Mtoto wangu amenyolewa nywele usingizini naomba ushauri

Mtoto wangu amenyolewa nywele usingizini naomba ushauri

karango

Senior Member
Joined
May 19, 2013
Posts
162
Reaction score
25
Jamani wadau naomba naomba ushauri/msaada. Nimeamka asubuhi wiki iliyopita nikakuta mtoto wangu amenyolewa nyele mpaka leo upara unaendelea kuongezeka sijui nifanyeje.

Naomba mawazo kwa wale ambao yashawakuta
 
Nimeamka asubuki nikakuta mtoto wangu amenyolewa nyele utosini ila mpaka sasa zinazidi kukatika zaidi ya asilimia hamsini naomba ushauri kwa wale ambao yashawakuta jamani sijui cha kufanya
 
Uwe Mkristo au siyo, anza kumwomba Yesu hapo ulipo. Usikemee mapepo kama wewe sio mkristo wa kweli kwani ni hatari.

Ila elekeza sala zako kwa Yesu ukimwomba akusaidie na halafu tafuta mkristo wa kweli, yaweza kuwa vigumu lakini ongea na watu unaofikiri wanaweza kukupeleka kwa wale wafanyao maombi ya kweli na utasaidiwa.

Mambo ya kichawi yapo sana na dawa yake ni moja tu, Yesu Kristo!
 
Pole, wafunga mafundo wapo kazini. Unaishi mitaa ipi mkuu.
 
Hahahaaa wana JF mmepinda nyie...i think ni aina ya fungus nenda hospital,mie nilishawahi kupoteza nywele sema ilikuwa kidogo sio sana,ugonjwa unaitwa alopecia i think,mie sio mtaalam watakuja madaktari kukusaidia
 
asante dokta " i think ".
 
Hao ni wachawi ila hawatamdhuru kwa lolote wanaleta hofu tu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Inawezekana kuna mganga anataka kupata pesa yako hivyo anakufanyia vituko wewe waeleze wote wanaokuja kukupa pole na ushauri kuwa wewe unamwachia mungu na mtoto wako atakuwa salama salimini
 
Hao ni wachawi ila hawatamdhuru kwa lolote wanaleta hofu tu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Sasa nitafanyaje ziote. Niliamua kumnyoa upara lakini nashangaa zilivyoota zimeota kama 20% asilimia nyingine hazioti. Nikiziangalia napata hasira mno
 
Mtoto wako ana akili sana, hata kama huoni hilo sasa, na utaona ataendelea kushuka kielimu Darasani, Unaweza kujua taarifa za mtu kwa kutumia nywele, lkn unaweza kutumia nywele za mtu kufanya mtu huyo afanye unachotaka,Kwa kutumia nywele za mtu unaweza kujua huyo mtu anawaza nini.

TAFADHALI-Nakuomba Tafuta Mtumishi wa Mungu, awe Mtumishi kweli sio msaanii, amwombee mtoto, kama utahitaji ushauri zaidi uwe huru.
 
cha kufanya rafiki njoo kwenye ibada eagt city centre kwa mchungaji katunzi viwanja vya sabasaba kuanzia saa kumi kila jumatano hadi jumamosi jumapili ni ibada saa tatu asubuhi nakwambia nywele zitaota huo ni uchawi nimeona mtu akifunguliwa wrngi tu wachawi hupenda watoto sana ukichelewa utajuta nakushauri huyu mchungaji anaombea buree na usikosee ukaenda kwa mitume au manabii utajuta mtafute mchungaji katunzi hakika huyo mtoto atapona sabasaba maonyesho karibu na uwanja wa taifa panda magari ya kwa azizally.ni datressalaam
 
komesha yao tafuta mifupa ya nguruwe uweke humo chumbani na kwenye madirisha..hawatarudi hao
 
cha kufanya rafiki njoo kwenye ibada eagt city centre kwa mchungaji katunzi viwanja vya sabasaba kuanzia saa kumi kila jumatano hadi jumamosi jumapili ni ibada saa tatu asubuhi nakwambia nywele zitaota huo ni uchawi nimeona mtu akifunguliwa wrngi tu wachawi hupenda watoto sana ukichelewa utajuta nakushauri huyu mchungaji anaombea buree na usikosee ukaenda kwa mitume au manabii utajuta mtafute mchungaji katunzi hakika huyo mtoto atapona sabasaba maonyesho karibu na uwanja wa taifa panda magari ya kwa azizally.ni datressalaam

Magari ya kwa "azizally" ndio mini???. Na hiyo datressalaam,
Ni kitu gani????, please.
 
Back
Top Bottom