Mtoto kuanza kuota meno ya juu, kibailojia na kimila inaashiria nini?

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,504
12,829
Habari za leo ndugu zangu wapendwa? Ni matumaini kuwa mpo safi kabisa. nimekuja hapa kwenye hili jukwaa nikiwa nina shida moja inayonitatiza.

Jana nilikuwa nampa chakula mwanangu (ana miezi 7 na siku kadhaa), sasa wakati nampa nikaona kuwa ameanza kuota meno ya juu badala ya meno ya chini kama ilivyokuwa kawaida.

Hali hii nilishangaa na hata baadae nikamwambia mke wangu ambae nae pia alishangaa na hakuwa na majibu. Sasa nimeleta hii mada hapa kwenu mnipe ushauri kama kutakuwa na shida yeyote katika maendeleo na ukuaji wa mwanangu mpendwa.

Nitashukuru sana kwa michango yenu.

NB: Kama hautakuwa na mchango wa maana tafadhali pita wima,

this is serious case.

===
JF doctors na wazee wa mila naombeni msaada kwa hili tafadhali,

Kwa kawaida mtoto hutakiwa kuanza kuota meno ya chini then meno ya juu hufutia!

Lakini kuna wale watoto ambao huanza kuota meno ya juu, Kwa mila za kiafrika hawa watoto wanaogopwa sana.

Miaka ya nyuma waliishia kutupwa maporini, na uchunguzi unaonesha watawala yaani machifu waliogopa kwamba watoto hao wakikua watawapindua kwani wana vipaji vya ajabu.

Kwenye makabila mengine hapa Tanzania watoto hawa hawaoi kisa atafiwa na wake wote.

Na mila nyingine nyingi tu!

Sasa leo nimeamua kukata mzizi wa fitina kuomba ushauri wa kitaalamu, nini kinatokea hapa!
 
Msaada wenu tafadhali, mwanangu ameanza kuota meno ya juu badala ya chini, mama yake amekuwa mtu wa wasiwasi kila mara, majirani pia wamekuwa wanamtisha bila kumwambia sababu nini?

Nijuzeni please.
 
Habari za leo ndugu zangu wapendwa? Ni matumaini kuwa mpo safi kabisa. nimekuja hapa kwenye hili jukwaa nikiwa nina shida moja inayonitatiza.
jana nilikuwa nampa chakula mwanangu (ana miezi 7 na siku kadhaa), sasa wakati nampa nikaona kuwa ameanza kuota meno ya juu badala ya meno ya chini kama ilivyokuwa kawaida.

Hali hii nilishangaa na hata baadae nikamwambia mke wangu ambae nae pia alishangaa na hakuwa na majibu. Sasa nimeleta hii mada hapa kwenu mnipe ushauri kama kutakuwa na shida yeyote katika maendeleo na ukuaji wa mwanangu mpendwa. Nitashukuru sana kwa michango yenu.

NB: Kama hautakuwa na mchango wa maana tafadhali pita wima,

this is serious case.
Cc; MziziMkavu, Mtambuzi, faizaFoxy na wengineo
 
jamani mbona hamji kuchangia hii kitu inaniua mwenzenu? Nimerudi kutoka kazini nimekuta mke wangu hata hajala kisa hana mood ila as far as I know amechanganyikiwa na hii ishu
 
Ndugu yangu ukiona kimya ujue wanaofahamu hizi habari hawajapita hapa bado. Endelea kuvuta subira, wenye majibu ya kueleweka watajitokeza tu.
 
It happens.. Nothing to worry about.. Ni uumbaji tu. Usianze kuwa na mawazo negative
 
Ahh nimekusudia kukwambia haina shida ni maimbile tu me watoto wa dada zangu wawili wapo tofauti waliota meno ya juu kwanza na wapo kawaida tu wakubwa ss hv, kwa kule kwetu wanasema mtoto akiota.meno ya juu mwanzo anakua mtukutu lkn me naona hamna lolote vitu vya kawaida tu.ila kama una was was muone dokta wa watoto atakusaidia zaidi.
 
mkuu ahsante sana kwa mchango wako, maana pia katikahoja ambazo watu wamekuwa wakimtisha wife kuwa mtoto atakuwa mtundu sana, hasikii na muongeaji kuliko kawaida. Ila Ahsante kama nothing of a sort happens. unajua tena hofu ya first born inavyokuwa...
 
mi wangu ana miezi tisa anatembea hana jino ht moja najiskiaga vbaya wanamcheka asa sielewi mtoto anatembea halafu hana jino
 
jamani mbona hamji kuchangia hii kitu inaniua mwenzenu? Nimerudi kutoka kazini nimekuta mke wangu hata hajala kisa hana mood ila as far as I know amechanganyikiwa na hii ishu

Inaweza kuwa ni kwa sababu tayari umechagua watu wako watatu ambao ungependa wachangie kwenye hiyo thread yako. Hata hivyo, bila kumumunya maneno, kitendo hicho kwa baadhi ya makabila ya Kanda ya Ziwa ni Taboo. Hata hivyo, ucjali kama hautokei eneo hilo, haina shida, kama unatokea eneo hilo usiwaeleze home, keep it closed within you family doors, for more info, pm me.
 
Wanasema siyo vizuri.

Na wakati mwingine wanasema inawezekana siyo meno bali kuna meno yanaitwa ya nailon/plastic.

Ukienda kwa Dr. wa watoto, miaka ile ya zamani walikuwa wanayapaka dawa fulani halafu yanapotea.

Ngoja nikuitie Dr. asakuta same aseme kitaalam.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom