Mtoto wa Kikwete ashinda kwa kishindo

Huyu mtoto anashiriki au anashirikishwa kwenye siasa? Miaka 11 ni michache sana kunishawishi kuwa huyu mtoto anaelewa lolote khs siasa.
Kumbuka alichanguliwa bila yeye kuwepo ukumbini na pengine wala hakujua kama kuna uchanguzi unafanyika .
 

Mkuu mbona sasa unaharibu. Wakati sisi tunasoma enzi za chama kimoja kulikuwa na haja ya chipukizi ili kuwaweka vijana tayari kukitumikia chama cha mapinduzi na ndiyo maana kulikuwa na somo la siasa mashuleni na tulilazimika kukariri katiba ya CCM ili ufaulu mtihani wako wa siasa. Nakumbuka mimi nilipata "A" ya siasa Form four enzi hizo.

Sasa tukija katika vyama vingi, haya mambo ya kuwashirikisha "minors" kwenye siasa si kuwatendea haki hata kama ni mtoto wako uliyemzaa. Unaweza kumuandaa kuwa mwanachama wa CCM, CHADEMA au CUF nyumbani ila siyo kumuweka public.

Hebu tuseme kuwa kila chama kina haki sawa na CCM na wote waingie mashuleni kugombania watoto kujiunga na Chipukizi za vyama vyao si itakuwa vurugu?. Mi nafikiri suala la kuwafanya watoto kuwa active kwenye siasa ni zuri lakini kuwa "indoctrinate" ni kuwanyima haki zao za kidemocrasia.

Na utakuta sasa wazazi wenye mawazo kama haya wanakuwa hawana mawazo zaidi ya kuwaandaa vijana wao kuwa wajasiliamali kwenye siasa, waibe mali za umma basi. Mtoto kama huyu atakuwa wapi na mawazo ya ubunifu katika sayansi ili kuendeleza nchi wakati anajua kuwa njia pekee ya kufanikiwa katika maisha kama baba/mama ni kuwa mtawala tu.

Kila mtu ana haki kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa lakini katiba hiyo imeweka wazi kuwa awe ametimiza miaka 18, sasa mtoto wa miaka 11 au 12 huko si kuvunja katiba ya nchi?
 
Yale yale, chama cha ukoo na familia.wakifanya vyama vya upinzani mnapiga kelele mpaka mapovu yanawatoka midomoni,wao wakifanya ni sawa kabisa,kazi kweli kweli.DOUBLE STANDARDS
 


Ndiyo kuandaliwa CV maana baba yake hata jeshi hajui likoje muda wote ni kada hata shule yake ni jina maana amekuwa kada hadi sasa Nchi inaendeshwa kwa ukada .
 
Kama kweli tungekuwa na nia ya kuwatayarisha hawa watoto wawe viongozi wa kesho, huu ndio wakati mwafaka wa kuwasisitizia umuhimu wa somo la uraia. Huu ndio wakati mwafaka wa kuwaelimisha maana halisi ya Uzalendo na Utaifa na kwamba watu wanaweza kutofautiana bila kupigana kwani wote ni Watanzania kwanza. Huu ndio wakati wa kuwaeleza kwa nini nchi yetu, pamoja na utajiri wa asili, tuko tulipo kwa sababu ya makosa tuliyoyafanya katika maamuzi kama watanzania. Hawa watoto pamoja na wenzao wote nchini ndio taifa la kesho lakini tukianza kuwasokomezea itikadi za kichama katika huu umri ni kama tunajenga kuta kabla ya kuimarisha msingi wa umoja na mshikamano. Tusipoangalia tutajikuta tuna jumuiya ya wanajeshi wa CCM, jumuiya ya wafanyakazi wa CCM, jumuiya ya madaktari wa CCM and the list goes on. Ndio, kwani mbona tayari tuna watanzania wanaowabagua wenzao Ulaya, Asia na Marekani kwa kuanzisha eti jumuiya ya wana CCM London, New Delhi, Boston hadi Moscow - jamani !

Akifunga mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa aliutaka uongozi huo wa chipukizi kuwa watetezi wa watoto kwa kukemea maovu na manyanyaso wanayofanyiwa wenzao nchini ili waone jumuiya hiyo ndiyo kimbilio lao.
Wakati wa chama kimoja, hii hali ingeweza kuelezeka na kueleweka lakini hivi sasa mawazo kama haya yanatwaliwa zaidi na ujinga na ubinafsi.
Ndilo ninalolipinga hili - eti sio kujenga itikadi ya kubaguana bali umoja miongoni mwao. Lakini hapo hapo unataja kujenga chama chao - yaani at this early stage unamfundisha huyu kinda kwamba kuna chenu na chao na kudai unajenga umoja - ni umoja wa Watanzania au umoja wa CCM ?. Halafu kama vyama vingine navyo vitaiga au vinaiga navyo vikemewe hivyo hivyo tunavyokemea CCM. Tofauti ni kuwa kwa hivi vyama, pamoja na kwamba ni reaction tu kwa matendo ya chama tawala, bado hii peke yake haiwapi uhalali wa kufanya hivyo. Ni kama vile na wao waanze ufisadi kwa sababu CCM ni mafisadi, la hasha, mambo hayaendi hivyo. Je , hawa watoto wanaambiwa ukweli k.m. kuwa CCM walikomba pesa hazina kushinda uchaguzi ? Thubutu, sana sana watakuwa wanahalalishiwa vitendo kama hivyo, sasa tutakuwa tunajenga taifa la namna gani hapa ?
Uongozi ni wito
Good leaders are born, not moulded.
Viongozi wazuri huzaliwa, hawafinyangwi
 
wahenga walienda......lakini misemo yao haihitaji kamusi wala kuwapigia simu akhera..SIKIO LA KUFA, HALISIKII DAWA...
 
kuna mtoto mmoja wa miaka 11 alizimia baada ya kushindwa kwenye uchaguzi huo wa chipukizi.......!!!!
 
Hongereni Chipukizi wote mlioshinda na kupata nafasi ya kuwakilisha chipukizi wengine!

kama nafasi za watoto, hawapo tayari kuona mtoto wa mkulima akishiriki zaidi ya wanamtandao. Je huko juu, mnategemea nini, hapo wanajimu is an obvious alternative na kifo kwa wagombea is an avoidable by all necessary means.

IDUMU DOMOKRASIA!
 
mtoto wa jk ni lini amecheza gwaride au halaiki!!..jamani vigogo mnakaba hadi penalti...hizo ndizo fursa za watoto wa wakulima kuchomoza hasa wale wanaojitoa kuwachezea gwaride na halaiki....sasa mkibana hadi huko watoto wa wanyonge watachomozea wapi kuwa viongozi???
 
Nafikiri CCM wana-andaa vijana wao wa baadae...tunajua sote kwa namna moja au ingine tulikuwa huko chipukizi wakati wa chama kimoja.

Idea nafikiri kama wapinzani wangekuwa kweli wana-THINK mbali nao wao wangekuwa na chipukizi wao...in 15 years now tangu Mfumo wa Vyama Vingi, tungekuwa na Waelewa Upinzani wengi sana. na Sembuse hivi makelele yangekuwa madogo sana.

na kama Chipukizi wa Upinzani wangekuwa na nguvu zao, basi Serikali ya CCM ungewasikia wakipiga Marufuku Kuhusika kwa Watoto na Mambo ya Kisiasa!!!,

the by Wapinzani as Whole au Individual ni fursa zao kuandaa Kizazi kuwapa awareness hawa Chipukizi. na ndio Powerfull Tool. Tunaona watoto..just say 11/12 yrs..hawa after 7 to 8 years wanapiga kura wakiwa na uelewa madhubuti.
 

Si jambo la kushangaza maana Chipukizi siku hizi imebaki kwa watoto wa wateule ambao wanajua bila Chama wasingepata maisha bora. KWa wtoto wa walala hoi hata maana ya Chipukizi hawaijui.
 
Upuuzi mtupu,huo ni mwendelezo wa kuchezea fedha tu,chipukizi kitu gani wakati hospitalini kina mama wana lala chini hawana vitanda ni shilingapi zimetumika kufanya huo uchaguzi wa kipuuzi kabisa.hayo ni mambo yakuyasifia nayo? mtoto ana miaka 11!huyo mwenyekiti mtoto wa makala miaka 12,si ajabu watoto wote waliochaguliwa ni watoto wa viongozi.wanaacha kufanya vitu vya msingi wanakaa na kujadili kufanya mikutano ya ccm chipukizi kwa kutumia hela za wananchi.who cares?
 
hao ni vijana chipukizi wa ccm kitaifa au ni vijana chipukizi wa ccm ambao ni watoto wa viongozi ambao wapo katika ccm? kuna mtoto wa mlala hoi aliyepata nafasi ya kugombea? wenye dataz plz....

Cha msingi ni uwezo wa kubeba mzigo uliopewa. Kufikiri kuwa mtoto wa mlalahoi anastahili kuchaguliwa kuliko mtoto wa Kiongozi au tajiri au ....ni UBAGUZI kama ubaguzi mwingine wowote ikiwemo ubaguzi wa rangi.

Kibaya ni kumchagua mtu kwa sababu tu ni mtoto wa mkubwa,..lakini awe mtoto wa mkubwa au mdogo kama anafaa...why not?
 
Nami ngoja nitafute ile family tree huwenda ni kitukuu au kilembwe chenye kubeba jina la mheshimiwa.... then nikagombee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…