Mtu anayefunza kompyuta kutambua harufu

Mtu anayefunza kompyuta kutambua harufu

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,314

_97580613_oshiagabi.jpg

Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.
Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.

Mfumo huo umefunzwa kutambua harufu ya vilipuzi na unaweza kutumiwa katika kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege, alisema.

Vilevile kifaa hicho kilicho na ukubwa wa modem na kupewa jina Koniku Kore kinaweza kuwa ubongo wa roboti za siku za usoni.

Kampuni kubwa za kiteknolojia, ikiwemo Google hadi Micrososft ziko katika harakati ya kutengeza roboti inayoweza kuwa na akili ya mwanadamu.

Huku kompyuta zikiwa bora kushinda mwanadamu katika kutatua hesabu ngumu, kuna majukumu mengi ambayo yanaweza kufanywa na ubongo wa mwanadamu ikiwemo kuifunza kompyuta kutambua harufu.

Bwana Agabi analenga kubadili baiolojia ya uhandisi ambayo tayari imetimiza uvumbuzi huo.''Biolojia ni Teknolojia''.

Kazi yetu kuu ni kujaribu kuiga ubongo.

Alizindua kifaa hicho cha koniku yapata mwaka mmoja uliopita na amefanikiwa kuchangisha dola milioni moja kama ufadhili na anasema kuwa kifaa hicho kimempatia dola milioni 10 katika mikataba na kampuni za usalama.

Koniku Kore ni kifaa kilichotengezwa kwa kutumia neva na silicon ambacho kina sensa zinazoweza kutambua harufu.

''Unaweza kuzipa neva hizo maelezo ya ni nini unachotaka zifanye ambapo upande wetu tunaziambia kutoa seli zinazoweza kutambua harufu'',alisema.

Chanzo: BBC
 
Hizi ndio akili kubwa - hongera zake. Kuna kitu wataalamu wakitusaidia watakuwa wametatua changamoto moja kubwa sana. Enzi hizo kwenye somo la fizikia ambalo niliachana nalo F.2 nakumbuka tulifundishwa theory moja muhimu sana: "Energy can neither be created nor distroyed but can be changed from one form to another". Na pia katika topic nyingine tukafundishwa "sound is a form of energy"; sorry inawezekana nimechapia ila idea ndio hiyo.

Sasa wataalamu watusaidie hili; I believe sauti za manabii na mitume wetu watukufu zingalipo in one or other form of energy. Wakiweza kuzi-capture na kuzirudisha katika original form possibly na picha itatusaidia sana. Tutamsikia na kumwona Jesus "live"; tutamwona Mtume Mohammad (SAW) "live"; na wengineo. Naamini kuna siku hii dream itafanikiwa. Mwenyezi Mungu na azidi kuwajalia vipawa watu wake vizazi kwa vizazi vijavyo; inshaallah iko siku.
 
Pathetic! what will it impact to this new development of science and technology?
 
Pathetic! what will it impact to this new development of science and technology?
Itamaliza ubishi na uongo mwingi. Wizi, ujambazi, na uhalifu wa kila aina utakwisha. Fikiria ikipatikana device ambayo inaweza ku-capture matendo na maneno ya mtu aliyofanya au kutamka siku za nyuma. Ukileta ubishi audio/video inawekwa hadharani.
 
Mkuu bila msaada wa video camera kurecord tukio, itakuwa ni upigaji ramri.
Labda uniambie kuwepo na namna mtu aingiziwe electronic chip ambayo itarecord matukio na matendo yote ya mhusika na yawe transmitted somewhere for future recall, kitu ambacho kinawezekana kabisa.
Kuhusu sauti ni rahisi kuchezewa kwa namna mtu atakavyo.

Lakini ku recall video na matendo ya watu wa kale, zama ambazo there was no enhanced devices ni kitu ambayo haiwezekani na sio big deal kuyajua ya wahenga katika zama hizi za uvumbuzi with more sophisticated technologies!
 
Back
Top Bottom