Mtoe out mkeo usiku wa leo

Mtoe out mkeo usiku wa leo

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,933
Hii inawahusu wanaume waliooa ila hawapendi kuwatoa out wake zao.

Mtoe out mkeo, ni mwanamke mzuri ambaye alihatarisha maisha yake ili kukupatia watoto.

Anakuhudumia chakula kitamu kila siku.

Anakuweka safi na nadhifu. Anakupa mwili wake kwa raha zako.

Anasimama nawe wakati wengine wote wanapokuacha.

Anatumia mapato yake na wewe na watoto wako.

Anastahili umakini wako.

Unaweza kumudu kumpeleka out kwa chakula kizuri usiku wa leo. Cheza naye music. Shika mikono yake yenye joto na mkumbatie kiuno chake hadharani!

Mapenzi sio jambo la siri. Upendo lazima udhihirishwe. Upendo huenda zaidi ya hisia kwa vitendo. Upendo ni kitenzi amilifu. Mapenzi sio matamanio. Upendo hubeba vitu vinne ambavyo ni..
Mawazo
Hisia
Neno
Tendo.

Wanaume wenye busara huwatendea wake zao kama malkia. Bali walio wajinga wanaendelea kulalamika kuhusu mwanamke waliyemchagua. Wanaume wenye busara wanajua ukitoa mapenzi yanarudi kwako.

Anayempenda mke wake anajipenda mwenyewe (Efe 5:28).

Barikiwa
 
Hayo mambo kafanyeni chumbani
Ikiwa kuna mwanaume ana ujasiri wa kushika hadharani kiuno cha kahaba halafu hawezi kushika hadharani kiuno cha mkewe utamuweka kundi gani mwanaume wa hivyo?
 
Mmh mama Sasha sasa nimwambie tutoke anaanza kunambia tukitoka tukajiachie hadi tukirudi tushatumia sio chini ya laki, hiyo hela si bora tuongeze ongeze tukaweke tofali hata 200 kule site, anachukua 5000 anaenda kuweka movie kwa flash ndo wikiendi imeisha hivyo, mamamkwe nafikiri alimpiga bamkwe somehow
 
Matumizi lazima yaende na kipato chako unaweza tumia hata buku kumi tu kwa kumtoa out hadi eneo lenye gharama nafuu.
 
Matumizi lazima yaende na kipato chako unaweza tumia hata buku kumi tu kwa kumtoa out hadi eneo lenye gharama nafuu.
Yaani mimi nishapiga hesabu namwambia haya j2 mapema beba sasha tukazurure sasa ataanza kuuliza tunaenda wapi, anaanza kupiga hesabu yeye sasa, hii tabia yake sijawahi kuiona na mwanamke yeyoye niliewah kukutana nae ukiachana yeye
 
Usilalamike kwa mwanamke uliyemchagua mwenyewe, tumia busara kama mwanaume mwenye akili timamu kumuweka sawa mama Sasha.
 
Back
Top Bottom