Mtoto wa Mengi kubambikiwa Madawa - VIGOGO POLISI KORTINI

.... kilichotokea hapo ni kwamba kijana alikuwa abambwe na biashara ambayo huenda amekuwa anafanya. Alichomoa mapema na WAKAWEZA kubadilisha kibao! habari ndo hiyo!!!!

Nzowa was right alipokejeli kwamba dau la USD 40K ni dogo sana ukilinganisha na mengine makubwa aliyokumbana nayo na AKAYAKATAA!!!
There is a lot more to this. Usanii tu!

Of course maelezo ya Nzowa yalikuwa yanajichanganya sana, na yalikuwa yana kitu yanaficha ambacho yeye binafsi anakifahamu kwa undani sana.
 
Mzee wetu Mengi alifanya BIASHARA gani zikamfikisha hapo alipo?

Kwa mujibu wa historia yake (Niliiona miaka kadhaa iliyopita ktk Channel 10 documentary), alianza kwa ku-assemble kalamu aina ya EPICA miaka hiyo. Then akakopa pesa km milioni 500 (enzi hizo ilikuwa ni pesa ndefu sana) kutoka benki ya NBC kabla haijavunjwa kuwa NMB na NBC, ndipo akapanua biashara zake. Lakini kuna stori nyingi sana kumhusu yeye, hebu pitia threads za zamani hapa JF ujue undani wake.
 
huyo mtu aliyetaka kumbambikizia ni geneus hata hiyo kesi atashinda tu amini usiamini hawawezi mfanya chochote angalia MENGI mwenyewe alishindwa kumtaja wazi hazarani zaidi ya kuwataja waliopewa rushwa na kusema kama kuna mtu kaonewa aende mahakamani,amejipanga kama walivyojipanga,........kama angetaka waende mahakamani angentaja huyo aliyeandaa huo mpango upo hapo.............polisi ndio waliopewa rushwa ndio wanashitaki unaona hapo kuna mtu atajiunguza kweli?ya kwangu hayo..............
 
Kwa kweli kila mtu mpenda maendeleo ya nchi hii anatakiwa kumpa heko Mzee Reginald Mengi. Ni mtu aliyejitolea kufa kwaajili ya nchi hii. Kupambana na watu kama kina Manji, Jitu Patel na Rostam si jambo dogo. Nani mwenye uwezo wa kupambana na mafisadi hao kama si Reginald Mengi, the true son of Africa? Fine, Mengi kama Mengi anaweza kuwa na mapungufu yake kama binadamu wengine lakini he is a good example of patriotic citizens in this country. Big Up RM.Ulishawahi kusikia Patel, Rostam au Manji amechangia Saccos au kula na walemavu popote katika nchi hii?Its only Reginald Mengi. May God Bless him a thousand times.
 
Kuna habari kwamba baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi na mfanyabiashara mmoja waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Abraham Mengi watafikishwa mahakamani kwa madai ya kutaka kumbambikizia mwanae dawa za kulevya.
Source; GP


Hamna shtaka hadi hapo. Cross check upya na source zako wakueleze mashtaka halisi!
 
Mtoto anafanya biashara, akataka kupitisha mzigo .alipojua dili limestukiwa akaenda kushtaki kwa baba kana kwamba kabambikiwa. baba kaingia kichwa kichwa kumtetea mtoto bila kujua au kujifanyisha mtakatifu.one day yes the big camera will capture you baby, come on.
 
Kuna habari kwamba baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi na mfanyabiashara mmoja waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Abraham Mengi watafikishwa mahakamani kwa madai ya kutaka kumbambikizia mwanae dawa za kulevya.

Habari zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya jeshi la polisi vimedai kuwa, vigogo hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili haki iweze kupatikana.

Taarifa hizo zimedai kuwa uhamisho wa vituo vya kazi uliofanywa ndani ya jeshi hilo ambapo Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kanda Maalum, jijini Dar es Salaam, Charles Mkumbo wamehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo, ni mpango mahususi wa kutoa fursa kuwafikisha kortini ili tuhuma zao zikaamuliwe na chombo hicho.
“Uhamisho uliofanywa ndani ya jeshi siyo wa kawaida kwani hata maofisa wengine waliohamishwa wamefanyiwa hivyo ili kufunika hili la watuhumiwa wa mzee Mengi.

