Mtoto wa Kim Kardashian apata rafiki wa kiume

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
17,233
2,000
North-West--1024x585.jpg
MAISHA kweli hayana usawa! Mtoto wa mwanamitindo Kim Kardashian, North West ametengeneza ‘headlines’ kibao mitandaoni baada ya kupata rafiki wa kiume. North West (5), amepata rafiki huyo wa kiume ambaye ni mtoto mwenzake mwenye miaka 7, Caiden Mills.


Caiden pia ni mtoto wa rapa, Consequence ndiye aliyeanza kuonesha viashiria kuwa anatoka na North West baada ya kutumia vizuri Sikukuu ya Wapendanao kwa kumzawadia North boksi la Chokolate kutoka kampuni ya Tiffany.


North-West-.pngHata hivyo inaelezwa kuwa, Februari 6, mwaka huu Caiden aliwahi kufanya siri kwa kumzawadia North begi lenye rangi ya bluu na kuandika; “Piga kelele kwa North, binti wa kike nitakuona hivi karibuni.”

Baada ya maneno hayo, aliambatanisha na kikatuni kinachoonesha mtu akibusu. Wazazi wa watoto wote hawajafungukia chochote kinachoendelea kati ya North na Caiden.
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,521
2,000
This is absurd,haya sio mambo ya kuigwa kabisa, na cha kushangaza sasa hivi utaona baadhi ya watu nao wanapost mambo kama haya kwa watoto wao kwenye mitandao...
 

mangelengele

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,295
2,000
Acheni utoto, hamjawahi kulea. Kwa umri huo watoto wanaweza kuwa marafiki bila kujua aina ya urafiki wao. Inaweza kua ilikua birthday wakapiga picha nyie mkaleta story za udaku.
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
11,610
2,000
Watu bwana mnataka kuwakuza tu watoto wa watu. Hebu fanyeni kazi achene ushambenga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom