Mtikila kufungua kesi ya kudai Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila kufungua kesi ya kudai Tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]


  Na Ramadhani Siwayombe, Arusha

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anakusudia kufungua kesi mpya katika Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika iliyoko Arusha, kudai serikali ya Tanganyika.


  Mchungaji Mtikila aliyasema hayo jana mjini hapa, mara baada ya kuahirishwa kwa kesi aliyoifungua katika mahakama hiyo kudai uwepo wa mgombea binafsi.

  Mtikila alisema kuwa kutokana na imani kubwa aliyonayo kwa mahakama hiyo, ana imani haki aliyokua akiitafuta kwa muda mrefu sasa iko mbioni kupatikana.


  Alifafanua kuwa katika kufungua kesi hiyo ya kudai Tanganyika, kuna wanasheria kutoka Nigeria wako tayari kuja kusimamia katika kesi hiyo ambayo alidai itakuwa ni ukombozi kwa Watanganyika wote.


  Aidha alisema kuwa wakati yeye anakusudia kufungua kesi hiyo tayari ana taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Wazanzibari wanakusudia kufungua kesi katika mahakama hiyo kupinga muungano.


  Awali katika mahakama hiyo, kesi iliyoanza kusikilizwa juzi na mahakama hiyo juu ya hoja ya mgombea binafsi iliyofunguliwa na Mtikila pamoja na kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu mara baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili iliahishwa.


  Kesi hiyo inayosikilizwa na majaji tisa kati ya 10 wa mahakama hiyo iliahirishwa hadi baada ya siku 90 ambapo itakuja kutolewa hukumu kutokana na pande zote mbili kukamilisha ushahidi wao.


  Katika kuwasilisha maelezo ya mwisho na kujibu maswali yaliyotolewa na majaji wa mahakama hiyo, upande wa Mtikila uliiomba mahakama hiyo itamke kuwa na haki kuwepo na mgombea binafsi katika chaguzi zote za kisiasa hapa nchini.


  Aidha kupitia kwa wanasheria James Jesse, Clement Mashamba, Donald Deye na Profesa Lajovi waliiomba mahakama hiyo pia iiamuru serikali ya Tanzania kulipa gharama zote za kesi hiyo.


  Jaji Elsien Thompson alimuuliza Mtikila ni kwa nini anataka kuwepo kwa mgombea binafsi wakati yeye tayari ana chama chake kinachomuwezesha kupata fursa ya kugombea.


  Kupitia mawakili wake, Mtikila alijibu kuwa kutokana na kuwepo na taratibu ngumu za uidhinishwaji wa vyama kuruhusiwa kusimamisha wagombea, imepelekea mteja wao kushindwa kupata haki hiyo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa tumefika Mtikila kaingia kwenye issue ya Muungano, alahaula... sasa tuko kwenye RED LIGHT DANGER...

  Tutasikiliza Mahakama kuu itasemaje sababu pia Wazanzibari wamepekeka Malalamiko yao Mahakama kuu
   
 3. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Akitaka washika mabango wa kwanza mimi.
   
 4. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mchungaji Mtikila aliona mbali sana kuhusu hili swala tokea siku nyingi, ila sema serikali ya ccm na akili zao za kitahira ndio ilikuwa kikwazo. Mungu aendelee kuilaani ccm...
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mtikila ameishiwa. Serikali ya Tanganyika ndiyo nini? Kwani Kikwete ni rais wa wapi?
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu Jasusi heshima yako. Madai ya Tanganyika yanakuja kutokana na muungano kuwa wa kiuni, haueleweki... Tunaambiwa muungano haujadiliki kwenye katiba mpya 'just' kuuboresha. Hata hivyo mbona hati/mkataba wa muungano hauonekani kama ilivyo katiba? Mkuu ishu ya muungano ina makunyanzi mengi, ndio maana inapelekea madai ya Tanganyika au Zanzibar...
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Mtikila anaelekea kuwehuka.
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,708
  Trophy Points: 280
  Hujui usemalo...
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa. Kikwete si Mtanganyika.
   
 10. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,708
  Trophy Points: 280
  Mtikila hadai uwepo wa Kikwete... Anadai uwepo wa Tanganyika, kuwepo au kutokuwepo kwa Kikwete madarakani haku uhusiano na madai ya uwepo wa Tanganyika. Selikari ya Zanzibar ipo, lakini wanaidai iwepo kikamilifu...sembuse sisi tuliopoteza kabisa. ETI KUNA MAMBO YA MUUNGANO NA YASIYO YA MUUNGANO... Kwani hayo yasiyo ya MUUNGANO YANASHUGHURIKIWA NA SERIKALI GANI HUKU BARA?
   
 11. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Najivunia kuwa Mtanganyika na ninahitaji saana serikali yangu ya Tanganyika let zanzibar go tuachane kwa amani na tusiachane kwa kupigana vijembe maana najua madhara yake ni makubwa.

  Sijui watanganyika wenzangu wanaona fadia gani na huu muungano? na hata wanzanzibar wanalalamika sasa which is which kila mtu ajieungue jamani viongozi wa serikali huwa hawamo humu jamvini kweli?? au wanamaslahi yao binafsi?
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tanganyika ipo. Ndani ya Tanzania. Ninaposafiri kutoka Arusha hadi Mwanza nimo ndani ya Tanganyika. Kikwete ni rais wetu na amiri mkuu wa jeshi. Zanzibar wanaye amiri mkuu wa jeshi? Hakuna tulichopoteza sisi Watanganyika ni kujidanganya tu. Hivi umewahi kujiuliza tukiwa na serikali tatu ni nani atakayekuwa amiri mkuu wa majeshi? Ni rais wa Tanganyika au rais wa serikali ya tatu?
   
 13. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Huyu ni kimanda sema yupo kimpango na harakati zake za mahakamani mzee anawachukia sana makabachori na muungano, namuunga mkono.
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  we siyo mzima!
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kabisa. Na wala sihitaji dawa ya mtu yeyote. Tanganyika imekuwepo na itaendelea kuwepo. Msichokifahamu ni kwamba Tanganyika ndiyo imeshika usukani wa muungano. Bila usukani huo Zanzibar mambo yatasarika.
   
Loading...