Mtoto wa Lowassa kugombea ubunge Monduli?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
KUNA TETE KUWA LOWASSA ANAMWAANDAA MTOTO WAKE KUGOMBEA UBUNGE-MONDULI
Kutokana na kashfa nyingi zinazomkabili Lowassa anasita kugombea tena Ubunge-Monduli 2010,hivyo anamwandaa Mtu (Mtoto)wake kwa ajili ya kugombea.Hata hivyo wananchi wa Monduli wasioendekeza takrima wanaonekana kutaka waongozwe na Mbunge safi na asiye tokana na Mtu yeyote mwenye kashfa ya ufisadi au kashfa yoyote ile.Mwenye undani wa suala hili aturushie.
 
Last edited by a moderator:
Inaonekana kuwa Lowassa anajiaada kwa second bounce back. Lakini ni simple kuwa mtoto wake akiwa mbunge haitakuwa kwa maslahi ya watu wa Monduli kama ilivyokuwa Lowassa mwenyewe. I hope tukienda kule monduli juu inawezekana marehemu Sokoine atakuwa anarusha mateke kila akisikia jina la Lowassa linatajwa kuhusisha wilaya hiyo.
 
KUNA TETE KUWA LOWASSA ANAMWAANDAA MTOTO WAKE KUGOMBEA UBUNGE-MONDULI.

Mwanae ana haki ya kugombea kama walivyo raia wengine iwapo anatimiza masharti yanayomfanya kuwa mgombea halali. Lakini linalobaki ni maamuzi ya wananchi, wao ndio waamuzi wa mwisho kama kura zinaendeshwa kwa haki.
 
Thanks Mkuu...

Naona haki za kikatiba siku hizi zinapoteza maana hasa ukiwa mtoto wa mkubwa, bora wangesema mtoto wa Lowassa ajiandaa kugombea ubunge
 
KUNA TETE KUWA LOWASSA ANAMWAANDAA MTOTO WAKE KUGOMBEA UBUNGE-MONDULI
Kutokana na kashfa nyingi zinazomkabili Lowassa anasita kugombea tena Ubunge-Monduli 2010,hivyo anamwandaa Mtu (Mtoto)wake kwa ajili ya kugombea.Hata hivyo wananchi wa Monduli wasioendekeza takrima wanaonekana kutaka waongozwe na Mbunge safi na asiye tokana na Mtu yeyote mwenye kashfa ya ufisadi au kashfa yoyote ile.Mwenye undani wa suala hili aturushie.

'ANAMWANDAA' kivipi? this is rubbish! ipelekwe kwenye udaku inakostahili!
 
Kuna mtoto wa Sokoine ambaye watu wa Monduli wanamtaka sana awe mbuge wao. Lakini kwa influence ya Lowasa huyu jamaa amepelekwa kufanya kazi kwenye balozi zetu na umoja wa mataifa siku nyingi mno na huwa anahamishwa tu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ali mradi tu asirudi nchini ili Lowasa aendelee kulimiliki jimbo hilo. Mwenye data zaidi aongezee.
 
Tetesi nilizozipata ni kuwa Mtoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine ndie anaeandaliwa kugombea Ubunge wa Monduli. Habari nyingine pia zinathibitisha kuwa mtoto huyo sie wa kumzaa mwenyewe, bali ni yule aliyewahi kulelewa na Hayati Sekou Toure anaejulikana kama Dr. Ahmed Toure.

Kama mtoto wa Lowassa anataka kugombea, nadhani atakuwa ni Fredrick Lowassa. Sina uhakika kama anakidhi mahitaji sahihi ya watu wa Monduli. Tusubiri tuone.
 
Ikiwa za kweli au ni za Uwongo ,hilo si tatizo ,shida inapatikana pale wananchi hawafahamu kuwa mabadiliko yanayotakiwa si ya kiongozi bali mabadiliko yanayotakiwa ni kukiondosha Chama Cha Manyang'au na kukivua hatamu za Nchi.

Wananchi mliokuwa mmeshaamka na kuiona dunia anzeni kampeni sasa na kuwaarifu ndugu jamaa pamoja na marafiki popote walipo Tanzania kuwa wabadilike,wachague Chama kingine chochote ,na haswa huko kwenye viti vya wabunge ili kuimaliza nguvu CCM ni lazima CCM ishindwe kwa kishindo kwenye viti vya ubunge.
 
Tetesi nilizozipata ni kuwa Mtoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine ndie anaeandaliwa kugombea Ubunge wa Monduli. Habari nyingine pia zinathibitisha kuwa mtoto huyo sie wa kumzaa mwenyewe, bali ni yule aliyewahi kulelewa na Hayati Sekou Toure anaejulikana kama Dr. Ahmed Toure.

Kama mtoto wa Lowassa anataka kugombea, nadhani atakuwa ni Fredrick Lowassa. Sina uhakika kama anakidhi mahitaji sahihi ya watu wa Monduli. Tusubiri tuone.

Toure?!! uganga ukuu wa mkoa ameuweza?
 
Ana haki kama mtanzania yoyote yule, na akishinda itakuwa chaguo la watu wa monduli...waacheni watu wa monduli wachague, ndio demokrasia hiyo hata kama mtoto wa mkubwa, yeye hakuchagua kuzaliwa au kuwa mtoto wa mkubwa...
 
Kama huyo mtoto wa Lowassa sio FISADI kama baba yake na ana vigezo vyote vinavyo hitajika ili aweze kugombea, kutakuwa hakuna ubaya wowote. Kwa sababu kugombea ni haki yake ya msingi. swala liliko hapo ni kuchaguliwa na wananchi wa wilaya ya Monduli.
 
Lowassa amejitahidi sana kuhakisha kuwa mtoto wa Sokoine anakaa huko ubalozini Washington D.C. ili asije kugombea ubunge wa Monduli. Mimi nimewahi kuonana nae na siku moja nilintania juu ya suala hili, hakujicommit lakini alionyesha kuwa siku moja atarudi kugombea ubunge huko Monduli; Sintaona ajabu kama akija mwaka kesho!!
 
Recta,

..Dr.Salaash Toure aliwahi kugombea zamani na mpinzani wake akiwa Ole-Molloimet.
 
Recta,

..Dr.Salaash Toure aliwahi kugombea zamani na mpinzani wake akiwa Ole-Molloimet.

Duh... kwa tuliofanya kazi na Toure tunawapa pole wanamonduli, maana kama yeye anapita na anaingia kwenye kapu la potential ministers tumekwisha

Jamaa ni kushnehi che kichwani, labda mdomoni:rolleyes:
 
Ana haki kama mtanzania yoyote yule, na akishinda itakuwa chaguo la watu wa monduli...waacheni watu wa monduli wachague, ndio demokrasia hiyo hata kama mtoto wa mkubwa, yeye hakuchagua kuzaliwa au kuwa mtoto wa mkubwa...

ni kweli kuwa mtoto wa lowasa ana haki kama watanzania wengine, kinachotusumbua ni huyu anaye mwandaa yaani lowasa, je ule wizi aliofanya nakufaidika na mabilioni yasije yakawanunua wananchi wa monduli wakachagua bomu kwa kulambishwa takrima
 
Ikiwa za kweli au ni za Uwongo ,hilo si tatizo ,shida inapatikana pale wananchi hawafahamu kuwa mabadiliko yanayotakiwa si ya kiongozi bali mabadiliko yanayotakiwa ni kukiondosha Chama Cha Manyang'au na kukivua hatamu za Nchi.

Wananchi mliokuwa mmeshaamka na kuiona dunia anzeni kampeni sasa na kuwaarifu ndugu jamaa pamoja na marafiki popote walipo Tanzania kuwa wabadilike,wachague Chama kingine chochote ,na haswa huko kwenye viti vya wabunge ili kuimaliza nguvu CCM ni lazima CCM ishindwe kwa kishindo kwenye viti vya ubunge.[/QUOTE]

Nakubaliana na wewe kwa hayo mengine lakini kwa hilo nililoli hilight hapo kwa sasa haiwezekani si unaona hao wabunge wa upinzani kwenye suala la mitambo ya DOWANS wamelambishwa asali na sasa wao ndio wamekuwa watetezi kuliko hata hao manyang'au wa CCM? Tanzanians were DOOMED believe me hakuna pa kukimbilia.
 
Tunapinga hawa wa kuandaliwa wasio na uwezo maana hata Mkapa aliandaliwa na matokeo tuliyaona. Think Twice.

SAHIBA.
 
Back
Top Bottom