Mtu kama huyu anafaa kuwa boss?

Furaha Fedson

Member
Mar 27, 2011
43
4
Jamani wana JF, nina boss wangu mmoja simuelewi anamatatizo au ndo uongozi ulivyo? huyu mheshimiwa anatabia zifuatazo: - hana siri kabisa, likijiri jambo ofsini kwake lazima kila mtu ajue - kazi yake ni kufukuzisha watumishi na kuajiri maswaiba - kama mtumishi anamatatizo ya kifamilia, mfano migogoro ya kifamilia, akijua tu basi linahamia ofisini kwake - hufokea watumishi wenzake bila aibu, akiambiwa si vema afanyavyo anadai eti anasauti ya uinjilisti! tumzoee JE? MTU KAMA HUYU ANAFAA KUWA KIONGOZI?
 
Mtu kama huyo si kiongozi kwani kiongozi yeyote lazima awe na sifa ya ujasiri huyo si mjasiri ndio maana ana kelele sana
 
huyo si kiongozi ni kama ka-meneja hivi. hiyo ni office ya umma au private kwa shakt kapoor?
 
huyo si kiongozi ni kama ka-meneja hivi. hiyo ni office ya umma au private kwa shakt kapoor?

Ha ha ha ha ...kwr kwi kwi kwi kwi.....nakufa mbavu zangu!!! Siku yangu imekuwa na itakuwa nyeupe!!! Kwa shakt kapoor unamaanisha kwa wahindi bila shaka...!
 
Twende mbali zaidi, je katika taasisi yenu tija imeongezeka ama imepungua ndani ya uongozi wake. Kama ufanisi miongoni mwa wafanyakazi itabidi awe model kwa viongozi wengine:help:
 
Kila mtu anafaa kuwa kiongozi ila huyu boss wako hafai kuwa Boss wako kwa tabia zake na nyie mnaendelea kumkumbatia kwa sasa...wanao-ongozwa nae ndio wanaomuweka hapo..wangekuwa hawamtaki angeshachapa malapa siku mingi. hebu shirikianeni wote mliopewa ajira hapo mpeleke malalamiko yenu kwa wakubwa wako muone kama watafuatilia. kwanza mtu kama huyu hajui kabisa ni nin maana ya kuwa kiongozi, sheria na maadili ya kuwa kiongozi...huyu hata nyumbani kwake hakuna familia yenye maadili..anachowafanyia nyie ndicho anachowafanyia hata familia yake na waliokaribu na yeye

Jamani wana JF, nina boss wangu mmoja simuelewi anamatatizo au ndo uongozi ulivyo? huyu mheshimiwa anatabia zifuatazo: - hana siri kabisa, likijiri jambo ofsini kwake lazima kila mtu ajue - kazi yake ni kufukuzisha watumishi na kuajiri maswaiba - kama mtumishi anamatatizo ya kifamilia, mfano migogoro ya kifamilia, akijua tu basi linahamia ofisini kwake - hufokea watumishi wenzake bila aibu, akiambiwa si vema afanyavyo anadai eti anasauti ya uinjilisti! tumzoee JE? MTU KAMA HUYU ANAFAA KUWA KIONGOZI?
 
Hafai kabisa anawaathiri kisaikolojia kwa intimidating voice n language. mtafutieni dawa.
 
Back
Top Bottom