Mtoto Aliyejifungua Mtoto

Mtoto Aliyejifungua Mtoto

MTOTO WA MIAKA 11 AJIFUNGUA HUKO PARAGUAY
150813214449_paraguay_child_rape_512x288_bbc_nocredit.jpg

150813214449_paraguay_child_rape_512x288_bbc_nocredit.jpg

Binti wa miaka kumi na mmoja nchini Paraguay aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wa kike baada ya mamlaka nchini humo kumzuia asitoe ujauzito aliokua nao.
Madaktari katika mji mkuu wa Asuncion wamesema binti huyo na mtoto wake aliyejifungua kwa njia ya upasuaji wanaendelea vizuri.Tukio hilo limesababisha utata mkubwa nchini Paraguay na katika mitandao ya kijamii, Paraguay ni taifa linaloamini zaidi katika Ukatoliki ambapo mwanamke anaruhusiwa kutoa mimba pale tu afya yake inapokuwa hatarini.Binti huyo alibakwa alipokua na umri wa miaka kumi pekee na Baba yake wa kambo mwenye miaka arobaini na miwili yupo rumande akisubiria kutajwa kwa kesi yake wakati huo huo baba huyo amekanusha kuhusika katika tukio hilo.
Source:BBC

Vijimambo
 
I hope aliyenzalisha ameshakuwa "castrated like a hog" na hata kuwa uraiani for the rest of his life
 
Duuuu! Ni hatari aisee! Sasa hii chukua kama ww ndio mzazi wa huyo mtt aliye aliyejifungua mtt, utafanyaje? Mambo mengine yanaumiza jamani!
 
hahahahahaa ss wanaume bhna akili zetu twazijua wenyewe
 
Hivi mwanamke huvunja ungo akiwa na umri gani?
saa nyingine inabidi tu tuachane na wanasayansi uchwara.
Na mimi huwa najiuliza mbona viumbe vingine vikivunja ungo tu vinaanza kuzaa? Kwa nini iwe tofauti kwa binadamu?
 
Dunia nzuri sana ila wapitaji ndani yake tuna mambo mengi sana
 
Mbona mabibi zetu walijifungua wakiwa na miaka hiyo hiyo
Sijui kwa jamii za wapi, ila nyingi zao hawakuwa wakijifungua ktk umri na maumbo madogo kama hayo. Mfano kwa jamii zenye unyago, waliachwa ndani hata kwa miaka 6 ili wakue ndo waolewe, hapo na mchumba alishapatikana. Mafundisho ya bibi wangu hayo.
 
Maoni yangu:Tunaishi na haya mambo mitaani kwetu, usiulize imetokea wapi.
Kama alijifungua salama, Mungu awabariki mama na mtoto.
 
Wadau angalieni umbo la huyo mwenye mimba na aliyemshika mtoto vina ufanano?
Pua na midomo yao ina ufanano? Labda macho yangu .
 
Back
Top Bottom