Mtoto wa Chacha Wangwe azua balaa CHADEMA

Mtoto wa Chacha Wangwe azua balaa CHADEMA

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
View attachment 106977View attachment 106978View attachment 106981

Kilichomo kwenye attachment kwa ufupi,

1. Upo mgogoro mkubwa wa kiuongozi ndani ya CHADEMA jimbo la Tarime, chanzo ni ubunge tangu mwaka 2008 alipofariki Chacha Wangwe.

2. Heche, Mwita Waitara wapo kwenye msuguano mkali wa nani hasa atakayegombea jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA. Mwita aligombea 2010 akabwagwa na Nyambari Nyangwine wa CCM, sasa anajiona ana mtaji wa watu huku Heche akimtuhumu Mwita kuwa ndio aliyepoteza jimbo.

3. Mtoto wa Chacha Wangwe aitwaye Zakayo ameibuka kwa kasi ya ajabu na kuonekana kuungwa mkono na wakazi wa Tarime kwamba ndiye mrithi wa viatu vya baba yake katika jimbo hilo kama atagombea kupitia CHADEMA au kupitia chama chochote.

4. Mwita bado haaminiki asilimia mia moja na wananchi wa Tarime kwa historia yake ya makuzi ndani ya CHIPUKIZI na UVCCM ambapo alifikia cheo cha katibu wa vijana mkoa kabla ya kujiunga na CHADEMA mwaka 2008.

5. Uongozi wa CHADEMA taifa unaonekana kumpendelea Heche ktk siasa za Tarime kitendo kinachomuudhi sana Mwita.

MY TAKE; HAWA VIJANA WANGEJIKITA KWENYE KUKIJENGA CHAMA BADALA YA KUKIMBILIA UBUNGE. UNAWEZA KUUTAMANI UBUNGE LAKINI UKAWA UMEKIHARIBU CHAMA UKAKOSA VYOTE.
 
hayo ni mawazo yako....chama kuwa na hazina ya vijana hodari ni ishara kuwa sasa kimeingia kabisa katika mioyo ya vijana na watu wa kizazi kipya.
ccm wamebaki na vibabu ambukizi na vijana wachache dhaifu na legelege.

249166_3194538225964_888897472_n.jpg
 
Mwaka 2015 ndivyo mnatakojua kuwa CCM ni legelege au vipi
 
hayo ni mawazo yako....chama kuwa na hazina ya vijana hodari ni ishara kuwa sasa kimeingia kabisa katika mioyo ya vijana na watu wa kizazi kipya.
ccm wamebaki na vibabu ambukizi na vijana wachache dhaifu na legelege.

249166_3194538225964_888897472_n.jpg

sasa hii picha ina uhusiano gani na mgogoro ndani ya CHADEMA
 
hawa ni wapiga dili hawa, wajasiriamali wa siasa. vijana wengi wanadanganyika na madaraka ndio mana wanaona chadema ni kibonde cha kufikia malengo
 
sasa hii picha ina uhusiano gani na mgogoro ndani ya chadema

kwa mtu ambaye asiyetazama mambo kwa kina hawezi ng'amua, CDM inafurahia vijana active kuendelea kukiunga mkono , wakati ccm inasikitika inapotokea vijana timamu, makini na wakakamavu wakijiunga nacho ndio nikatoa mfano wa ulegelege wa ccm
 
Magamba kwanini hamtumii muda wenu kusafisha magamba wenzenu badala ya kuongelea cdm muda wote?Hiyo picha inaonesha magamba walivyozeeka kimawazo
 
hayo ni mawazo yako....chama kuwa na hazina ya vijana hodari ni ishara kuwa sasa kimeingia kabisa katika mioyo ya vijana na watu wa kizazi kipya.
ccm wamebaki na vibabu ambukizi na vijana wachache dhaifu na legelege.

249166_3194538225964_888897472_n.jpg

hii ni kufuru_halafu huyu nape ndio kwanza anakaza shingo......
 
Gazeti la UDAKU la TAZAMA ni la LOWASA,TUNALIPUUZA KAMA TUNAVYO YAPUUZA UHURU,JAMBO LEO,HABARI LEO,NA TBC,magazeti hatuyanunui wala kuyasoma,TBCCCM hatuiangalii,Hivyo kuleta propaganda hapa za kwenye gazeti la udaku ni kujisumbua,Heche na Waitara pamoja na DOGO hawana ugomvi wala tofauti yeyote kwaajili ya Ubunge wa 2015,wanapigania kuikomboa nchi dhidi ya Wakoloni weusi ccm,na kujaribu kunusuru tembo ambao kinana anawamaliza.
 
CHADEMA ndio habari ya nchi sasa hivi.Gazeti,TV,Radio na vyombo vingine visipoandika habari yake haviuzi kabisa.Hebu chungulia humu ndani uone ni post ngapi zinahusu CDM na zile za CCM.Nyie subirini kuapishwa kwa Dr.Slaa,hivyo jiandaeni kwenda Segerea na hivi palivyojaa,mbona nawapa pole!
 
Ikulu ni mahali patakatifu. hawalali wazinzi pale
 
Back
Top Bottom