Mtoto wa Bakhresa afa katika Rally Zanzibar

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
1,250
Kuna habari kwamba mtoto wa Said Bakhresa amefariki katika ajali ya gari kwenye mashindano mjini Zanzibar. Hii ni mara ya pili kwa rally kuua Zanzibar, mwaka jana alikufa Nasir Khan katika mashindano hayo. Hata hivyo kuna utata, Wako wanaosema aliyekufa ni Yussuf Said Bakhresa na wengine wanasema aliyekufa ni Khalid Said Bakhresa. Khalis ndiye ameonekana katika gazeti la The Citizen na ndiye anayefahamika kuwa dereva mashuhuri
 

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
0
Yaaa ni kweli ajali imetokea, huyu Khalid nilimuona akihojiwa kwenye TV muda mfupi kabla ya mashindano kuanza. Mugu amlaze mahala pema.
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
1,250
Yes, ajali imetokea na imethibitishwa na Daktari wa mashindano hayo DK. Karrim Zam.

Imetokea katika Kijiji cha Dongwe Mkoa wa Kusini Unguja wakati akiwa kasi Khalid alijaribu kupunguza mwendo kwa kuwakwepa watoto waliokuwa njiani na kujikuta akipinduka. na alipasuka kichwa na kusababishwa na kutoka damu nyingi, wanasema imetokea saa 3:45 asubuhi wakati Yussuf akijaribu kunusuru maisha ya watoto waliokuwa wakikata njia kwa kupunguza mwendo lakini kwa bahati mbaya gari lake likapinduka.

marehemu tayari alikuwa ameshatumia kilomita 26 tangu kuanza kwa kituo cha kwanza katika hoteli ya Zamani Kempiski iliyopo Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Msaidizi wake Raia wa Uganda Moses Matovu, hajapata madhara makubwa lakini alionekana kuchanganyikiwa kutokana na ajali hiyo.Hili ni tukio la pili la madereva wa mbio za magari kupoteza maisha tangu yalipoanza Kisiwani hapa ambapo Nassir Khan alifariki dunia mwaka jana wakati wa mashindano kama hayo.
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
1,250
Picha ya Khalid.. iliyotoka katika gazeto la The Sunday Citizen
 

Attachments

  • khalid.jpg
    khalid.jpg
    76.5 KB · Views: 1,167

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
2,000
Makosa ya waandaaji inakuwaje watoto wanakatisha barabara ambayo magari hayo yanapita? Badala ya kufa yeye angeweza kuua hao watoto.

Hivi ni kweli hakuvaa Helmet? Ilikuwaje wakamruhusu aondoe gari bila kuvaa Helmet? Hata huyo msaidizi wake ilikuwaje akakubali waendeshe gari kwenye mazingira hayo?

Marehemu apumzike kwa amani.
 

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
0
Labda hawakuwa na "Safety Expert" kwenye kamati ya maandalizi. Ni muhimu sana kuajiri mtu mwenye utaalamu wa usalama. Lakini hata matrafiki pia wanajua jukumu hilo.

Sijui kunkuwaje !!
Tunabakia kazi ya Mungu.
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
1,250
Makosa ya waandaaji inakuwaje watoto wanakatisha barabara ambayo magari hayo yanapita? Badala ya kufa yeye angeweza kuua hao watoto.

Hivi ni kweli hakuvaa Helmet? Ilikuwaje wakamruhusu aondoe gari bila kuvaa Helmet? Hata huyo msaidizi wake ilikuwaje akakubali waendeshe gari kwenye mazingira hayo?

Marehemu apumzike kwa amani.

Mtanzania, wanasema alivaa helmet ila aligonga mti wa mnazi likapasuka
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
1,250
Kuna taarifa kwamba wanazika leo leo huko Zanzibar,, walioko Unguja tufahamisheni
 

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,552
0
kwa jinsi ninavyoijua serikali ya zenji sitoshangaa kama wakipiga marufuku mashindano haya kama walivyopiga maruufuku boxing
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,178
2,000
kwa jinsi ninavyoijua serikali ya zenji sitoshangaa kama wakipiga marufuku mashindano haya kama walivyopiga maruufuku boxing

yeah ss zanzibar hatupendi michezo inayohatarisha maisha ya watu.

kwa hio sitoshangaa kupigwa marufuku au kuchukua hatua za usalama zaidi
 

Mbalamwezi

JF-Expert Member
Sep 30, 2007
800
225
RIP brother. Poleni nyote mlioguswa na msiba huu.

Serious challenge to improve safety standards.
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,217
1,225
Nascar, huwa inatokea mizinga ya kutisha......lakini toka afe Dale Einhardt, Sr, taratibu zilibadilika na hajafa mtu tena!!!. Mizinga gari mpaka linakatika na kushika moto lakini suka anatoka shwari.......kupiga marufuku haitakuwa soln nzuri, suala hapa ni kuimarisha usalama wa madereva na raia.
Pole kwa familia!!!.
 

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
0
M/Mungu amlaze pema.Haya mashindano ya wenye pesa..sio sie Hohehae...
Samahan hii habari inatakiwa iwepo hapa au la? Pia najiuliza hivi vifo vingapi vinaripotiwa namna hii? Halisi uliekuja na hii..watu wangapi wafa daily na hatuna data? nafikiri iwepo Chumba maalum ndani ya JF juu ya Taarifa za VIFO...unless forum itakuwa haina issue muhim
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom