Mtu anaishi baada ya kufa?

Ghost boss

Member
May 3, 2019
33
56
MTU anaishi baada ya kufa?

Mara nyingi kume kuwa na mafundisho mengi ya upotoshaji, nazaidi wengi wao wakifanya kama alivyo Fanya shetani kutumia maandiko matakatifu kumjaribu Yesu mwanawa Mungu. Tumeona na kusikia habari mbali mbali juu ya nini utokea baada ya kifo.

Mara nyingi tumesikia MTU aliyekufa hajui lolote wengine ukifananisha kifo na usingizi.. Sasa tujiulize nini kinatoa uhai yaani kipi kinachofanya mwili uwe na utendaji? Imeandikwa Mungu baada ya kuumba mwili aliupulizia pumzi ya uhai. pumzi ya uhai ninini? Pumzi ya uhai ni roho... roho ndio itiayo uzima na roho ndio uhai kamili.

MTU hufa kwa sababu roho inapofika kikomo cha kuendelea kukaa ndani ya mwili dhaifu.. Roho inauhai na haina udhaifu ila mwili sio hai na nidhaifu.

Mwili unapokuwa umechoka sana na hauwezi kufanya tena Kazi zinazo amriwa na roho... Hapo roho utoka ndani ya mwili na kifo ndio hutokea... Baada ya roho kutoka katika mwili uendelea kuishi kwa nyakati zote kwakua Mungu alipotuumba tu alitupa umilele kwa kutujalia roho isiyo kufa... Pale bustanini kulikuwa na mti Wa uhai na kifo...

Mti Wa kifo ulikuwa maalumu ya kuharibu utdndaji Kazi Wa mwili na hivyo kulelekea mwili kushindwa kuendelea na utendaji na kupelekea kifo.. Ukiwa msomaji mzuri Wa biblia utaungana nami mkono pale Yesu aliposema roho ilazi lakini mwili ni dhaifu.. Alielezea jinsi gani mwili na roho vilivyovitu viwili tofauti

Roho ndio uhai..asiye elewa ajiulize. Nini kinafanya MTU aongee? Na nini ninafanya ashindwe kuongea au nini kinafanya MTU apumue na kipi kinafanya ashindwe? Kwa maana MTU hufa na hewa ikiwa imezunguka eneo lake lakini kwanini anakufa? Ndio maana nasema MTU hufa pale mwili unaposhindwa kutekeleza kile roho inachotaka kifanyike.

Je! Kuna uhai baada ya kifo....? Jibu ni ndio duniani mwili aupo ila roho IPO... Ushawahi kujiuliza kwanini wanaita mwili Wa .... Nasio Fulani? Jiulize mwenye mwili yupo wapi? Ukweli ni kuwa yupo mahali Fulani amekaa anaangalia na anaishi ila hana Kazi tena na mwili wake maana hauwezi tena...

Ndio maana tunaambiwa baada ya kufufuliwa tutapewa miili mipya isiyo na udhaifu ili isijeikashindwa Kazi roho ikaiacha tena..

Tunakufa kwakuwa mwili hauwezi kitu hapa ndio pale msemo Wa wafu awajui lolote unakuja..ishu ya wafu ni mwili ila roho ambaye ni Mimi nitasikia kwa wanadamu na eidha kwa wenzangu Wa roho eti kuwa nimekufa ila kimsingi nipo hai ila bila mwili..Leo tuishie hapa tupate mmeng'enyo wayale tuliyosoma
 
Ila JPM kama dk chache kabla ya kufa alifanya huduma ya maombi , mwamba sku ya mwisho kuna hatari akasepa mbinguni 😀😀...mana calculation za Mungu za ajabu sana , kukufutia issue zako za nyuma ni swala la robo sekunde tuu...! Nafas za wachache Sana hzo , za kujua it is almost home tyme duuh... Wengine tutakufa ghafla kabla hata hatujawekana Sawa na Mungu wetu ...
 
