Mtoto wangu hataki kuniita Baba nifanyaje?

Ushauri wangu muache hivyo hivyo Mkuu, unaweza mfanya akakuita Baba alafu akawachukia binamu zake au akawaona kama sio kundi moja na yeye akawatenga.

Ni swala la muda tu akikuwa ataona majina yake mwishowe atajua ulikua utoto tu usio na madhara sana.
 
Anakuita hivyo kwa sababu "intellect" yake bado iko pure, haijawa polluted na some processes za reasoning; bado iko kwenye pure form kama ambavyo Adam na Hawa walivyokuwa kabla hawajatenda dhambi. Kwa sasa bado anatumia logic peke yake without reasoning. Mind yake itakapokuwa polluted, ndiyo kipindi ambacho sasa ataanza ku-incorporate reasoning kwenye logic.
Kwa sasa akimusikia mtu anakuita uncle, naye anakuita hivyo.

Logically kama mtu A anakuita wewe "uncle", then logically hata mimi pia mtu mzima hapa nilipo lazima nikuite hivyo. Hata hivyo kwa kutumia reasoning, mimi siwezi kukuita uncle. Kwa hiyo kinachopelekea mimi nisikuite wewe uncle, ni reasoning niliyo nayo kichwani kwangu. Bila reasoning, hata mimi pia nitakuita wewe "uncle", iwapo tu nitamsikia mtu mwingine anakuita hivyo!

Kwa hiyo mtoto wako bado hajawa na reasoning ya kujua kuwa kuna wanaokuita hivyo kwa sababu wewe siyo baba yao mzazi. Baadaye tena atakuja sasa kujua hilo na hivyo reasoning itamfanya ajue kuwa kwake yeye wewe unaitwa baba na siyo uncle. Sasa hivi anatumia logic, ambayo kwa mimi naamini is a powerful form of reasoning.
Tuchukulie kwa mfano, wewe hapo ulipo kama ungezaliwa tangu ukiwa mdogo unaona kitu kikirushwa juu kinaendelea kwenda juu hakirudi chini hadi kufikia kupotea moja kwa moja hewani, halafu leo uje uone kitu kinarushwa juu halafu baadaye kinarudi na kuanguka chini,; hali kama hii ingepelekea ushangae sana. Kwa nini? Ni kwa sababu ungekosa logic kutokana na ukweli kuwa siku zote huwa unaona kitu kikirushwa juu kinaendelea kwenda juu hakirudi chini. Kwa hiyo kitendo cha kitu kurushwa juu na hatimaye kurudi chini, mind yako iingeshindwa kuki-accommodate. Kingekuwa ni kitu kigeni kabisa kwako.

I, very much like the way kids think!
Mkuu mimi napenda sana watoto na kuona namna wanavyofikiri na kuwaza na kufanya.

Kuna mambo mengi sana huwa natamani kuyafanya katika research ya kutambua watoto na makuzi yao na namna ya kuzuwia tabia mbali mbali mbovu kwa watoto wadogo.

Nilifikiria kuanzisha uzi utakaozungumzia maswala yote haya na wadau muje kutoa michango yenu kadha wa kadha.

Mathalan kuna siku dada yangu aliniambia "anko wako anakula hatari,bakula la uji analimaliza lote lile kubwa"

Ni mtoto wa mwaka tu alafu ananiambia hivyo.

Nikamuambia unamtesa mtoto,akauliza kwa nini ?

Nikamuambia ushawahi kumvisha nguo yako akavaa ?akasema hapana kaka si hazimtoshi.

Nikamuambia basi unamuumiza kumpa bakuli la uji ambalo unakunywa wewe alafu anamaliza.

Akaniambia "lakini ukimpa kidogo naywe kisha ukibaki ukaaacha kumywesha analia,"

Nikamuambia umeshamzoesha hivyo huyo mtoto anachojua kuwa yeye inabidi maalize tu.
.nikamuambia kama unamtafutia mtoto kiatu cha saizi yake,nguo za saizi yake,kofia saizi yake,wakati mwingine kitanda saizi yake basi kwa nini usiwe na tamaduni ya kumtafutia mtoto kikombe cha saizi yake kuna vikombe viduuchu vya wtoto na sahani zao n.k

Hii itamfanya mtoto asifanye vitu oversize na kumuepusha na balaa la kuwa na litumbo likubwa na obesity baadae.

Mtoto hajui kuwa nguo alizovaa yeye baba yake hazimtoshi anachojua yeye kuwa nguo zote sawa tu,ndio mana anaweza kutaka kuvaa kiatu cha baba yake kwa kuamini hata yeye kinamtosha.

Jambo hili wazazi wengi wanaharibu.

Utakuta mtoto wa mwaka mmoja anawekewa wali kwenye sahani anakula inaskitisha sana mtoto huyu badae anakuja kuwa ma tumbo ambalo mtu mzima amgetakiwa faanye diet
 
Nuoxian
Mtoto aliwahi kuingia chumbani kwangu siku moja halafu akaacha mlango wazi; nikamwambia "John rudisha mlango", halafu yeye akaniangalia machoni akaniuliza swali "wapi?". Reasoning ya hali ya juu sana
Hhhaahahha mkuu mtoto anataka lugha fasaha kabisa ambayo yeye ameiskia.

Ukimuambia hujambo ? Ataitikia sijambo.

Ila ukimuambia mambo vipi ? Atashangaa hajui cha kujibu au atajibu kile anachohisi kinaendana na kitu fulani alichowahi kusikia.

Anaweza akakujibu "mama yupo" ukaona kama hajakusikia vizuri kumbe anafananisha sentensi "mambo vipi" inafanana na neno gani analolijua

Katika maajabu ya mtoto ukiomgea kitu ambacho hukijui ni ngumu kusema hajaelewa 😀😀😀😀
 
Habari ndugu, jamaa, na marafiki kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki.

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle kama wenzake wawili wanavyoniita, saivi ana miaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba? Maana najaribu kumuambia mimi sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.

Umeovariact,ni 3 yr old,atazoea tu
 
Habari ndugu, jamaa, na marafiki kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki.

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle kama wenzake wawili wanavyoniita, saivi ana miaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba? Maana najaribu kumuambia mimi sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.

Usijali mkuu mm nimemuita mama yangu aunt miaka nenda rudi
 
Binti yangu alpozaliwa niliimuita "Mamu",

Kila nikija namuita "Mamu" "Mamu" nae anaitikia "Mamu" "Mamu"

Baadae akiulizwa khs Mimi, uyu Nani?

Anajibu "Mamu"

Basi akazoea ivyo ananiita "Mamu"



Alipofikisha Miaka miwili na nusu, Mama ake akampiga marufuku,

Taratibu akaacha na kuzoea kuniita baba mpaka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom