Wakati sensa na makazi ikiibua siri ya wazazi kulala chumba kimoja, Wapo watumishi wa umma wanalala chumba kimoja

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
Kada zenye watumishi wa umma wenye kutoa huduma maeneo ya vijijini mfano afya,elimu na kilimo,kada hizi zinaongoza Kwa watumishi hao kulala chumba kimoja, kutokana na ukosefu wa nyumba za watumishi hao wa umma.

Utakuta nyumba moja ina vyumba vitatu na ni maalum Kwa familia moja lakini kutokana na ukosefu wa nyumba na kuwepo na makazi duni maeneo wanayohudumu, watumishi wa umma wanajikuta Wapo kwenye mkumbo huo,unaodhalilisha utu na faragha zao na kushusha molari ya kufanya kazi.

Tembelea mkoa wa Pwani maeneo ya pembezoni mfano maeneo ya pembezoni mwa wilaya za Kibaha Vijijini, Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji maeneo yake ya pembezoni yanatajwa ni maeneo yenye mazingira magumu kwa mtumishi wa umma kufanya kazi.
 
Ungeandika tu kwamba familia nyingi Tanzania zina hali mbaya kiuchumi hadi yanatokea mambo yanavunja maadili.Umasikini ni tatizo.Si kwa watumishi tu.Ni matabaka karibu yote.Na haijalishi mjini au vijijini.Na katika miji mikubwa,DSM unaongoza kwa watu kuishi(malazi yao)kijima.Nimeshuhudia bila kupewa dokezo na mtu.
 
Kama ni wa kujitolea na temporary sawa. Ila kama wanalipwa mshahara na stahiki zingine na wanalala hivyo basi hao ni wehu
 
Kama ni wa kujitolea na temporary sawa. Ila kama wanalipwa mshahara na stahiki zingine na wanalala hivyo basi hao ni wehu
Jamaa anataka wajengewe nyumba waishi bule mishahara yao isihusishwe..sijui mawazo ya wapi haya.
 
Akili za kiwehu kabisa.
Dar es salaam watumishi wa ofisi nyingi tunalipa Kodi kubwa za makazi bila kusaidiwa na mwajiri mpaka tunajenga. Kijijini kodi nyumba mzima sh. 50k kwa mwezi na bado wanarundikana kijumba kimoja cha bure
Jamaa anataka wajengewe nyumba waishi bule mishahara yao isihusishwe..sijui mawazo ya wapi haya.
 
Back
Top Bottom