Mtihani wa kidato cha pili warudishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani wa kidato cha pili warudishwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mwanajamii, Jan 11, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Naibu waziri wa elimu Philipo Mulugo ametangaza kuwa serikali imerudisha mtihani wa kidato cha pili kwa lengo la kuboresha kiwango cha ubora wa elimu ya Tanzania.amesema kuwa mwanafunzi ambaye hatafaulu mtihani huo wa kidato cha pili hataruhusiwa kufanya mtihani wa kidato cha Nne.
  Source.Tbc habari saa 10 alasiri
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Amesema utekelezaji wa zoezi hilo unaanza mwaka huu 2012
   
 3. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Haya matamko ya kilevi tu, wawafundishe watoto wetu, wawape waalimu bora na elimu bora yenye viwango ndio wawatishe. Shule yenye mwalimu mmoja unaishindanisha na shule zenye waalimu wenye sifa na waalimu wakutosha sio kuprone watoto wa masikini huku?

  Ndio tunataka elimu bora tena inayoendana na dunia ya leo yenye mitaala yenye tija na na mitihani isiyosimamiwa na wizara ya elimu. mitihani hii itungwe kutokana na vitabu, na kama watoto wakiwa wanashindwa kufaulu tuangalie tatizo ni nini ni watoto, vitendea kazi , waalimu au mazingira duni au vyote.
   
 4. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Kwani ilikuwa imeenda wapi, si kila mwaka huwa inafanyika.
   
 5. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye red mkuu, ina maana huyo atakayefeli ataendelea na kidato cha tatu lakini hatofanya mtihani wa kidato cha nne bila kufaulu ule wa kidato cha pili? Mie sijaelewa!
   
 6. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kila nayeingina anakuja na sera zake!
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Mtihani wa form 2 ulikuwa indication nzuri kabisa ya kile mtoto atakachovuna akifika form 4. Kurudia form two ni kuchezea resources, mtihani unapaswa uwepo lakini uwe kama kipimo tu. Ili mzazi ajue kama form four atanunua mtihani ama atafanyaje. Wazazi wa siku hizi are pathetic for real! Hawataki majukumu ya kulea watoto wao!
   
 8. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  shukran Mkuu, amesema watarudishwa kwa wastani wa ngapi?
   
 9. GIUSEPPE

  GIUSEPPE JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 4,498
  Likes Received: 4,509
  Trophy Points: 280
  utumbo mwingine wa elimu za bongo,

  hivi hatuna sera ya elimu ya taifa? mpaka kila waziri anayechukuwa wizara aje na ufundi wake? sasa na hizo shule za kata zenye form one mpaka form four na mwalimu mmoja zitakuwaje?
  nadhani hapa lengo si kutoa elimu bora ila ni kuongeza kiwango cha wasiosoma nchini, jambo la muhimu lingekuwa ni kuongeza waalimu, kisha kuwalipa mishahara mizuri, shule kuwa na vifaa vyote muhimu vya kufundishia. hapangekuwa hata na haja ya kuwa na mtihani wa darasa la saba. mtu unapiga mpaka darasa la 12. kisha baada ya hapo tunafikiria tukupeleke wapi, ufundi au a level.
   
 10. M

  Mussa Mussa Senior Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu wasomaji naamini wote ni mashahidi ya kwamba selikali ya Mh. Kikwete haiko makini hasa kwenye maamuzi ya msingi likiwepo swala la kuondolewa mitihani ya kidato cha pili (Yaani mtihani ulikuwepo lakini mwanafunzi alikuwa anaendelea hata kama amefeli).

  Hili suala nakumbuka wabunge wengi wa upinzani walilipinga lakini kama kawaida ya CCM kutumia uwingi wao na kupitisha mambo mbalimbali yasiyo na tija kwa taifa likiwemo hili walilipitisha. Uamuzi huu utakuwa umekuja baada ya matokea ya kidato cha nne kuvunja rekodi ya kufeli baada ya kuondolewa mitihani hiyo.

  Utakumbuka kwamba waziri wa elimu alitangaza matokea ya darasa la saba hivi karibuni na kudai kuwa ufaulu umeongezeka hasa kwa somo la hisabati, lakini mtindo uliotumika ulikuwa ni danganya toto kwa kuwa maswali yote ya hisabati yalikuwa ni ya kuchagua yaani multiple choice. Hii ni wazi kwamba hata asiyejua hesabu lakini anauwezo wa kusoma na kuchagua hawezi kupata zero kwa kuwa atakisia na kupata. Ndugu zangu msishangae mwakani mkiona utaratibu huu uliwa umebadilika kwa sababu wanafunzi hao wanaodai wamefaulu vizuri yatawakuta huko wanakoenda yaani sekondari.

  NINI KIFANYIKE
  Wabunge hasa wa CCM waache kufanya mchezo katika mijadala mhimu wanapokuwa bungeni kwani wapigakura wao tunaona upuuzi wanaofanya la sivyo kura zitaamua 2015. Watanzania wenzangu tukifanya mchezo na hawa CCM itakula kwetu na hasa kwa watoto wetu(Kizazi kijacho) kwani selikali hii itawaachia mashimo ya dhahabu wanetu kisa wao wengi bungeni wanauwezo wa kufanya wanachotaka.

  Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki Afrika.
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  nami nashangaa...........mbona hii mitihani ipo!!.....labda kuna kitu tofauti huyu Waziri ameongelea........
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida zima moto yao na maamuzi yasiyo na msimamo
  mara ufutwe mara urudishwe sijui tuamini lipi kwa hawa watawala wetu
   
 13. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  hili alilisema mwaka jana akiwa jimboni kwake, tulidhani utekelezaji wake unaanza na form2 wa 2011, kumbe 2012...!

  kwa kweli mtihani huu ni muhimu sana! wanafunzi siku hizi hawasomi coz hawaoni athari za kushindwa kupata wastani wa kwenda form 3... anayepata avarege ya 08 na anayepata avarage ya 75 wote wanakwenda form 3
   
 14. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wastani wa ufaulu ni 30.Pia wazazi au walezi watalazimika kuchangia kiasi cha Tsh. 10,000/= na kwa mtihani wa kidato cha nne mchango utakuwa Tsh 35,000/=Mchango wa mtihani wa vidato vya nne na sita uliondolewa na serikali ikajigamba kwamba ingegharimia, yako wapi sasa au ilikuwa kampeni ili 'chama chetu' kishinde?
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kulingana na maelezo ya huyo mheshimiwa inaonekana wataendelea na kidato cha tatu hata kama wamefeli..
   
Loading...