Ila JPM kama dk chache kabla ya kufa alifanya huduma ya maombi , mwamba sku ya mwisho kuna hatari akasepa mbinguni ...mana calculation za Mungu za ajabu sana , kukufutia issue zako za nyuma ni swala la robo sekunde tuu...! Nafas za wachache Sana hzo , za kujua it is almost home tyme duuh... Wengine tutakufa ghafla kabla hata hatujawekana Sawa na Mungu wetu ...
 
Ila JPM kama dk chache kabla ya kufa alifanya huduma ya maombi , mwamba sku ya mwisho kuna hatari akasepa mbinguni 😀😀...mana calculation za Mungu za ajabu sana , kukufutia issue zako za nyuma ni swala la robo sekunde tuu...! Nafas za wachache Sana hzo , za kujua it is almost home tyme duuh... Wengine tutakufa ghafla kabla hata hatujawekana Sawa na Mungu wetu ...
Acha kujisemea mambo ya hatari maana kufa bila kuweka mambo sawa na Mungu nimajanga hayo..tuombe wakati wakifo tufanye upatanisho kwanza maana vngnevyo huwezi kuuona USO Wa Mungu..
 
MHU. :9:5
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa

MHU. :9:6
Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.

MHU. :9:10
Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe
 
Ila JPM kama dk chache kabla ya kufa alifanya huduma ya maombi , mwamba sku ya mwisho kuna hatari akasepa mbinguni 😀😀...mana calculation za Mungu za ajabu sana , kukufutia issue zako za nyuma ni swala la robo sekunde tuu...! Nafas za wachache Sana hzo , za kujua it is almost home tyme duuh... Wengine tutakufa ghafla kabla hata hatujawekana Sawa na Mungu wetu ...

Yeye amepata bahati na upendeleo wa Mungu kwa kweli.....

Mara Paap tuliobaki tunakufa halafu unamkuta mlangoni yeye ndio anakuonyesha pa kukaa 🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Bibilia inatuambia, “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kasha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe… Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena” (Ayubu 14:1-2,14)?

Kama vile Ayubu, karibu sisi sote tumekabiliwa na swala kama hili. Ni jambo gani hasa hutukia kwetu baada ya kufa? Je, ni kukosa kuwepo duniani tu? Je, maisha ni kufa na kufufuka tu ili tujipatie umaarufu tena duniani? Je, watu wote huenda mahali pamoja, au huenda mahali tofauti? Je, kunayo kweli Mbingu na Jehanamu, au ni maneno tu ya kujitungia?

Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia,wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).

Yesu alichukua adhabu aliyostahili kila mmoja wetu na akajitoa maisha yake. Siku tatu baadaye, akathibitisha ushindi wake juu ya mauti kwa kufufuka kutoka kaburini, katika roho na katika mwili. Alibaki katika dunia kwa mda wa siku arubaini na kushuhudiwa na maelfu ya watu kabla ya kupaa nyumbani kwake Mbiguni kwenye uzima wa milele. Warumi 4:25 yasema, “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu,na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.’’

Ufufuo wa Kristo lilikuwa ni jambo lililodhihirika Mtume Paulo aliwapatia watu changamoto kwamba wawaulize wale waliokuwapo wakati jambo hilo likitendeka wahakikishe kama jambo hilo si kweli. Hakuna aliyeweza kushindana juu ya ukweli huo. Ufufuo ndio msingi imara (jiwe la pembeni la) wa imani ya Mkristo; kwasababu Kristo alifufuka katika wafu, sisi pia tunaweza kuwa na imani ya kwamba tutafufuliwa.

Paulo aliwaonya wakristo wa kwanza ambao hawakuyaamini haya: “Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka” (Wakorintho 15:12-13).

Kristo alikuwa pekee wa kwanza kati ya mavuno makuu ya wale watakao inuliwa kutoka kwa wafu. kifo kiliingia duniani kuputia mtu mmoja, Adamu ambaye sisi sote ni wa ukoo wake. lakini wale ambao wamefanywa wana wa Mungu kupitia imani juu ya Yesu Kristo watapewa maisha mapya (Wakorintho wa kwanza 15:20-22). Kama vile Mungu alivyofufua mwili wa Yesu, vivyo hivyo ndivyo miili yetu itakavyofufuliwa Yesu atakaporudi (Wakorintho wa kwanza 6:14).

