Mtoto wa baba, mtoto wa mjomba

Mtoto wa baba, mtoto wa mjomba

Babuyao

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2009
Posts
1,740
Reaction score
274
Katika jamii (makabila) nyingi hapa Tanzania watoto wanaozaliwa katika ndoa wanakuwa wa ukoo wa baba (Patrilineal system), na baba mzazi ndiye mwenye watoto. Lakini pia kuna jamii chache ambazo watoto wanaozaliwa wanakuwa wa ukoo wa mama (matrilineal system), yaani watoto wanakuwa wa wajomba (kaka za mke wa ndoa).
Swali 1: Nini faida na hasara ya kila system za hapo juu?
Swali 2: Je, system hizi bado zina uzito katika karne hii ya 21?

Karibu wana JF.
 
jamii ambazo zinatoa jina la ukoo kutokea upande wa mama wanakuwa na logic hii, ni kwamba mtoto atakaezaliwa lazima atakuwa na damu ya mama na mama tu ndio anajua ukweli wa kuwa mtoto ni wa nani, na ushahidi kwamba mtoto ni wa huyo mama ni kwa kila mtu anakua ameuona wakati mama akiwa mjamzito, wao wanaamini kuwa mama anaweza kuwa kacheat na kuweza kumbambikia mtoto mwanaume yoyote, hivyo ili kuondoa utata mtoto anapewa jina la ukoo wa upande wa mama
 
Kuliweka sawa si twambie ni makabila yapi? hapa hujawa wazi katika bandiko lako
 
jamii ambazo zinatoa jina la ukoo kutokea upande wa mama wanakuwa na logic hii, ni kwamba mtoto atakaezaliwa lazima atakuwa na damu ya mama na mama tu ndio anajua ukweli wa kuwa mtoto ni wa nani, na ushahidi kwamba mtoto ni wa huyo mama ni kwa kila mtu anakua ameuona wakati mama akiwa mjamzito, wao wanaamini kuwa mama anaweza kuwa kacheat na kuweza kumbambikia mtoto mwanaume yoyote, hivyo ili kuondoa utata mtoto anapewa jina la ukoo wa upande wa mama
Mila hii na teknolojia tulio kuwa nayo leo sidhani kama inafaa.
 
Kwa nini haifai?

Mkuu SMU, nimejibu kulingana na Mtoa hoja hapa chini.
jamii ambazo zinatoa jina la ukoo kutokea upande wa mama wanakuwa na logic hii, ni kwamba mtoto atakaezaliwa lazima atakuwa na damu ya mama na mama tu ndio anajua ukweli wa kuwa mtoto ni wa nani, na ushahidi kwamba mtoto ni wa huyo mama ni kwa kila mtu anakua ameuona wakati mama akiwa mjamzito, wao wanaamini kuwa mama anaweza kuwa kacheat na kuweza kumbambikia mtoto mwanaume yoyote, hivyo ili kuondoa utata mtoto anapewa jina la ukoo wa upande wa mama
 
Mimi niliwahi kusindikiza msafara wa kwenda kuoa hapo Msoga (km kama 15 hivi kutoka Chalinze). Muoaji (ambae kwa asili msukuma) alikuwa anaoa pale kijijini (kama sikosei pale wapo Wakwere). Baada ya shughuli zooote kidogo tunyimwe mke baada ya baba mzazi wa mume mtarajiwa kumkaribisha binti kwenye ukoo wao na kusema karibu sana kwenye ukoo wa Masanilo (jina limebadilishwa). Mjomba wake bi harus mtarajiwa alikuja juu sana na kutoa hotuba namna ambavyo hata watoto wakizaliwa wanapaswa kuitwa majina (ubini) wa kwa mama yao. Sasa wale ndugu zangu wasukuma (nafikiri walikuwa wanyantuzu) walikuja juu kama moshi wa kifuu. Anyway, to make it short, ilibidi itumike hekima na busara ya ziada kusawazisha mambo. Nilitoka pale nimepigwa butwaa, it was my first time kuona kitu kama kile.
 
Mimi nafikiri ni wakati mke na mme tuu ndio waanze kuamua majina ya mtoto. Au watoto waitwe majina matatu first name, mother's surname/first name then fathers surname/first. Kama wenzetu wa spanish wanavyofanya na wengineo
 
kwenye jamii hizo ambazo mjomba ndo mwenye nguvu,matunzo ya watoto hao hutoa nani?
 
Watoto ni wa mjomba. Wewe baba wa damu hata ukitoa matunzo wale watoto ni wa mjomba (ukoo wa mama). Wewe unabaki dume la mbegu tu. Ndoa ikivunjika watoto wanaenda nao mama kwao (kwa kaka zake).
 
jamii ambazo zinatoa jina la ukoo kutokea upande wa mama wanakuwa na logic hii, ni kwamba mtoto atakaezaliwa lazima atakuwa na damu ya mama na mama tu ndio anajua ukweli wa kuwa mtoto ni wa nani, na ushahidi kwamba mtoto ni wa huyo mama ni kwa kila mtu anakua ameuona wakati mama akiwa mjamzito, wao wanaamini kuwa mama anaweza kuwa kacheat na kuweza kumbambikia mtoto mwanaume yoyote, hivyo ili kuondoa utata mtoto anapewa jina la ukoo wa upande wa mama

we myao nini!!teh teh teh
 
Back
Top Bottom