Mtoto wa Bakhresa afa katika Rally Zanzibar

kwa jinsi ninavyoijua serikali ya zenji sitoshangaa kama wakipiga marufuku mashindano haya kama walivyopiga maruufuku boxing
mimi naishauri kabisa iyapige marufuku mashindano haya mpaka pale watakapohisi kwamba wanaweza kuyadhibiti.mwaka jana kafariki mmoja na sasa mwengine .vipi tutauruhusu mchezo ambao kila unapochezwa unapoteza roho ya mtu.
 
M/Mungu amlaze pema.Haya mashindano ya wenye pesa..sio sie Hohehae...
Samahan hii habari inatakiwa iwepo hapa au la? Pia najiuliza hivi vifo vingapi vinaripotiwa namna hii? Halisi uliekuja na hii..watu wangapi wafa daily na hatuna data? nafikiri iwepo Chumba maalum ndani ya JF juu ya Taarifa za VIFO...unless forum itakuwa haina issue muhim
absolutely NO!
 
Huyu Marehemu alikuwa anasumbua sana gari lake alilotoboa exhaust makelele kila siku Kisutu pale
 
M/Mungu amlaze pema.Haya mashindano ya wenye pesa..sio sie Hohehae...
Samahan hii habari inatakiwa iwepo hapa au la? Pia najiuliza hivi vifo vingapi vinaripotiwa namna hii? Halisi uliekuja na hii..watu wangapi wafa daily na hatuna data? nafikiri iwepo Chumba maalum ndani ya JF juu ya Taarifa za VIFO...unless forum itakuwa haina issue muhim

dooh!!aiseee hayo mawazo yako...................
anyways pole kwa wafiwa woooote wenye misiba na Mungu azilaze Roho za marehemu pema peponi!
nasi tu njiani!
 
MUngu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ameen..bwana alitoa ,bwana ametwaa ..jina la bwana lihimidiwe,AMEN!!
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mhali pema peponi.
Serikali inabidi ifuate taratibu za kiusalama zinavyotakiwa.

Picha ya gari la marehemu baada ya ajali.
293381276.jpg
 
Quote: Chuma
M/Mungu amlaze pema.Haya mashindano ya wenye pesa..sio sie Hohehae...
Samahan hii habari inatakiwa iwepo hapa au la? Pia najiuliza hivi vifo vingapi vinaripotiwa namna hii? Halisi uliekuja na hii..watu wangapi wafa daily na hatuna data? nafikiri iwepo Chumba maalum ndani ya JF juu ya Taarifa za VIFO...unless forum itakuwa haina issue muhim

absolutely NO

Chuma na Under Age,
Muyasemayo ni sahihi kabisa, lakini nilipoweka katika habari mchanganyiko ikahamishiwa hapa katika siasa, naamini waliohamishia hapa wanafahamu fika (japo hatupendi) kwamba Bakhresa ana mguso mkubwa katika siasa za Tanzania na ndio maana viongozi wa juu wa serikali walifika katika mazishi hayo kama inavyoonekana katika picha ya mazishi Rais Karume amehudhuria. Si vyema kwenda katika undani maana hii si mada ya mjadala wa Bakhresa na siasa za Tanzania.
 
Attachments

  • KHALID-4.jpg
    KHALID-4.jpg
    101.6 KB · Views: 580
Mimi ni mshabiki wa rally, na kila nitazamapo, madereva huvaa helmet. Lakni ajali ni ajali, kazi ya Mungu haina makosa! Mungu amlaze mahali pema, awape faraja wafiwa, amen!
 
Kitia swali lako liliulizwa na kujibiwa kama ifuatavyo
Quote:
Makosa ya waandaaji inakuwaje watoto wanakatisha barabara ambayo magari hayo yanapita? Badala ya kufa yeye angeweza kuua hao watoto.

Hivi ni kweli hakuvaa Helmet? Ilikuwaje wakamruhusu aondoe gari bila kuvaa Helmet? Hata huyo msaidizi wake ilikuwaje akakubali waendeshe gari kwenye mazingira hayo?

Marehemu apumzike kwa amani.

Mtanzania, wanasema alivaa helmet ila aligonga mti wa mnazi likapasuka
 
Michezo Habari nyingine zaidi!
Serikali yasimamisha mbio za magari Zanzibar
Suleiman Pandu, Zanzibar
HabariLeo; Tuesday,December 18, 2007 @00:06

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesitisha kwa muda usiojulikana kufanyika mashindano ya mbio za magari visiwani hapa hadi hapo waandaaji wake watakapopata njia na kuwepo kwa miundombinu ya barabara ambazo hazitakuwa na muingiliano na watu.

Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna, alisema hayo jana ofisini kwake Migombani, kwamba tangu kuanza kwa mashindano ya mbio za magari miaka mitatu iliyopita imeonekana zaidi kuwapo kwa hasara, ikiwamo ajali ambazo zimesababisha kupotea kwa maisha ya binadamu.

“Tumeona tangu kuanza kwa mbio za magari miaka mitatu iliyopita hakujaonekana faida yake....lakini tumeona hasara zaidi ikiwamo kupotea kwa maisha ya binadamu,” alisema Shamuhuna.

Shamuhuna alisema moja ya faida kubwa ya kuwapo kwa mashindano ya magari ni kuimarisha sekta ya utalii, lakini kwanza kuzingatia maisha ya watu na sio biashara.

Alisema serikali imezingatia mazingira ya mbio za magari kwa hapa visiwani na kuona kwamba njia zinazotumika kwa gari hizo pia zinatumiwa na wananchi.

Tamko la Serikali ya Mapinduzi limekuja siku moja baada ya kutokea kifo cha mmoja wa washiriki wa mbio za magari za Zamani Zanzibar Kempinski Motar Rally ya Km 300, Khalid Saidi Bakhressa, aliyefariki dunia juzi baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga nguzo ya taa Pongwe Wilaya ya Kati Unguja alipokuwa katika harakati za kuwakwepa watoto waliokuwa wakicheza barabarani.

Bakhressa alikuwa akiendesha gari la kisasa aina ya Subaru Impreza N.12 lenye thamani ya Sh milioni 50 akiwa na dereva msaidizi Mosses Matovu wa Uganda aliyepata michubuko sehemu za mkono.

Bakhressa alizikwa juzi katika kijiji cha Kiyanga wilaya ya Magharibi Unguja na Rais Amani Abeid Karume aliongoza mamia ya waombolezaji katika maziko hayo.

Hiyo ni ajali ya pili kutokea tangu kuanza kwa mashindano ya magari miaka mitatu iliyopita, dereva Nazir Khan alifariki dunia baada ya gari lake kupinduka katika eneo la barabara hiyo ya Uzini, wilaya ya Kati Unguja.

source..http://dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=5953
 
NAIPONGEZA SERIKALI KWA HATUA MLIOCHUKUA, ILA MARA NYENGINE KUWENI MAKINI KABLA MAMBO HAYAJATIA MADHARA.

MSIWE KAMA WATU WA KUSADIKIKA HAMTAFUTI FIMBO MPAKA MUUMWE NA NYOKA
 
I think serikali ya zanzibar imemake big shot, zanzibar infrastracture does not support this non sense races. The organizer need to find other strategy which will put safety on first place, and profit next.
 
Michezo Habari nyingine zaidi!
Serikali yasimamisha mbio za magari Zanzibar
Suleiman Pandu, Zanzibar
HabariLeo; Tuesday,December 18, 2007 @00:06

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesitisha kwa muda usiojulikana kufanyika mashindano ya mbio za magari visiwani hapa hadi hapo waandaaji wake watakapopata njia na kuwepo kwa miundombinu ya barabara ambazo hazitakuwa na muingiliano na watu.

Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna, alisema hayo jana ofisini kwake Migombani, kwamba tangu kuanza kwa mashindano ya mbio za magari miaka mitatu iliyopita imeonekana zaidi kuwapo kwa hasara, ikiwamo ajali ambazo zimesababisha kupotea kwa maisha ya binadamu.

“Tumeona tangu kuanza kwa mbio za magari miaka mitatu iliyopita hakujaonekana faida yake....lakini tumeona hasara zaidi ikiwamo kupotea kwa maisha ya binadamu,” alisema Shamuhuna.

Shamuhuna alisema moja ya faida kubwa ya kuwapo kwa mashindano ya magari ni kuimarisha sekta ya utalii, lakini kwanza kuzingatia maisha ya watu na sio biashara.

Alisema serikali imezingatia mazingira ya mbio za magari kwa hapa visiwani na kuona kwamba njia zinazotumika kwa gari hizo pia zinatumiwa na wananchi.

Tamko la Serikali ya Mapinduzi limekuja siku moja baada ya kutokea kifo cha mmoja wa washiriki wa mbio za magari za Zamani Zanzibar Kempinski Motar Rally ya Km 300, Khalid Saidi Bakhressa, aliyefariki dunia juzi baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga nguzo ya taa Pongwe Wilaya ya Kati Unguja alipokuwa katika harakati za kuwakwepa watoto waliokuwa wakicheza barabarani.

Bakhressa alikuwa akiendesha gari la kisasa aina ya Subaru Impreza N.12 lenye thamani ya Sh milioni 50 akiwa na dereva msaidizi Mosses Matovu wa Uganda aliyepata michubuko sehemu za mkono.

Bakhressa alizikwa juzi katika kijiji cha Kiyanga wilaya ya Magharibi Unguja na Rais Amani Abeid Karume aliongoza mamia ya waombolezaji katika maziko hayo.

Hiyo ni ajali ya pili kutokea tangu kuanza kwa mashindano ya magari miaka mitatu iliyopita, dereva Nazir Khan alifariki dunia baada ya gari lake kupinduka katika eneo la barabara hiyo ya Uzini, wilaya ya Kati Unguja.

source..http://dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=5953

hivi mnajua kama serikali ya ZNZ ilipiga marufiku mchezo wa BOXING?
 
bumping??ndio mchezo gani huo??au ndio ule nijuao mimi??duh kama na huo umepigwa marufuku basi znz kuna shughuli sio ndogo

wakati wa mh aboud jumbe wenzetu kule bara kulikuwa kuna wanaume huweka manywele mikubwa, kisha huvaa mashati yanawabana na suruali ambazo chini zimechanua jina lake nimelisahau sasa wakienda dancini wanaume hucheza kisha wakapigonganisha viuno vyao.

mheshimiwa aboud ajumbe akaupiga marufuku mchezo huo, akasema mchezo wa kibaradhuli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom