Mtoto Akataa shule; Bora aende jela

Hilo nalo wazo maana elimu ya sasa matatizo tu
 
Huko Veta anaenda kusomea nini ambacho kwenye mfumo wa elimu ya kawaida hakipo?
 
Dunia imebadilika Sana.Diamond angesoma asingemiliki rose royce.
Samatta angesoma asingemiliki ghorofa.
Bakresa angesoma asingekuwa milionea
Ila kumbuka na upande wa pili.
MO asingesoma asingemiliki simba kijanja.
Mello asingesoma asingeanzisha JF.
Japo dogo yupo sahihi binafsi nilichukua maamzi kama hayo
 
Dogo sijui wamemvuruga nini!

Amekomaa na msimamo wake "Sisomi"
 
Mess na Ronaldo wanalipwa na waliosoma ukumbuke. Wanacheza mpira kwenye viwanja vilivyojengwa na mainjinia wanalipwaa matangazo ya biashara ya kampuni zinazotumia wasomi kuzalisha bidhaa ata hayo matangazo yameandaliwa na wasomi.
 
Dogo kaamua akapige singeli inalipa kuliko shule.
Elimu sahihi ni form four kisha ingia mtaani upate elimu ya maisha.
Kusoma zaidi ni kujitakia umasikini
Kweli aisee elimu ya sasa ni kama unaweka odds
Kusoma 1.4 kutosoma 2.8
Kazi kwa mbetiji
 
Ila hapo napo uko sawa ila labda wamemzingua shuleni ndo maana kaamua kukomaa asisome
 
Hii inaitwa mind your own business...

saikolojia yake ndiyo ishagoma kuona umuhimu wa shule...
 
Kwenye hiyo video dogo yupo serious kabisa.
Ila swala la kukataa shule athari zake huja Kulingana na bahati ya mtu Kwa mfano mwingine anaweza kataa shule na akatoboa kimaisha ila mwingine anaweza kataa hivyo hivyo na maisha yanamkataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…