Andindile
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 304
- 16
Ni kweli yametokea, kijana alikuwa anasoma Bsc. Engineering geology . Wazazi wake ni maskini wa kutupwa. Ni wa kulima wa kujikimu mkoani mbeya. Mtoto wao baada ya kufaulu vizuri alichaguliwa kujiunga chuo kikuu Dar mwaka 2007/2008 hivyo mwaka huu alikuwa anamalizia mwaka wake wa pili. Bodi ya mikopo ilimpatia asilimia 40% tu ya mkopo hivyo kutakiwa kumalizia iliyobakia. Kwa vile hakuwa na uwezo alilikata rufaa lakini ilitupiliwa mbali. Ulipotokea mgomo wale wasio na uwezo waliambiwa kuwa wakate rufaa kwa waziri. Zile rufaa ziliishia kushugulikiwa na bodi ya mikopo hivyo kijana kujikuta rufaa yake ikigonga mwamba kwa mara ya pili. Alijaribu kumwona waziri mwenye dhamana lakini wapi. hivyo akawa hana jinsi zaidi ya kuomba kuahirisha masomo na kuingia mtaani kushika chaki labda atadunduliza hiyo ailimia 60% ya miaka minne. Hivi ninavyo andika ujumbe huu kijana yupo mtaani akishika chaki.
Ukitaka kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya HESLB utaona ni kwa jinsi gani wale wote ambao wazazi wao ni maskini rufaa zao zilivyotupwa kasoro tu wale ambao ni yatima na wenye ulemavu. Kwa bodi ya mikopo kama wewe wazazi wako ni maskini hicho si kigezo cha kupewa 100%.
-Je ni wanafunzi wangapi watakosa/wamekosa elimu ya juu kwa sababu ya umaskini wao?
-Je tunataka vijana wafoji vyeti vya vifo vya wazazi wao ndipo tuwahurumie na kuwasomesha? Kwa nini tufike huko?
-Ndugu wana JF tunajenga taifa la watu gani kama mtu tutamsubject kwenye shida zote hizi ili tu apate elimu katika nchi yake?
Nawasilisha