Mkuu swala la wokovu ni tofauti kabisa na fikra za kibinadamu ni tofaut kabisa na kuhudhiria kanisan ama msikitini ni tofaut kabisa na kuwa kiongozi wa dini , ni mahusiano yako na Mungu ndani kabisa ya Moyo wako boss, kinachoangaliwa ni Nia ya dhati ya toba basi, na sio toba ya juu juu , toba ya that ya Moyo na kusikitikia maovu .... Kwa sababu moyo ( hapa nazungumzia mindset sio Moyo nyama inayodunda) ndo unaotamka hvyo huwez kudanganya .....
Mkuu ukianza kusema fulan aliua , sjui fulan alifanya hivi ...yaan hata wewe hapo Mungu angekuwa na Akli kama zetu usingekuwepo ,mana umefanya maovu mengi sema Tu Kwa vile hauna popularity ndo mana wanazengo hatuhajui na hata tukiyajua hayawezi kutupotezea mda .....
Nakupa mfano mmoja wa kwenye biblia ndo ujue sasa calculation za Mungu ni amazing.... Mfalme Manase ni moja ya wafalme waovu kuwahi kutokea , inasemekana jamaa alifikia hatua ya kufanya uzinzi kwenye hekalu , anaanzisha ibada ya mashetani , nabii isaya alipomkemea mfalme manase alimkamata na kumuua , .... Na jamaa akatawala mda mrefu kuliko hata mfalme mwema Daudi , zaidi ya miaka 50 jamaa lipo Ikulu na maovu yake ....
Mwisho ufalme ukashambuliwa na maadui mshikaji akakamatwa i , akateswa Sana...akiwa gerezani akamrudia Mungu , jamaa akaomba aisee , biblia inatamaka wazi kabisa kwamba Mungu akamsikia .... Manase alikufa akiwa na Tumaini la wokovu , jiulize sasa mtu aliyefanya maovu vile but with in a second anarudi kwenye mstari....
Tuachane na huyo Yule mwizi msalabani , dk ya mwisho kabisa jamaa anasepa .....