Mtoto wangu anatapika kila anachokula

Mtoto wangu anatapika kila anachokula

Ntikwite

Member
Joined
May 13, 2017
Posts
94
Reaction score
54
Habari za mda huu wana janvi wenzangu,

Mimi nina mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitato, leo ni siku ya nne kila anacho kula anatapika hata akinywa maji tu anatapika hata maziwa ya mama anatapika, tumempeleka hospitali zaidi ya tatu wamempima Maralia na vipimo vingine wanasema hana shida wametupatia dawa ya kuzuia kutapika inaitwa pedzinc ila nayo tukimpatia anatapika hata haukai dakika.

Naombeni ushauri wenu
 
Mrudishe hospital uwaeleze madaktari haya kuepusha mtoto kukosa maji mwilini. Hii ifanye kama emergency case.
 
Mtoto wangu alikua ana nimonia, anaendesha na kutapika. Pedzinc aligewa ili kuzuia kuendesha, kutapika aligewa dawa jina limenitoka. Hizi hazikusaidia, niliambiwa pedzinc ndiyo dawa ya juu ya kuzuia kuendesha baada ya ile hua hakuna nyingine. So ingawa dawa haikuonyesha kusaidia sikutakiwa kuacha kumpa.

Tulianzia Mnazi Mmoja kisha tukaja Temeke, akalazwa zaidi ya wiki mbili. Chukulia serious hii ishu mkuu. Mtoto alikua hagomi kula, hata zile oral alikua anakunywa hakatai ila shida ni akila atatapika.

Mwanzo bibi yake alifikiri mtoto kanyonya maziwa ya mama wakati mama katoka kushiriki tendo, na ninafikiri ukiwauliza baadhi ya watu wanaweza wakakuambia hivi pia. Rudini hospitali mkuu.
 
Mpeleke hospitali kubwa kama Muhimbili sio tuvituo tudogo dogo hutu Mpeleke kwa madakitari bingwa
 
Mpeleke kwa mtaalam wa watoto dr.nani sijui nimemsahau jina nasikia ni bingwa wa magonjwa ya watoto Yupo Kariakoo.
 
Mkuu ni dalili ya kuonyesha mtoto wako Meno yana anza kuota hayo jaribu kumpa maji ya uvugu ya chumvi na sukari au mpe glucose kila mara atapona maradhi yake. Tumia ushauri wangu kisha leta hapa majibu yako aka mrejesho wako.
 
mzizi mwaka na miezi mi5 dalili za meno?
Mkuu ni dalili ya kuonyesha mtoto wako Meno yana anza kuota hayo jaribu kumpa maji ya uvugu ya chumvi na sukari au mpe glucose kila mara atapona maradhi yake. Tumia ushauri wangu kisha leta hapa majibu yako aka mrejesho wako.
 
Nenda hospital wamchome Sindano ya kuzuia kutapika mkuuu maana Oral drug zote anatapika.. Kuna dawa za kuchomwa ataacha kutapika tu!

Pedzinc haizuii mtoto kutapika ila inazuia mtoto kuharishaaa.. Kama ana harisha pia ndo umpe Pedzinc..ORS na uji wake mumpe wa CHUMVI sio muweke Sukari.
 
Mkuu ni dalili ya kuonyesha mtoto wako Meno yana anza kuota hayo jaribu kumpa maji ya uvugu ya chumvi na sukari au mpe glucose kila mara atapona maradhi yake. Tumia ushauri wangu kisha leta hapa majibu yako aka mrejesho wako.
Meno kuota hakusababishi mtoto Kutapika labda kuharishaa na haiwii severe kiasi hicho!! Meno labda apate homa kidogo na kuharisha na si kutapikaaa
 
Back
Top Bottom