Ijapokuwa sote tutakuwa tumefufuliwa, hatutaenda sote mbinguni mahali pamoja. Mtu sharti afanye uamuzi wa kuchagua sasa juu ya mahali anapotaka kuenda kwa umilele wake. Bibilia inasema ya kwamba imetupasa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Wale waliotakaswa wataenda kwa uzima wa milele mbinguni, lakini wasioamini watapelekwa kwa hukumu ya milele ama jehanamu (Mathayo 25:46).

Jehanamu, kama vile mbinguni, si mahali patajwapo kwa utisho tu bali ni mahali dhahiri. Hapa ni mahali ambapo wasiohaki watakutana na ghadhabu isiyokoma ya Mungu. Watavumilia mateso ya kihisia, kiakili, na kimwili wakiwa katika akili zao timamu huku wakijihisi kuaibika na kujuta kwa matendo yao maovu.

Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na ziwa la moto, liwakalo na kiberiti amabpo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.

Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele? Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).

Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36). Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya kristo.
 
Jf nowdays....

Ume uliza swali au umetoa conclusion?

Nilidhani unakaribisha watu kwenye mjadala wa kujibu swali lako

Ungepata mchango mzuri Wenda kuliko hicho ulichoandika hapo
Unaruhusa kamili ya kuchangia maoni yako ila sio umuelekeze MTU Fulani na nimetoa mada hiyo kuwa eleza ukweli ulivyo kuepukka false doctrine za wapotoshaji..
 
Mkuu nakubaliana nawewe pasina chembe yenye kutia shaka,mwili ndo hufa ila roho haifi, ndo maana mwenyezi mungu anasema kwa sisi wakristo :-

Mathayo 10:28.

Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu.

So mwenye uwezo Wa kuua roho ni mungu pekee.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
🙏
 
eti roho haifi,upagani huo roho hupatikana baada ya mwili kupuliziwa pumzi ya uhai hivyo roho ni muunganiko wa pumzi ya uhai na mwili,pumzi ya uhai inapomtoka mtu inarudi kwa aliye itoa kwa hiyo roho inakuwa imevunjika kwani Ni matokeo ya muunganiko wa pumzi na mwili,kufundisha roho haifi Ni kukubaliana na shetani aliye sema hutakufa hakika.
 
Ijapokuwa sote tutakuwa tumefufuliwa, hatutaenda sote mbinguni mahali pamoja. Mtu sharti afanye uamuzi wa kuchagua sasa juu ya mahali anapotaka kuenda kwa umilele wake. Bibilia inasema ya kwamba imetupasa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Wale waliotakaswa wataenda kwa uzima wa milele mbinguni, lakini wasioamini watapelekwa kwa hukumu ya milele ama jehanamu (Mathayo 25:46).
Nimesoma maelezo yako lakini napingana na hiyo hoja yako hapo juu 👆.
Iko hivi; Binadamu hajahaidiwa MBINGU kama mahali atakapoenda kuishi baada ya maisha haya. Watakatifu hawakupewa ahadi ya kuishi Mbinguni kwa MUNGU. Biblia imeeleza wazi kabisa kuwa Watakatifu watairithi "nchi" yaani dunia mpya na siyo Mbinguni.
Ndiyo maana YESU atakuja duniani tena kuuleta Ufalme wa MUNGU hapa duniani na makao makuu ya Ufalme huo wa MUNGU yatakuwa Jerusalem. Siku YESU atakaporudi haji kuwachukua Watakatifu na kuwapeleka Mbinguni bali anakuja kuwafufua na kuishi nao hapa hapa duniani kwa miaka elfu moja kwanza kisha baada ya hiyo miaka elfu kupita, MUNGU mwenyewe atashuka kuja duniani na kuungana na Watakatifu hao na kuishi nao hapa hapa Duniani milele na milele.
UFUNUO 20:7-10
"Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake; naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya Watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka Mbinguni ukawala. Na yule Ibilisi mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti...... "

Kwa maelezo hayo utaona kwamba YESU atakaporudi atakaa na Watakatifu hapa hapa duniani katika kambi ya Watakatifu kwa miaka elfu, wakati huo Shetani atakuwa amefungwa gerezani. Hivyo tunaona wazi kabisa YESU haji kuwachukua Watakatifu na kuwapeleka Mbinguni. Hebu tusome kifungu kinachofutia..

