Mtu na dada yake wamejaliwa uzuri

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,511
40,598
Mnavyojua tena wakuu, mimi huwa napenda vitu vizuri vizuri vyenye mng'ao mng'ao, na vinavyotamanisha kuliwa.

Kuna kipindi nilikuwa kwenye mahusiano, na mlimbwende mmoja na tulidumu kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitatu hivi; katika uhusiano wetu tulifanikiwa kupata mtoto, na kwa sasa naendelea kuhudumia katika matunzo.

Kwa bahati nzuri huyu mrembo, ana dada yake ambaye naye pia ni kifaa kweli kweli. Nikiwa kwenye mahusiano na mdogo wake, kuna muda tulikuwa tunatoka naye 'out' yeye, mdogo wake pamoja na mimi.

Imepita zaidi ya miezi sita bila kuwa na mawasiliano na huyu dada mtu; sasa leo mtoto wangu alipelekwa na mama yake aende kwa mama yake mkubwa ili acheze na mtoto wa hapo, kwa sababu sasa hivi shule zimefungwa.

Mimi sijui hili wala lile, leo nikapigiwa simu na namba ambayo siijui;baada ya kupokea, nasikia sauti ya mwanamke, nami nikawa namjibu tu kama namfahamu; ndipo akaniuliza unajua unaongea na nani, nikamjibu naomba unikumbushe; ndipo aliponiambia mimi ni fulani, nimemuona mtoto wako hapa nikakukumbuka.

Tuliongea naye kama dakika 25 hivi; kutokana na sauti yake nikivuta picha na umbo lake, akili ikaniambia nitafute siku angalau nichakate hii kitu.

Sasa wakuu, hapa nawaza; nikiichakata hii kitu haiwezi kunipa shida kwa malezi ya mtoto wangu?, Hasa pale akiwa mkubwa, na kujua nilitoka na mama yake mkubwa?
 
Ama kwer hii Tanzania tushauzwa kumbe ni kwer haijawai tokea mtu kumtaka dada mtu kwa kupagawishwa na figure ya familia husika acha upuuzi lete madini ya kimaendeleo sio kukaa unatuwazisha ngono🚶
Njoo tujadili namna ya kufungua kiwanda cha kutengeneza vifaru na ndege za kivita; tukiwauzia huko nje tutapata fedha nyingi za kigeni, na uchumi utapaa sana.
 
Back
Top Bottom