Mtoto Pendo wa IFM

Mtoto Pendo wa IFM

Status
Not open for further replies.
Haloo! hilo kweli fundisho. Ila utaweka vipi appointment na mtu usie mjua? jamani tubadilike, hiyo michepuko haifai.
 
Nilikua na muongopea mie nilipanga ni mlie mijiela sasa nitimtajia kuwa na somea Accountant siange kata mwawasiliano na mimi hata kabla hatuja panga kuonana maana angeona huyu demu anasomea Accountant mambo ya kufunga makabati siutani angetoka ndukiii coz angeona ningeapply hiyo kwake hahahah
hahahahaha mbona kaka pita ulimwmbia unasoma BAF?
 
Niaje wadau
Jumanne wki iliyopita Nikiwa kwenye harakati zangu za kusaka watoto wa nchi hii Mara naona namba mpya ina ingia kwenye simu yangu

Mimi:Hello
Yeye (sauti ya kike nyororo) :Hello nani?
Mimi: Kwani unamtafuta nani?
Yeye: Samahani kaka nimekosea namba
Mimi: Hahaha Hujakosea dada bila shaka unanitafuta mimi naitwa Peter nafanya kazi TPA
Yeye:Jamani Peter nimefurahi sana kukufahamu me naitwa Pendo nasoma IFM BAF
Mimi: Nami nimefurahi kukufahamu Pendo da unaishi pande zipi
Yeye: Naishi hostel za kigamboni nawewe je?
Mimi:Me naishi Sinza Palestina
Yeye:Jamani Peter,unaishi na nani?
Mimi:Mwenyewe kibachelor
Yeye:Jamani,karibu mwaya
Mimi:Asante lini utakuwa na muda?
Yeye:Weekend, Hivi upo wasap
Mimi:mm huwa nipo ila kwa sasa simu yangu imepata hitilafu kidogo hivo sipo kwa sasa
Yeye:Owky I hop to see yaa Peter,si utakuja kunitembelea my dear?
Mimi:Yap ntakuja jmosi siunajua tunafanya half day,husiwaze
Yeye:bye Peter (simu ikakata)

Baada ya mazungumzo hayo kamanda nikajisemea lazima huyu mtoto nimtimbie kwa gharama zozote hata kama nimepinda ntakopa kwa masela hata buku ten ya kuzugia. Yote niliyomwambia ni uongo hakuna cha kazi TPA wala siishi Sinza me naishi zangu Pugu kinyamwezi tangu nimalize chuo mwaka sasa sijawahi kupata hata kibarua cha kulipwa buku kwa siku. Kama kawa mtoto Pendo anatuma sms gud 9t dear,ushakula? ushatoka ofisn,upo jam una drive.na sms nyng nzuri
Da kamanda jmosi ikafika mida ya saa 4 mapema nikala DCM yangu taratibu huyo mida ya saa 7 nilikuwa zangu feri namsikilizia mrembo Pendo anishtue akitoka discussion.Mfukoni ilikuwa imebakia buku 6 na mia 3 me mwenyewe ubao ushaanza kute8t coz chai sikunywa. Baada ya nusu saa hivi akanipigia bado upo kwa ofis My baby Peter.nikamwambia ya but ndo natoka ntadrive fasta i hop baada ya dk 10 ntakuw hapo kgambonino. akaniuliza so itabidi nikusubili hapa njia ya kutokea feri ili twende beach maana jua kali, hvi gari lako peter linarangi gani?coz hapa na friends wagu watatu niliokuwa nao discusion wanataka wakuone my babyby.Du Nilichoka na nilihisi kigugumizi mwanaume yamenikuta ila nikamwambia ni Nissan Murano Nyeusi. Kipindi tunaongea hayo Pantoni linatia nanga kigamboni me nilitoka fasta kumpimia mapema, nikasogea hadi pale lango la kutokea magari ili nimwone Pendo. Du nilichoka sitaki kumkosoa mungu but it was out of my expectation sifa zote nilizomjengea hana hata moja. Baada ya hapo nikazima simu yangu nilirudi kwenye panton leo ndo nimeiwasha .

SOMO
Hivi ni msichana gani mrembo na mzuri atahangaika kumtafuta mtu ambaye hajawahi kumwona?wakati kuna mijidume kibao imemtokea na yenye pesa ikaipiga chini Tujifunze tuchukue hatua namba ambayo huijui iache.

ni shidaaaaaasa
 
Mbona mnapenda haribu vyuo vya watu sa ifm na baf wapi na wapi tungeni hadith zenye ukwela hakuna baf ifm kuna bbf
 
Wenzako wajanja wanasuuza rungu hata kwa huyo mwenye sura kama karabai la wavuvi...

Mvuvi akitupa nyavu hata kama alitaka avue tasi au mkole, wakiingia humo kibua, kolekole hawezi waachia...

Sasa we subiria huyo mwenye sura kama tachi skrini ya Aipad miaka mia tisa wakati hata ngawira yakupiga chenga...
 
huyu atakuwa ni mimi tu... nilikasirika sana wakati huo nimetoka moshi nilikuja kumsalimia mama mdogo unaroho mbaya sana

hAA Haa pole sn miss chaga kama kweli ndo wewe. Usjali nipm namba yako nikrushie japo kijivocha cha kukusababishia usumbufu
 
Last edited by a moderator:
Huyo pendo namfahamu kabisa wa IFM..Ni mwembamba sana amesoma Olevel, primary. Morogoro mjini.. Anaitwa pendo msafi..ri..! Km Ni yeye Ni pm now., she used to be....
 
Heu tupe mambo yake ya chini, taarabu imo au haimo?

Maana naona mambo ya juu tushaambiwa ni kama nyago la kumtishia mtoto ale...

Huyo pendo namfahamu kabisa wa IFM..Ni mwembamba sana amesoma Olevel, primary. Morogoro mjini.. Anaitwa pendo msafi..ri..! Km Ni yeye Ni pm now., she used to be....
 
badilisha jina kwani kuna mtu anaitwa hivyo hivyo IFM na yupo hostel Kigamboni, embu andika jina "Okonko wa IFM ama Enugu wa IFM
 
hAA Haa pole sn miss chaga kama kweli ndo wewe. Usjali nipm namba yako nikrushie japo kijivocha cha kukusababishia usumbufu

yani naomba unipe na hela ya nauli mwaka mzima kuniacha natoa macho pale kama mjinga .... uliamua kunidhalilisha mkuuu sitakusamehe kabisa mpaka unipe hela
 
nilimkimbia dem mmoja mliman city..... tulichat fb, kukutana nae ni dwarf gunia la mkaa ni refu na unene komba kapten ni mwembamba....
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom