Hapa napata shida sana,kumtofautisha Lowasa na mtoto wake!Kwani kama ufisadi ulifanyika ulimnufaisha nani?Si familia yake?Mtoto akiwa mmojawapo?Je kuna uhakika gani kama hizo fedha za ufisadi hazitatumika katika kampeni ya mtoto.Lakini angalizo lingine ni kwa mtoto,kweli kama yeye ni mzalendo tofauti na baba yake basi angeona aibu kuingia kwenye siasa zilizoifedhehesha familia yao!Kwa upande mwingine huyu mtu Lowasa tunayemtuhumu kuwa hastahili kuiongoza Tanzaia katika nafasi yoyote ya kutumikia umma,Mbona bado anapeta kama mtu mwingine huru tuu?Tena mjumbe wa NEC ,CC na kamati kibao ?Si alipaswa kuwa katika mstari wa mafisadi walioko Keko na Segerea?
Sasa kama Lowassa hayupo huko na wala hatuna mpango wa kumpeleka huko?Kwa nini tumnyime haki yake ya kikatiba yeye pamoja na wanaomzunguka akiwemo mtoto wake?........)
Jambo moja ambalo akili ya kawaida haitaki kulikubali ni kuwa Lowasa ametutia katika hali ngumu kimaisha yeye akiwa kama kiongozi wa juu mwenye dhamana ya Watanzania,Akiwa na wadhifa wa Waziri Mkuu.Ina maaana kweli sisi wananchi hatupati uchungu kumfikiria tena huyu Lowasa kuingia madarakani hata kama ni kwa ngazi ya Kijiji tuu??Lowasa,Mtoto wake wote hawana tena nafasi wa kupewa dhamana ya kuongoza katika nchi hii kwani sifa kubwa ya uongozi wa kuwatumikia wananchi wameipoteza.Wananchi wa Monduli hata msiwasingizie kitu hawa maskini,Kwani hapo awali walidhani kuwa Lowassa angefaa hata kuwa Kiongozi wa jamii yao ya kimasai,Lakini waligundua kuwa wamdhaniaye ndiye kumbe siye.
Umefika wakati Watanzania kuelewa kwamba viongozi tunao wengi sana katika jamii zetu,Tatizo ni huo mwanya wa kuchaguliwa hasa kupitia katika chama chetu cha Mapinduzi.Chama kimechoka,kimekosa mwelekeo na dira kwa kuwa na wazee vikonngwe madarakani .Huku wakiwanyima nafasi vijana wenye upeo wa kutuvusha katika matatizo tuliyonayo.Chama cha watu wakongwe wasiotaka mabadiliko,Wenye uroho wa madaraka hata kufikia kurithishana madaraka!Iweje sisi wapiga kura tuendelee kulalama tuuu wakati tuna uwezo kabisa wa kuwatoa kina Lowasa na wengine wa aina yake? Kama ikishindikanika kwa sababu za ukongwe wa chamaTawala basi shime tuungane kuanzisha vuguvugu la waungwana ndani ya chama chetu na kukiacha njia panda kwa kuanzisha Cha Cha Fikira Endelevu ndani ya CCM.Kigumu sana Chama cha Mapinduzi.