“Unajua swala hili hata sisi polisi linatuchanganya na sioni sababu ya kutolitolea tamko kwani hata tume iliyoundwa haikusema itachukua muda gani na mpaka sasa wananchi hawajui kinachoendelea, lakini watafikishwa kortini ili ukweli ukajulikane huko,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina gazetini

Kwa upande mwingine askari mmoja wa ngazi za juu aliliambia gazeti hili kuwa tuhuma zilizotolewa na Mzee Mengi ni nzito na kitendo cha polisi kuwabadilisha kazi watuhumiwa kimeleta tafsiri mbaya kwa wananchi ambao wengi wanadhani kuwa uhamisho huo umekusudia kufunika kombe ili mwanaharamu apite, (yaani kuzima hoja).

Aidha, afisa huyo alisema ingefaa serikali ingetoa kwanza taarifa ya tume iliyoiunda kuhusiana na sakata hilo ndipo wahamishwe kuliko kuwahamisha wakati ukweli haujajulikana.

Aliongeza kwamba, suala la madai ya mzee Mengi lilikuwa rahisi kwa sababu mdai alisharuhusu jambo hilo lifikishwe mahakamani lakini serikali inajikanyaga, kitu ambacho kinaleta minong’ono isiyo na sababu katika jamii na kusababisha kitendawili kisiweze kutenguliwa.

Hata hivyo, afisa huyo alimsifu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema kwa kazi nzuri ya kuliletea heshima jeshi hilo hasa kipindi cha uchaguzi ambapo alisema kuwa demokrasia ilitumika kwa kiwango cha hali ya juu na hivyo kwa hali hiyo asikubali kukalia tuhuma ambazo baadaye zinaweza kuja kumchafua.

“IGP Mwema tunajua kwamba kokoro linaweza kubeba kila kitu sasa ni kazi yako kuchambua samaki na kisichokuwa kitoweo,” alisema afisa huyo.

Mwandishi wetu alifanya mahojiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SSP Advera Senso kuhusiana na suala la maofisa waliotuhumiwa na mzee Mengi kama watafikishwa mahakamani ambapo alisema sakata hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini, (Takukuru).

“Mimi nakushauri uende Takukuru, jeshi la polisi lilikabidhi kesi hiyo huko,” alisema Kamanda Senso.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Takukuru, Doreen Kapwani alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alikiri kuwa wanalishughulikia.

“Tunashughulikia malalamiko yale lakini taarifa za kupelekwa mahakamani watuhumiwa bado hazijanifikia,” alisema Kapwani.

Gazeti hili lilimtafuta mmoja wa watuhumiwa, Bw. Nzowa alipohojiwa alisema hana la kusema bali suala hilo amelikabidhi kwa Mungu. Mkumbo hakupatikana.
Wakati huo huo, taarifa sahihi tulizozipata wakati gazeti hili likienda mitamboni zinasema polisi 12 wametiwa mbaroni jana kuhusiana na wizi wa mabomba 160 uliotokea Temeke.

Chanzo chetu cha habari kilisema mabomba hayo yaliibwa Novemba 16, mwaka huu katika ghala la vifaa vya ujenzi la Kampuni ya United Bulders Limited lililopo Barabara ya Nyerere .

“Polisi hao 12 walikamatwa kwa tuhuma za kuwakamata majambazi waliohusika na wizi huo wakiwa na gari lililotumika kubeba mabomba hayo kisha kuwaachia,” alisema mtoa habari wetu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alipoulizwa kwa njia ya simu juu ya tukio hilo jana Jumatatu alisema ni kweli limetokea na akaongeza kuwa raia saba na askari wanaotuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.


Source; GP





Umbea mtupu!
 
Big up Chorne, ukweli ndio huo. mtoto wa mengi inasemekana ni mfanyabiashara mzoefu(baba yake anweza kujua au asijue) na siku hiyo alikuwa anataka kupitisha mzigo jammaa wakamshtukia wakaanza kumnyatia, akakaikimbilia kwa baba naye kama kawaida kaenda kutafuta public sympathy na kupoliticize issue. inasemekana kinachozuia dogo na dingi wake kuchukuliwa hatua stahili ni uhusiano wa karibu kati ya baba na JK. Baada ya tukio hilo JK alienda kwa mengi nyumbani, haijulikani waliongea kitu gani lakini kwa sababu swala lilikuwa hewani uwezekano mkubwa waliongea pia hilo. kusema kweli hao mapolisi hata kama watashtakiwa itakuwa ni dhambi kubwa kwa maana walikuwa wanafanya kazi yao. Ukumbuke kuwa wanaoifahamu biashara hii siku nyingi wanatafuta jinsi ya kumuondoa Nzowa kwenye kitengo hicho.
 
Watafikishwa mahakamani siku yoyote kuanzia sasa........ Siku yoyote bado haijafika tuendelee kukaka kwenye viwanja vya mahakama hadi siku yoyote ifike.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom