Mtoto wa Mengi kubambikiwa Madawa - VIGOGO POLISI KORTINI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Mengi kubambikiwa Madawa - VIGOGO POLISI KORTINI

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by JoJiPoJi, Nov 23, 2010.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  Kuna habari kwamba baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi na mfanyabiashara mmoja waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Abraham Mengi watafikishwa mahakamani kwa madai ya kutaka kumbambikizia mwanae dawa za kulevya.

  Habari zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya jeshi la polisi vimedai kuwa, vigogo hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili haki iweze kupatikana.

  Taarifa hizo zimedai kuwa uhamisho wa vituo vya kazi uliofanywa ndani ya jeshi hilo ambapo Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kanda Maalum, jijini Dar es Salaam, Charles Mkumbo wamehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo, ni mpango mahususi wa kutoa fursa kuwafikisha kortini ili tuhuma zao zikaamuliwe na chombo hicho.
  “Uhamisho uliofanywa ndani ya jeshi siyo wa kawaida kwani hata maofisa wengine waliohamishwa wamefanyiwa hivyo ili kufunika hili la watuhumiwa wa mzee Mengi.

  “Unajua swala hili hata sisi polisi linatuchanganya na sioni sababu ya kutolitolea tamko kwani hata tume iliyoundwa haikusema itachukua muda gani na mpaka sasa wananchi hawajui kinachoendelea, lakini watafikishwa kortini ili ukweli ukajulikane huko,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina gazetini

  Kwa upande mwingine askari mmoja wa ngazi za juu aliliambia gazeti hili kuwa tuhuma zilizotolewa na Mzee Mengi ni nzito na kitendo cha polisi kuwabadilisha kazi watuhumiwa kimeleta tafsiri mbaya kwa wananchi ambao wengi wanadhani kuwa uhamisho huo umekusudia kufunika kombe ili mwanaharamu apite, (yaani kuzima hoja).

  Aidha, afisa huyo alisema ingefaa serikali ingetoa kwanza taarifa ya tume iliyoiunda kuhusiana na sakata hilo ndipo wahamishwe kuliko kuwahamisha wakati ukweli haujajulikana.

  Aliongeza kwamba, suala la madai ya mzee Mengi lilikuwa rahisi kwa sababu mdai alisharuhusu jambo hilo lifikishwe mahakamani lakini serikali inajikanyaga, kitu ambacho kinaleta minong’ono isiyo na sababu katika jamii na kusababisha kitendawili kisiweze kutenguliwa.

  Hata hivyo, afisa huyo alimsifu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema kwa kazi nzuri ya kuliletea heshima jeshi hilo hasa kipindi cha uchaguzi ambapo alisema kuwa demokrasia ilitumika kwa kiwango cha hali ya juu na hivyo kwa hali hiyo asikubali kukalia tuhuma ambazo baadaye zinaweza kuja kumchafua.

  “IGP Mwema tunajua kwamba kokoro linaweza kubeba kila kitu sasa ni kazi yako kuchambua samaki na kisichokuwa kitoweo,” alisema afisa huyo.

  Mwandishi wetu alifanya mahojiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SSP Advera Senso kuhusiana na suala la maofisa waliotuhumiwa na mzee Mengi kama watafikishwa mahakamani ambapo alisema sakata hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini, (Takukuru).

  “Mimi nakushauri uende Takukuru, jeshi la polisi lilikabidhi kesi hiyo huko,” alisema Kamanda Senso.
  Afisa Uhusiano Mkuu wa Takukuru, Doreen Kapwani alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alikiri kuwa wanalishughulikia.

  “Tunashughulikia malalamiko yale lakini taarifa za kupelekwa mahakamani watuhumiwa bado hazijanifikia,” alisema Kapwani.

  Gazeti hili lilimtafuta mmoja wa watuhumiwa, Bw. Nzowa alipohojiwa alisema hana la kusema bali suala hilo amelikabidhi kwa Mungu. Mkumbo hakupatikana.
  Wakati huo huo, taarifa sahihi tulizozipata wakati gazeti hili likienda mitamboni zinasema polisi 12 wametiwa mbaroni jana kuhusiana na wizi wa mabomba 160 uliotokea Temeke.

  Chanzo chetu cha habari kilisema mabomba hayo yaliibwa Novemba 16, mwaka huu katika ghala la vifaa vya ujenzi la Kampuni ya United Bulders Limited lililopo Barabara ya Nyerere .

  “Polisi hao 12 walikamatwa kwa tuhuma za kuwakamata majambazi waliohusika na wizi huo wakiwa na gari lililotumika kubeba mabomba hayo kisha kuwaachia,” alisema mtoa habari wetu.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alipoulizwa kwa njia ya simu juu ya tukio hilo jana Jumatatu alisema ni kweli limetokea na akaongeza kuwa raia saba na askari wanaotuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.


