Mtoto wangu hataki kuniita Baba nifanyaje?

Mtoto wangu hataki kuniita Baba nifanyaje?

mimi nina miaka 26 sijawai muita mamangu "Mama" namwitaga aunt mpaka leo japo natambua ni mama nililelewa ujombani nikakuta watoto wa mjomba wanamuita hivyo nami nikaunga na pia mjomba na mke wake ndo nawaitaga baba na mama,hata nilipomjua babangu ilikua ngumu kuzoea kumuita baba mama wa kambo ndo kumuita mama ilishindikana lakini mungu anisamehe tu
 
Habari ndugu, jamaa, na marafiki Kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki,

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle Kama wenzake wawili wanavyoniita, saiv anamiaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba.? Maana najalibu kumuambia mm sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.
Inawezekana ukawa anko kweli[emoji14][emoji14][emoji14][emoji14][emoji14]


Mwambie mkeo amfundishe hamna njia nyingine banana na mama yake
 
Hio kawaida nilikuwa namwiita Maza kwa jina lake halisi nilizoea wadogo zake jinsi wanavyomuita
 
Kawaida mkuu

Mwanangu anamuita mama yangu mama badala ya Bibi na amezoea hadi watu wameshazoea .

As anavyokuwa anaona tunamuita mama, nae ndio amezoea na ni binti mkubwa sasa.
 
UNA HAKIKA NI WAKO BWASHEEE......ila kuwa mpole atajitambua mda si mrefu.....ila hata hao wa dada zako...tell them kukuita BABA......sio mbaya......BABA - the one who take responsibility ya familia nzima.....(wa nyumbani kwako)....
 
Habari ndugu, jamaa, na marafiki kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki.

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle kama wenzake wawili wanavyoniita, saivi ana miaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba? Maana najaribu kumuambia mimi sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.

Katika kitabu ambacho nimeplan kukiandaa kuhusu malezi ya watoto hili nalo nitaligusia.

Ni kwamba mtoto anakuita jina fulani kwa sababu ya vile anavyo experience ulimwengu unavyokutambua wewe.

Kama mtoto anasikia kila siku watu wakikuita mama basi na yeye atakuita mama hata kama ni mwanaume.

Sasa cha kufanya aanza na mambi madogo madogo yafuatayo.

Kama umerudi nyumbani mwambie mkeo amwambie mwanao "haya nenda kwa baba amerudi baaaba yuleeee"

Hapo mtoto taratibu ataanza kujua kwamba kumbe natambulishwa kwamba huyu ni baba angu"

Lakini pia wewe mwenyewe jitahidi kumuita mtoto wako " baba " nayeye itamfanya akuite baba hivyo hivyo,kwa sasa hatoelewa ila baadae atajua kwa nini anakuita baba wakati huo tayari neno baba ashalizoea.

Nduo maana zamani mimi mwanaume ila shangazi yangu ananiita shangazi,bibi yangu ananiita bibi,mjomba ananiita mjombaa,baba ananiita baba.

Hii ikafanya kila mtu nimuite vile anavyoniita mama,baadae tena unakuja kujua kwa nini uliwaita hivyo.
 
Habari ndugu, jamaa, na marafiki kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki.

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle kama wenzake wawili wanavyoniita, saivi ana miaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba? Maana najaribu kumuambia mimi sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.




dah samahan kama nitakuwa ninekukwaza ila nahs hujui akili ya mtoto mdogo inavyofanya kazi

mtoto mdogo akili yake iko curious wakat wote na njia peke ya kujifunza kwa mtoto ni copy and paste ya maneno na matendo.. then anavyoendelea kukua ndo anajua maana ya hayo matendo. hata hilo neno uncle au baba hajui maana yake. so kuanza kupata stress inashangaza


kwa ufupi anatumia mda mwingi na wenzie so kuna mambo amecopy kwa wenzie pengine ww unakaa nae masaa unataka umkaririshe vitu ambavyo hakuna mwingine anafanya. ye anajua uncle ni jina lako kama wengine wenye majina

ungekuwa ww ni mzaz wa hao watoto wa ndugu yako na yy ndo mtoto wa dada yako basi angekuwa anakuita baba kama
wanao na sio uncle

Mob psychology is at play dont stress akikua akajua utofaut ataanza kukuita baba. kuna waliolelewa na bibi zao waliwaita Mama badala ya bibi
 
Kapime DNA inawezekana we ni uncle kweli na mtoto ni wa Ole Sabaya
 
Habari ndugu, jamaa, na marafiki kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki.

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle kama wenzake wawili wanavyoniita, saivi ana miaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba? Maana najaribu kumuambia mimi sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.

Anakuita hivyo kwa sababu "intellect" yake bado iko pure, haijawa polluted na some processes za reasoning; bado iko kwenye pure form kama ambavyo Adam na Hawa walivyokuwa kabla hawajatenda dhambi. Kwa sasa bado anatumia logic peke yake without reasoning. Mind yake itakapokuwa polluted, ndiyo kipindi ambacho sasa ataanza ku-incorporate reasoning kwenye logic.
Kwa sasa akimusikia mtu anakuita uncle, naye anakuita hivyo.

Logically kama mtu A anakuita wewe "uncle", then logically hata mimi pia mtu mzima hapa nilipo lazima nikuite hivyo. Hata hivyo kwa kutumia reasoning, mimi siwezi kukuita uncle. Kwa hiyo kinachopelekea mimi nisikuite wewe uncle, ni reasoning niliyo nayo kichwani kwangu. Bila reasoning, hata mimi pia nitakuita wewe "uncle", iwapo tu nitamsikia mtu mwingine anakuita hivyo!

Kwa hiyo mtoto wako bado hajawa na reasoning ya kujua kuwa kuna wanaokuita hivyo kwa sababu wewe siyo baba yao mzazi. Baadaye tena atakuja sasa kujua hilo na hivyo reasoning itamfanya ajue kuwa kwake yeye wewe unaitwa baba na siyo uncle. Sasa hivi anatumia logic, ambayo kwa mimi naamini is a powerful form of reasoning.
Tuchukulie kwa mfano, wewe hapo ulipo kama ungezaliwa tangu ukiwa mdogo unaona kitu kikirushwa juu kinaendelea kwenda juu hakirudi chini hadi kufikia kupotea moja kwa moja hewani, halafu leo uje uone kitu kinarushwa juu halafu baadaye kinarudi na kuanguka chini,; hali kama hii ingepelekea ushangae sana. Kwa nini? Ni kwa sababu ungekosa logic kutokana na ukweli kuwa siku zote huwa unaona kitu kikirushwa juu kinaendelea kwenda juu hakirudi chini. Kwa hiyo kitendo cha kitu kurushwa juu na hatimaye kurudi chini, mind yako iingeshindwa kuki-accommodate. Kingekuwa ni kitu kigeni kabisa kwako.

I, very much like the way kids think!
 
Nuoxian
Mtoto aliwahi kuingia chumbani kwangu siku moja halafu akaacha mlango wazi; nikamwambia "John rudisha mlango", halafu yeye akaniangalia machoni akaniuliza swali "wapi?". Reasoning ya hali ya juu sana
 
Back
Top Bottom