Soma UFUNUO 21:1-8
"kisha nikaona Mbingu mpya na nchi mpya kwa maana Mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita wala hapana bahari tena. Nami nikauona ule mji mtakatifu Jerusalem mpya, ukishuka kutoka Mbinguni kwa MUNGU, umewekwa tayari kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa ikitoka katika kile kiti cha Enzi ikisema, tazama, maskani ya MUNGU ni pamoja na Wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye MUNGU mwenyewe atakuwa pamoja nao........ "

Hapa napo tunaona sasa MUNGU akiwa ndani ya ule mji Mtakatifu yaani Jerusalem mpya uliojengwa Mbinguni anashuka duniani pamoja na mji huo na kuja kufanya makao yake pamoja na Watakatifu waliopo hapa duniani. Hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa Watakatifu hawataenda Mbinguni kwa MUNGU bali watamsubiri MUNGU naye atakuja kuishi nao hapa hapa duniani lakini katika dunia mpya yaani "paradiso". Kwa uhakika zaidi hebu tusome kifungu kingine kutoka kwa Ezekieli.

EZEKIELI 37:12-14
"Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi, tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi Ndimi BWANA, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu...... "

Hakuna neno lililo dhahiri shahiri kama hilo hapo juu. Tumeona wazi kabisa kuwa wafu watafufuliwa na kuwekwa katika nchi yao hapa hapa duniani na wala siyo Mbinguni. Jamani msidanganyike, baada ya ufufuo Watakatifu hawataenda Mbinguni bali wataanza maisha mapya hapa hapa duniani!. Hebu tumalizie kwa kusoma kifungu cha Isaya.

ISAYA 65:17-25
"Maana tazama mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni......... Nao watajenga nyumba na kukaa ndani yake, watapanda mizabibu na kula matunda yake. Hawatejenga na kukaa mtu mwingine ndani yake, hawatapanda akala mtu mwingine, maana kama Siku za mti, ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu na wateule wangu watazifurahia kazi za mikono yao muda wa siku nyingi. Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu, kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao. Na itakuwa ya kwamba kabla hwajaomba nitajibu, na wakiwa katika kunena nitasikia. Mbwa Mwitu na mwanakondoo watalisha pamoja, na Simba atakula majani kama Ng'ombe, ........"

Tumeona wazi kuwa Watakatifu wataishi katika dunia mpya na siyo MBINGUNI kwa MUNGU.
ikiwa mnaamini mtu akifa anaenda Mbinguni kwa MUNGU, Je, kuna haja gani basi ya mtu huyo kufufuliwa tena na kutoka kaburini mwake ikiwa tayari yupo Mbinguni kwa MUNGU???

Wakristo wenzangu, tusidanganywe, tuyasome "maandiko" na tutaijua KWELI nayo hiyo KWELI itatuweka HURU.
 
Ahsante mkuu kwa kujazia naimani itasaidia wengi
 
Ila JPM kama dk chache kabla ya kufa alifanya huduma ya maombi , mwamba sku ya mwisho kuna hatari akasepa mbinguni 😀😀...mana calculation za Mungu za ajabu sana , kukufutia issue zako za nyuma ni swala la robo sekunde tuu...! Nafas za wachache Sana hzo , za kujua it is almost home tyme duuh... Wengine tutakufa ghafla kabla hata hatujawekana Sawa na Mungu wetu ...
Una uhakika kwamba ukitubu siku ya mwisho hua unasamehewa unaenda direct? Yani hujawah kutubu au kutenda mema usubiri kutubu siku za mwisho kutubu baada ya kuona huchomoki eti mungu akusamehe hakuna ujinga wa hivo..Hell to hell
 
Mwangalie mwizi pale msalabani alichomokaje...unasomaga biblia gan ww chief ....wokovu hauangalii matendo yako ya nyuma , just ni Nia dhabit ya toba toka moyoni , with in a second anaclear kila kitu, .....jidanganye na matendo yako sasa .....
 
