesa unyenyekevu wangu kwake uko pale pale mimi siwezi kushindana na mwanaume ila kama wakati ana pesa alikuwa hanisaidii chochote na alikuwa ananisaliti siku zikimuishia kwanini ndo anikumbuke mimi?

Wanaume bwana yaani mnahangaikaga na michepuko huko nje mnasingizia kwamba sisi wake zenu ndo tunawafanya mchepuke ila yakitokea ya kutokea hiyo michepuko yenu ikiwakimbia ndo mnajifanya kurudi kwa wake zenu wawatie moyo kwanini na kipindi mambo yakiwa magumu msiende kwa hiyo michepuko yenu mliyokuwa mnaihonga kuliko wake zenu?
Kwa hiyo kumbe mwanaume anayekunyanyasa kipindi akiwa na hela, siku akiporomoka kiuchumi hakuna sababu ya kumsaidia kivyovyote vile bali huo ndio muda wako na wewe wa kumpanda kichwani..? halafu siku akirudi kwenye hali nzuri ya awali na wewe unarudi kwenye unyenyekevu na uvumilivu kama mwanzo tu sio?
 
Mbona hata wanaume mna tabia ya kutulinganisha wanawake? Tofauti ni kwamba ninyi hamsemagi mnafanyaga tu vitendo ila sisi tunasemaga tu na hatufanyi vitendo mfano unakuta mwanamke wako labda mpole na mnyenyekevu lakini ni mbaya kisura na siyo mvumilivu ila unakutana na mwanamke mwingine mpole, mnyenyekevu, mzuri na mvumilivu

Sema tu ukweli kutoka moyoni mwako wewe hautamuacha huyo wa kwako ukaenda kwa huyo mwingine? Sasa ndo muone changamoto tunazokutana nazo sisi wanawake yaani mfano mwanaume wangu anajua kujali lakini hana pesa halafu ninakutana na mwanaume mwingine anayejua kujali na ana pesa wewe unadhani sitamtaka huyo mwanaume mwingine?

Nitamtaka ila tu sitahitaji kuwa naye na nitabaki nakwambia tu ufanye kama yeye na mara nyingi hizo zinakuwaga ni kauli tu lakini huwa hatumaanishi kutoka moyoni nimesema mara nyingi siyo mara zote na sisi ni binadamu kama ninyi yaani wanaume ninashindwaga kuwaelewa mnapotakaga wanawake wakamilifu

Yaani hamtakagi wanawake wenye kasoro hata moja sijui aliyewadanganya kuwa dunia hii kuna mkamilifu ni nani basi waumbeni ninyi wenyewe hao wanawake mnaowataka maana hata Mungu aliyetuumba anatuelewa na mapungufu yetu sasa sijui ninyi wanaume ni akina nani mnaolazimisha wanawake tuwe wakamilifu
"Tatizo umezubaa sana, kuwa kama James huoni mwenzio atafika mbali sana yule"
 
Ndiyo wanawake wa kibongo tumeumbwa kuhudumiwa tu kwa sababu majukumu yetu hamtaki kutusaidia hao wanawake wa kizungu ambao wanahudumiana sawa na waume zao hata hao waume zao wanawasaidia majukumu yao yaani hapo ni mgawanyo tu wa majukumu sasa ni kuchagua moja kati ya hayo mawili tu

Ni either tuwaige wazungu completely na siyo partially eti kutaka wanawake tu ndo tuanze kuhudumia wanaume ila wanaume wasitake kusaidia kazi za nyumbani au tuendelee na mila na desturi za kiafrika ambazo mwanaume ndo anatafuta pesa na kuhudumia mke na watoto na mwanamke ndo anafanya kazi za nyumbani na kulea mume na watoto
kmmmae yani balaa sana. Wanawake wa kibongo wameumbwa kuhudumiwa tu. Wakikosa huduma ni vita kali ya taarabu!
 
Ndiyo wanawake wa kibongo tumeumbwa kuhudumiwa tu kwa sababu majukumu yetu hamtaki kutusaidia hao wanawake wa kizungu ambao wanahudumiana sawa na waume zao hata hao waume zao wanawasaidia majukumu yao yaani hapo ni mgawanyo tu wa majukumu sasa ni kuchagua moja kati ya hayo mawili tu

Ni either tuwaige wazungu completely na siyo partially eti kutaka wanawake tu ndo tuanze kuhudumia wanaume ila wanaume wasitake kusaidia kazi za nyumbani au tuendelee na mila na desturi za kiafrika ambazo mwanaume ndo anatafuta pesa na kuhudumia mke na watoto na mwanamke ndo anafanya kazi za nyumbani na kulea mume na watoto
Kimila za kiafrika itapendeza zaidi..😂😂😂
 
Mbona hata wanaume mna tabia ya kutulinganisha wanawake? Tofauti ni kwamba ninyi hamsemagi mnafanyaga tu vitendo ila sisi tunasemaga tu na hatufanyi vitendo mfano unakuta mwanamke wako labda mpole na mnyenyekevu lakini ni mbaya kisura na siyo mvumilivu ila unakutana na mwanamke mwingine mpole, mnyenyekevu, mzuri na mvumilivu

Sema tu ukweli kutoka moyoni mwako wewe hautamuacha huyo wa kwako ukaenda kwa huyo mwingine? Sasa ndo muone changamoto tunazokutana nazo sisi wanawake yaani mfano mwanaume wangu anajua kujali lakini hana pesa halafu ninakutana na mwanaume mwingine anayejua kujali na ana pesa wewe unadhani sitamtaka huyo mwanaume mwingine?