  Source; GP
   
 2. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mwema awe mwangalifu hili jeshi lisirudi enzi zile za kina Zombe kwani kipindi kile ilikuwa ni jehanamu
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mengi ni mfanya biashara msomi na jasiri. Ameweza kupambana na vigogo kadhaa nchini akiwemo Masilingi, Masha na kuibuka kidedea, sidhani kama Manji atasimama mbele ya Reginald. He knows the rules of the game.
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena, mzee Mengi ana technique nyingi sana halafu informers ni kibao tena wengine kwa kujitolea kabisa bila kupewa hata chochote kwa kuwa wana imani naye. Deal yoyote chafu kwa mzee utaponzwa nayo tu. Uliza kina Masha na Masilingi kwa ujeuri wao, kwisha kazi!! Masha kule Mwanza nyumba yake inalindwa na polisi maana muda wote itatiwa kiberiti na kule hatakiwi kufika!!! Ha ha ha jamaa kafukuzwa kwao na nguvu ya umma. Mioto mingine inachoma sana tuwe nayo makini. Sasa hao mafisadi wapumue tu hiki kipindi cha mptito halafu 2015 atafute makazi kabisa nje ya nchi maana ni hatari kuishi hapa. We want tu regain our lost wealth to only 1% of the capitalists while 99% are citizens in abject poverty. And the 99% of the 1% are the mafisadi papas!!

   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kinachomlinda Mengi ni uzawa alionao kwa nchi yake.
   
 6. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ndio maana manji yuko busy na yanga sasa hivi alikuwa anajidai hataki tena, anatafuta public sympathy
   
 7. t

  togo Member

  #7
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mengi naye anatuzingua nindumila kuwili anasapoti ccm huku anapiga vita ufisadi while ccm=ufisadi
   
 8. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Presumption of innocence. Let's wait and see what kind of evidence they would put forth. "If it doesn't fit, you have to acquit"
   
 9. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kuna mdau alishawahi kusema tungekuwa na Mengi kama kumi kila mkoa nchi ingebadilika, umaskini ungepungua kiasi kikubwa sana.
   
 10. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Dogo huhitaji kuchukia ccm wala chadema wala tlp au CUF ;;;;Chukia wale wanaofisadi mali za nchi hii.
  IMANI YA MTU NI TOFAUTI NA DINI YAKE.
   
 11. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  ngoja wapambane, polisi wamezidi kubambikia watu wakosa
   
 12. U

  Uswe JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  am starting to love this dude, i wish kila mtu angekua jasiri kama Mengi. ye angedeal na mifisadi papa (rostam, manji and the like) sie tungehangaika na vidagaa (polisi) lakini sasa ye anahangaika nao wote!
   
 13. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Acha Mengi awe CCM. Mbwa hawa huwezi kuwatupia mawe ukiwa unatembea kwa miguu, watakuuma!
   
 14. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa nini tusiwe mamengi sisi wenyewe.
   
 15. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,224
  Likes Received: 2,089
  Trophy Points: 280

  Issue ya Mengi na Masilingi ilikuwa kubwa kuliko uwezo wa Masilingi kuizima, ilibidi wazee wa busara kumtaka Masilingi a-shut up for good. Ilikuwa inahusu rushwa katika uuzaji wa hoteli ya Kilimanjaro pale Sokoine Drive. Masilingi na wenzake walikuwa wanataka 'CHA JUU' katika uuzaji huo, akiwa anashughulika na uuzaji wa mashirika ya umma, enzi za PSRC.
   
 16. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mzee Mengi hata kama kuna tusiyoyajua nyuma ya pazia naamini yatakuwa ya kawaida sana kama binadamu au mfanya biashara wa kawaida. Ana tofauti kubwa na wafanyabiashara wengi esp wa asili ya asia (manji, somaiya, rostam sijui wa iran???) amabao hata uraia wao ni tata.

  Mengi ni jasiri na anajua fitina za nchi hii kama tulivyoona mitanange yake na Malima, Masha, Rostam, Manji, Masilingi, now Polisi etc ambapo yote kaibuka kidedea. Tukumbuke kuwa nguvu yake pia inatokana na support anayowapa wagombea wa urais CCM ndio maana hata Guninita wa CCM-Dar alipozusha kwamba RM sio mwanaCCM makao makuu walimshukia kwa spidi ya mwanga. Big up to your self RM.
   
 17. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Siasa si Uadui....SABODO J SABODO... mnazi wa falsafa za Mwalimu Nyerere... ni kada wa CCM na anasaidia upinzani!!
   
 18. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  mzee mengi ni kielelezo cha watu makini na wapenda maendeleo. Anajari sana utu. Kwa kweli anafaa sana kupongezwa na kuigwa kwa mambo mazuri anayoifanyia jamii yetu.jamani chanda chema huvikwa...... Jamani tusiwe wachoyo wa shukurani wala tusiwe wanafiki huyu mzee anafaa sana kuigwa kwa mema yake. Sawa anaweza kuwa na mapungufu yake km binadamu wote tulivyo lakini mi naona hata km kuna mapungufu basi ni madogo ukilinganisha na mema anayofanya ktk jamii yetu. Big up mzee mengi.mungu azidi kukupa afya njema na amani.
   
 19. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  .... kilichotokea hapo ni kwamba kijana alikuwa abambwe na biashara ambayo huenda amekuwa anafanya. Alichomoa mapema na WAKAWEZA kubadilisha kibao! habari ndo hiyo!!!!

  Nzowa was right alipokejeli kwamba dau la USD 40K ni dogo sana ukilinganisha na mengine makubwa aliyokumbana nayo na AKAYAKATAA!!!
  There is a lot more to this. Usanii tu!
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Dec 6, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba mafisadi wanalindwa kwa gharama yoyote na ccm!
   
Loading...