Ok dhulumu/Ibia watu tesa watu tembea na wake za watu halafu uje utubu siku za mwisho Mkuu, halafu tutakutana wote peponi.
 
eti roho haifi,upagani huo roho hupatikana baada ya mwili kupuliziwa pumzi ya uhai hivyo roho ni muunganiko wa pumzi ya uhai na mwili,pumzi ya uhai inapomtoka mtu inarudi kwa aliye itoa kwa hiyo roho inakuwa imevunjika kwani Ni matokeo ya muunganiko wa pumzi na mwili,kufundisha roho haifi Ni kukubaliana na shetani aliye sema hutakufa hakika.
Wewe ndio wale wale embu fikiria kilicho zaliwa kwa mwili ni mwili na kilicho zaliwa kwa roho ni roho.. Mungu ni hai naye ni Roho ..kwanza nikuambie kwanini Roho ya Mungu huwa herufi kubwa..nikwasababu yeye ni asiri ya roho zote..hii inamaana kuwa chanzo cha uhai wakila kiumbe ni Roho ambaye ni Mungu na roho zote ndizo zitiazo uzima katika kila mwili Wa kiumbe.. Mwili hauna muunganiko Wa lazima na roho hivyo roho haitegemei mwili kuishi ila mwili utegemea roho kuishi..jiulize pumzi ya uhai alipewa MTU na baadae urudi kwa muumbaji wake..inamaana kile kitiacho uzima mwili ndio huondoka...aya tukumbuke wale malaika waliopenda wanawake Wa duniani walijitengenezea miili na kisha kuivaa wakawa watu ila hawakubanwa na mwili kwakua sio Kazi waliyopewa ila roho ya binadamu ilianzia Kazi kwenye mwili na kwaagizo la Mungu roho inabanwa na mwili ila kama mwili utakubali kutoa ushirikiano kwa roho.. Izo Sera za kuwa roho ya binadamu inayeyuka ni uvumi wakijinga na false doctrine.. Ila nikuambie kitu rahisi tu.. Mwogope awezaye kuua mwili na roho na sio auwaye mwili ila hawezi kuiua roho..shetani apendi kukuambia habari za roho maana anajua hana uwezo nayo kuishinda ila anasema kuhusu mwili kwani anajua ni dhaifu kwaiyo angalia fundisho unalopokea maana fundisho la mwili ni lashetani na roho nila mbinguni maana niuhai ila mwili nikifo..unasema eti kuamini roho haifi ni kumuamini shetani kuwa hatufi..shetani aliposema vile alisema pia mtajua mema na mabaya haya walipokula wakawa wanajua mema na mabaya ila ishu ya kufa hapo shetani alisema uongo ila tundra lilikuwa maalumu kuharibu mwili ili roho itoke na mpango Wa Mungu uharibike..shetani alikuwa anataka kuharibu Kazi ya Mungu yaani lengo la Mungu niawe na viumbe vyenye mwili vitawale duniani sasa shetani anaonekana wazi anataka kusiwe na kiumbe mwenye mwili na dunia isitawalike na wenye mwili maana roho haitawali dunia ila roho ikiwa ndani ya mwili kwaiyo hata Yesu aliposema yeye sio waulimwengu alimaanisha kiroho ndio maana hiyo ila kimwili anahusika na dunia... Hivyo Kazi ya shetani ni kuharibu Kazi ya Mungu anajua binadamu kuishi kwa roho halikuwa lengo la Mungu na akishakuwa roho dunia haimuhusu..hivyo Basi shetani alitaka kuuharibu mwili iliutengane na roho yake na sasa anajua Mungu kaja na njia mpya hivyo nayeye anataka watu wafikiri wao ni mwili ili washindwe kwa udhaifu Wa mwili maana roho nikazi...ROHO ILAZI LAKINI MWILI NI DHAIFU.
 
