Mtoto wa kiume na mama yake wanalala Chumba Kimoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa kiume na mama yake wanalala Chumba Kimoja

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kameja, Mar 9, 2011.

 1. k

  kameja Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman huyu jamaa ni rafiki yangu wa karibu umri wak ni miaka 26. Alinishangaza aliponambia jana kua analala chumba kimoja na mama yake,nilikosa cha kumwambia kwasababu niliona ni maajabu.

  Jamani nipeni ushauri nimshaulije mwenzangu aweze kuhama? au unahis kuna nini hapo?
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmmhhhhh,unafikiri yeye hajui kuwa hilo si sahihi kwa umri wake?? ni maajabu kwa kweli,nyumba yao ina vyumba vingine au ndo kimjini mjini???wameanza lini?isisje ikawa wameanza zamani.......!!!wonders shall never end....oooohh!!

  muulize kwanza,anaelewa hilo ni kosa mshauri na msaidie kuhama kama unaweza...........!!!!!!!!!!!!
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Baba yake yuko hai?
   
 4. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama hali yao kimaisha ni tete, hilo so la kushangaa,,,,, kwani maisha ni jinsi unavyoishi we mwenyewe kwa hali ya kipato chako..
   
 5. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii taarifa haijakamilika hujasema kama wana chumba kimoja tu au labda mama ana matatizo ya kiafya anahitaji kuangaliwa usiku,hata mimi nililala chumba kimoja na mama alipopata stroke mpaka alipopata nafuu.
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Labda mamake anaogopa kulala peke yake au rafiki yako anaogopa kulala peke yake lol.


  Kama kaweza kukwambia analala chumba kimoja na mamake, basi ana uwezo wa kukwambia sababu inayomfanya walale chumba kimoja. Wewe ulifanya kosa kuto muuliza pale plae.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Uliza vizuri labda ni kipato maisha ya mijini yasikie tu.....omba Mungu hapo ulipo maana kuna mengine balaaaaaa.....tembea uoneee
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Unashangaa we una nyumba kubwa??????

  Hivi unaelewa hasa maana ya neno umasikini??????

  Hebu tembea uone kwanza.....kabla ya kushangaa mambo ya kawaida mno kwa
  watanzania wengi...
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Sababu ni nini?
  Kuna mmoja alikuwa analala na kaka yake halafu umri wao ulikuwa unakaribiana.
  Tatizo ilikuwa ni kipato.
  Ni jambo la kuhuzunisha sio kushangaza.
  Msaidie huyo rafiki yako.
   
 10. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Mwambie ahamie kwako ulale nae wewe chumba kimoja
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Yaani wewe unafurahisha sana (Kama si ya kutunga hii)

  Kwanza huyo rafiki yako kakueleza tu kuwa analala chumba kimoja na mama yake
  Pili wewe hujaomba ushauri unaanza kuuliza umshaurije?? Kakwambia ana matatizo hapo anapolala na mama yake??

  Punguza u**** utasutwa bure uvalishwe na khanga. Hayakuhusu kabisa hayo mambo ya nyumba za watu uyaache
   
 12. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ungejuwa navopenda wadada wenye hasira we acha tu.
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Labda ni maisha magumu...labda anampenda sana mama yake....labda anaogopa kulala mwenyewe..labda ni maagizo ya mganga!!We angalia mambo yako....siku akichoka au akiweza atajua mwenyewe cha kufanya maana wewe hata ushauri hajakuomba bado kwahiyo hayuko tayari kwa mabadiliko.
   
 14. s

  shosti JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ndio hali zetu hizo,sasa wewe kumsaidia ndo waja kumsimanga humu ama kweli rafiki mkia wa fisi....nashukuru mungu sina hata mmoja:spider:
   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kama si umaskini basi wametumwa hao,
   
 16. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #16
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha wewe acha mambo yako. Hujambo lakini
   
 17. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mi mzima sijue wewe.
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Niko poa kabisa.

  Ombi langu kwako: Hiyo signature weka font nzuri basi na sie wavaa miwani tusome kwa raha
   
 19. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ombi lako ni amri kwangu,naibadili.
   
 20. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #20
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Thanks you made my night stress free in my mind now.

  G9t
   
Loading...