Mchungaji Christopher Mtikila amewasifu Dr Slaa na Prof Ibrahim Lipumba kwa kusikiliza na kutii sauti ya Mungu kupitia dhamira zao.
Amedai wagombea wote wawili wa CCM na CHADEMA wana mapungufu lakini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atajua wazi mapungufu yao yanazidiana kwa kiasi kilicho dhahiri mno!
Na kama kuna mtu haoni hilo basi anatakiwa kupimwa akili.
Amedai wagombea wote wawili wa CCM na CHADEMA wana mapungufu lakini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atajua wazi mapungufu yao yanazidiana kwa kiasi kilicho dhahiri mno!
Na kama kuna mtu haoni hilo basi anatakiwa kupimwa akili.
Mch machachari Mch Christopeher Mtikila akiwa katika studio star TV leo asubuhi katika kipidi cha tuongee amesema kwamba Jaji Lubuva ni mkwewe Lowasa. Alizungumza hiyo habari kufuatia kitendo cha kampeni alizozifanya mgombea Urais kuiptia Ukawa alipokua ziarani Tabora pale aliposema kuwa hii ni zamu ya warutheri kuongoza nchi. Pamoja na hayo mambo mengine aliyaongea ni juu ya kauli za viongozi waandamizi wa UKAWA ambazo zinatoka katika kauli ndimi moja lakini zinatofautiana.
Mfano: Kauli ya Mgombea Urais kupitia Ukawa alipokuiwa CCM alisema '' Rais kikwete ni Visionary Leader ana uwezo wa kuona mbali'' na alipotoka CCM akiwa ukawa akasema "Rafiki yangu Jakaya Mrisho Kikwete, kahuaribu uchumi wa nchi" Pia Mhe Fredrick Sumaye'' Enadpo CCM itampitisha Lowasa kugombea Urais mimi nitahama chama" na alipokuwa ameama CCM akasema" Lowasa anastahili Urais yeye ndiye Jemedari wetu" Kauli ya Tundu Lissu "CCM wamempatia Fisadi Lowasa Fomu ya ugombea Urais, Ni hatari''….leo amegeuka kua mpiga debe mkuu….
Kauli ya Mnyika " Nina Ushahidi wa kutosha kuhusina na ufisadi na wizi wa Lowasa na Rostam… Mwisho akasema ata mchungaji mwenzake Mh Peter Msigwa anayemuunga mkono Lowasa akapimwe akili leo amegeuka kuwa mpiga Debe mkuu… Akasema kauli tofauti katika vinywa hivyo haviwezi kuongoza fikra za watanzania…..hizo ni mbinu za kuwania madaraka wakipata madaraka wanaanza kuwa na lugha za utetezi….
Na alipoulizwa kuwa inawezekana amenunuliwa na CCM kutokana na kauli yake ya kusema mgombea wa CCM John Pombe Magufuri ana nafuu kuliko Mgombea wa UKAWA…akajibu yeye anaendelea kusisitiza kuwa hawa wagombea wote wana matatizo ya kiafya lakini mmoja ana nafuu au matatizo yake mpaka uyafanyie research huyu mwingine hata ukiwa mjinga kiasia gani unamuana kabisa ubongo umepoteza mawsiliano na mwili. Hivyo Ikulu siyo Hospital
Akasisitiza kuwa CCM imemuweka ndani mara kadhaa zaidi ya mara 40 hawezi kuwamsemaji wao hata kidogo…..