Nitamtaka ila tu sitahitaji kuwa naye na nitabaki nakwambia tu ufanye kama yeye na mara nyingi hizo zinakuwaga ni kauli tu lakini huwa hatumaanishi kutoka moyoni nimesema mara nyingi siyo mara zote na sisi ni binadamu kama ninyi yaani wanaume ninashindwaga kuwaelewa mnapotakaga wanawake wakamilifu

Yaani hamtakagi wanawake wenye kasoro hata moja sijui aliyewadanganya kuwa dunia hii kuna mkamilifu ni nani basi waumbeni ninyi wenyewe hao wanawake mnaowataka maana hata Mungu aliyetuumba anatuelewa na mapungufu yetu sasa sijui ninyi wanaume ni akina nani mnaolazimisha wanawake tuwe wakamilifu
Sasa ukiwa na Reception Jau Jau kwanini usumbue watu😃😃😃 ukiwa na sura ya Ndali~yours inabidi uwe mpole sio kiherehere kama mfukobwa shati
 
Kama vile mnavotuweka kwenye mkumbo mmoja na sie

Kwanza uelewe wengine humu hatufungamani na upande wowote na hua tunachangia vile kutokana na mada husika na si kila mada utachangia uonekane umechangia

Pili elewa kua binadamu hatufanani kama vidole usikandamize wala kulazimisha kutuweka kwenye mzani sawa ili tu kile ulichojiwekea akili kiwe ndicho badili mfumo wa fikra akilini mwako tupo wanawake tuna ndoa zetutunajielewa na wapo wasokua na ndoa zao na wanajielewa vile vile

Samahani sana na nikuambie tu mimi mume wangu naamini ndio mtu ambae anaweza tukashare mambo bila kificho sitaki kujua ananificha au la lakini ile tu mke wangu kuna kadha wa kadha nisaidie ushauri au unashauri vipi kwangu me naona nimethaminika na natoa ushauri wangu kama inavyopaswa

Halaf si kua mtaishi kwenye ndoa au mahusiano kila siku mtapata fedha, au kila siku mahela yanaingia kuna leo na kesho maisha ni kupanda na kushuka, akikosa bas sitaacha kumfariji sababu najua anatafta japo na mie natafta tusaidiane lakini naelewa ye kama baba ndio kichwa cha nyumba nikianza kumkatisha tamaa tutaishi vipi?? Lazima nimpe moyo kwanza nilivyo sipendi kumuona ana sononeka et kisa mambo hayaendi sawa wakat mimi ndio mkewe naweza mpa moyo nikamfariji hivo elewa tu kama wema upo na ubaya upo bas wanawake wenye sifa nzuri wapo vile vile
Dah kiukweli uliyo yasema hapa kama ni kweli basi nimpe hongera zake huyo jamaa kwamba kapata mwanamke mwenye sifa za kuitwa mke.
Lakini ukweli ni kwamba ni wanaume wengi sana wamajikuta wakikimbiwa na wake zao ama wapenzi wao kwasababu ya kuteteleka kiuchumi, mara nyingi sana wanawake wamekuwa si watu wavumilivu katika suala la ugumu wa maisha unapowakuta wenza wao.
Hili la kusema maisha ni kupanda na kushuka wanao lijua ni wachache sana.
Hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa ama mahusiano kwa lengo la kulelewa au kuhudumiwa na si kujenga familia, yaani familia kwao ni jambo la pili lakini kubwa kwake ni kupata huduma.
Siwalaumu kwasababu ni jukumu la mume kulea familia yake lakini wanawake wanapaswa kutambua kwamba maisha hayawezi kuwa sawa siku zote. Usimdharau masikini unae muona leo huwezi jua kesho atakuwaje.
 
Tatizo wanaume hamuangaliagi mambo mnayowafanyia wake zenu kipindi mna pesa ila kipindi hamna pesa ndo mnaanza kuangalia mambo wanayowafanyia wake zenu hakuna mwanamke ambaye ulikuwa unamsaidia na haumsaliti halafu yeye akaja kukuvunja moyo ukija kupata shida labda awe na roho mbaya tu ila kama wakati una pesa ulikuwa haumsaidii na unamsaliti kwanini na wewe utake akutie moyo kipindi ukiwa hauna pesa?
Nakuamini sana lakini kwa hili nadhani uliangalie upya, kama ni hivi basi kuna uwezekano mkubwa wa mke kufanya hata hila za kumuangusha mumewe ili amkomoe.
Kwahiyo mume alikukosea kipindi akiwa na pesa ukamvumilia ila umeshindwa kumvumilia wakati hana pesa, hii inamaana kwamba unachokitaka kwake ni pesa na si vingine kama si hivyo basi ungemvumilia pia kipindi ambacho hana pesa.

Alafu ikitokea akapata tena pesa je arudie tena kukunyanyasa kwasababu ulimdharau wakati wa hali ngumu?.
Huoni kwamba huu ni wakati pekee wa kumbadilisha mumeo ajifunze kuijua thamani yako kwa khwa naye karibu ili asije rudia yale mabaya badala ya kumkomoa.
 
Kwahiyo kumbe wanaume wengi wanapooa wanakuwa hawajui thamani ya mwanamke bali wanaoa ili wake zao wakawafundishe huko huko ndoani? Aise kuna wanawake wana huruma jamani yaani wanakubali kuolewa na wanaume wasiojua thamani ya mwanamke?

Hivi ninyi wanaume mnaweza kuoa wanawake ambao hawajui thamani ya mwanaume na mkwafundisha huko huko ndoani? Siyo ninyi mnaotakaga wanawake ambao ni ready-made kitabia? Sasa mbona sisi tukitaka wanaume ambao ni ready-made kiuchumi mnatuona kama vile hatuna mapenzi ya dhati?
 
50 Reactions
Reply
Back
Top Bottom