MTU anaishi baada ya kufa?

Mara nyingi kume kuwa na mafundisho mengi ya upotoshaji, nazaidi wengi wao wakifanya kama alivyo Fanya shetani kutumia maandiko matakatifu kumjaribu Yesu mwanawa Mungu. Tumeona na kusikia habari mbali mbali juu ya nini utokea baada ya kifo.

Mara nyingi tumesikia MTU aliyekufa hajui lolote wengine ukifananisha kifo na usingizi.. Sasa tujiulize nini kinatoa uhai yaani kipi kinachofanya mwili uwe na utendaji? Imeandikwa Mungu baada ya kuumba mwili aliupulizia pumzi ya uhai. pumzi ya uhai ninini? Pumzi ya uhai ni roho... roho ndio itiayo uzima na roho ndio uhai kamili.

MTU hufa kwa sababu roho inapofika kikomo cha kuendelea kukaa ndani ya mwili dhaifu.. Roho inauhai na haina udhaifu ila mwili sio hai na nidhaifu.

Mwili unapokuwa umechoka sana na hauwezi kufanya tena Kazi zinazo amriwa na roho... Hapo roho utoka ndani ya mwili na kifo ndio hutokea... Baada ya roho kutoka katika mwili uendelea kuishi kwa nyakati zote kwakua Mungu alipotuumba tu alitupa umilele kwa kutujalia roho isiyo kufa... Pale bustanini kulikuwa na mti Wa uhai na kifo...

Mti Wa kifo ulikuwa maalumu ya kuharibu utdndaji Kazi Wa mwili na hivyo kulelekea mwili kushindwa kuendelea na utendaji na kupelekea kifo.. Ukiwa msomaji mzuri Wa biblia utaungana nami mkono pale Yesu aliposema roho ilazi lakini mwili ni dhaifu.. Alielezea jinsi gani mwili na roho vilivyovitu viwili tofauti

Roho ndio uhai..asiye elewa ajiulize. Nini kinafanya MTU aongee? Na nini ninafanya ashindwe kuongea au nini kinafanya MTU apumue na kipi kinafanya ashindwe? Kwa maana MTU hufa na hewa ikiwa imezunguka eneo lake lakini kwanini anakufa? Ndio maana nasema MTU hufa pale mwili unaposhindwa kutekeleza kile roho inachotaka kifanyike.

Je! Kuna uhai baada ya kifo....? Jibu ni ndio duniani mwili aupo ila roho IPO... Ushawahi kujiuliza kwanini wanaita mwili Wa .... Nasio Fulani? Jiulize mwenye mwili yupo wapi? Ukweli ni kuwa yupo mahali Fulani amekaa anaangalia na anaishi ila hana Kazi tena na mwili wake maana hauwezi tena...

Ndio maana tunaambiwa baada ya kufufuliwa tutapewa miili mipya isiyo na udhaifu ili isijeikashindwa Kazi roho ikaiacha tena..

Tunakufa kwakuwa mwili hauwezi kitu hapa ndio pale msemo Wa wafu awajui lolote unakuja..ishu ya wafu ni mwili ila roho ambaye ni Mimi nitasikia kwa wanadamu na eidha kwa wenzangu Wa roho eti kuwa nimekufa ila kimsingi nipo hai ila bila mwili..Leo tuishie hapa tupate mmeng'enyo wayale tuliyosoma
watoto wa marehemu wasingenyanyaswa na mashangazi na wajomba kama marehemu angekua sehemu anaona
 
Ukifa mambo ya mwili haya kuhusu na hauwi katika mwili..shangazi na wanao ni binadamu na sio roho. Kwani watu awauliwi au awateseki kwani Mungu hayupo? roho zote ufanya sawa sawa na asili yao ya roho
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom