Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo: Jitahidi kumlea katika njia impasayo!

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854
Na: Denis Mpagaze
______________________________
Kulea ni kazi nyie. Binti mmoja alilelewa katika maadili mazuri sana, ukubwani akapata mchumba kama unavyojua tena binti mwenye tabia nzuri kuolewa ni kugusa tu maana hata mwanaume mwenye tabia mbaya atataka mke mwenye tabia nzuri. Basi bwana binti akachumbiwa na hatimaye akaolewa. Siku tatu tu baada ya ndoa binti akarudi nyumbani akiwa na hasira huku analia. Wazazi walipomuuliza kulikoni akasema aliyemuoa ana tabia mbaya sana. Hakutegemea. Walipomuhoji ni tabia gani hiyo, akasema yule kijana anataka wafanye matusi wakati kimaadili haikubaliki.

Faulo katika malezi ni nyingi.Unafika kwenye familia fulani kusalimia vitoto havina adabu vinakuja vinakupokonya simu vinakimbia nayo kucheza game bila hata kukusalimia. Badala mzazi akemee, utasikia, "Mmmmh yaani hawa ndivyo walivyo, watundu kweli!" Vitoto vingine vinakufuata ulipokaa vinaanza kukufinya ili utoke kwao maana mama kapika wali kuku, havitaki ule. Utasikia "toka kwetu." Ukikigusa kidogo kinaangusha kilio utadhani kimechinjwa! Malezi haya! Loh!

Kuna wazazi wako busy kuharibu watoto wakidhani ndiyo malezi. Unakuta mama anaenda kuogelea na mtoto wake wa kiume akiwa na bikini, anajibinuabinua mbele ya mtoto wake wa kiume. Baada ya muda kijana naye anaanza kujibinua binua mbele za watu. Akija kuwa punga mnaanza kusema huyo mtoto alizaliwa na hormone za kike. Mtoto wa kiume kalegea hadi macho! Inatisha nyie!

Huu uzungu mwingiii kwenye hamna unatuharibia taifa la kesho. Mama anakiss na mwanaye wa kiume wa miaka hata tisa, analala naye chumba kimoja kwa sababu tu ni single mother. Halafu baba wa mtoto yupo anajidai mtaani kwamba ana mtoto wa kiume. Anatunzwa na single mother. Hopeless kabisa. Una mtoto hujui anaishije! Kijana aliyelelewa hivi akipewa mke hawezi kummudu. Atamkimbia tu.

Mtoto ni wako halafu kumtuma hata dukani mpaka umbembeleze. Utasikia "Jamani Mami, si unifatie vocha mwanangu, simama basi eeee." Mtoto anajibu "Mamy si unaona mimi naangalia katuni? Basi hapo anaitwa dada wa kazi afuate hiyo vocha halafu wakiita wazazi bora na wewe unatoka mbele. Mzazi bora au mzazi balaa. Mtoto anatumwa vocha akichelewa kuinuka muinue kwa kibao! Hayo ndiyo malezi halisi ya Kiafrika. Hayo malezi ya kuazima ughaibuni msituletee huku.

Sasa hivi kuna familia ukienda kuwatembelea hadi aibu. Vitoto havisalimii hadi mama aseme Tony, umemsalimia anko? Kitony ndiyo kinasalimia kwa dharau, shikamoo anko bila hata kukuangalia. Kiko busy na katuni za mashoga. Zamani usiposalimia ulitandikwa kibao usalimie, ukilia ulitandikwa unyamanze.

Siyo siku hizi litoto linabembelezwa kwa smart phone ya mama yake. Yaani ili litulie basi lazima lishinde na simu ya maza, na meseji za mama linasoma. Ndiyo linasoma. Siunajua vitoto vya siku hizi vinaanza shule vikiwa vidogo? Miaka minne linajua kusoma kila kitu. Ukilipa simu linaingia mpaka sehemu ambazo hujawahi kufika.

Mko kwenye mazungumzo mazito na wageni mara kitoto kinalilia kuwekewa katuni! Mnakiwekea, halafu kinashangilia kwa nguvu hadi kuvuruga mazungumzo yenu. Unakatisha mazungumzo kukibembeleza kitoto kipunguze sauti utakinunulia mdoli ndiyo kinatulia. Aisee malezi ya sasa ni mtihani mkubwa hasa ukilegeza akili.

Hivi unajua watoto wanajua uwezo wako wa kufikiri ndiyo maana hata ukiwauliza nikuletee nini anakwambia niletee biskuti, icecream na big G? Hawezi kukwambia niletee kitabu cha hesabu kwa sababu hujamfundisha kutumia akili, umemfundisha kulakula tu na kuchezea simu! Anza kubadilisha fikra za watoto wako basi waanze kukuagiza hata vitu vya kujenga akili!

Katika hili kila mzazi atafute njia anayoona itasaidia kunusuru watoto wake wawe na uwezo wa kuchambua mambo na kufanya maamuzi sahihi. Eti mtoto akiwa na baba au hata mama analilia kitu dukani na hasikii mpaka akipate. Msipompa anazila kula. Kwamba mama anajisikia faraja kumtimizia mtoto kila anacholilia hata kama ni kwa kukopa. Mtoto anakua mkubwa na akili za kufanyiwa kila kitu.Tunawalea watoto kama yai kwenye hamna.

Halafu huu ujinga huwezi kuukuta kwa matajiri. Utaukuta kwa kina sisi tunaoparangana kuishi. Watoto wanavalishwa pamba za kufa mtu wakati huo account za wazazi wao zinasoma masafa ya redio, salio lako ni Sh 93.7. Hawa ikitokea dharula wanavyohaha kutafuta wa kuwakopesha huwezi amini kama ndiyo wenye watoto wanaopiga pamba za kufa mtu! Sikatazi kupiga pamba,ila tukumbukage na kuweka akiba kwa ajili ya dharula.

Mtoto anatakiwa ajue mipaka yake lakini kama wazazi wanageuka yes man kwa kila kitu inakuwa sio poa kabisa.

Wazazi wafundisheni watoto wenu katika njia ifaayo maana wakikua hawataiacha inasema Biblia Takatifu. Hakuna neema itakayo toka Mbinguni kuja kumuokoa mwanao au kumlinda asiwe mtu wa hovyo.

Hili wimbi la watoto kuwaua wazazi wao ni matokeo ya ulezi mbovu. Hata ongezeko la mabinti kuzalia nyumbani ni mafunzo kutoka kwa wazazi wao. Sasa hivi imekuwa fashion.

Sikiliza! Ukimdekeza mtoto wako kizembe atakudhalilisha mbele ya watu hutoamini
Kumbuka ukicheka na mbwa atakufuata hadi msikitini. Uzuri mtoto akifanya upuuzi wanauliza ni mtoto wa nani? Aibu kwako mzazi wako!
 
Wazazi wameachia dunia iwasaidie kulea...

Wanadekeza watoto wakijua wanawasaidia kumbe wanawaharibu...

Mithali 23: 13

Neno la Mungu linasema...
Usimnyime mtoto wako mapigo maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
 
Haahaa,humu hutawaona,kwenye hii mada watajifanya wako upande wa mleta mada. Humu wamejaa masnitch,itategemea ulivyojidhihirisha.....njooni nyie si huwa mnajidai MNA uzungu mwingi?
 
Back
Top Bottom