Mtetezi wa wasafirishaji amepandisha nauli, mtetezi wa wasafiri mbona kimya?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,184
11,607
Kupanda kwa nauli za daladala na mabasi ya mikoani kungeendana na maboresho ya huduma husika.

Mathalani miundombinu ya stendi, mfano sehemu za kupumzika abiria, muda wa kuondoka mwanzo wa safari hadi mwisho wa safari, ubora wa vyombo vya usafiri na unadhifu wa watoa huduma nakadhalika na kadhalika.

Mamlaka zenye dhamana ya usafirishaji, kuweni wabunifu zaidi ya kubuni kupandisha nauli tu...

Haya sasa mwende mkalitizame na hili.

Gharama za usafiri ziendane na ubora wa huduma ya usafiri. Abiria wanateseka mabasi machache, huduma mbovu na huku gharama zikiwa juu.

Natoa Rai kwa Msemaji wa abiria kutoa neno kwenye jambo hili.

Asanti.
 
Kwani bei ya mafuta kwa pipa huko duniani ikoje?
Sababu za kupanda kwa nauli zimetajwa?
 
Achana na vyombo vya moto jitahidi kutembea kwa ajili ya afya yako pale unapoweza kufika, ukifanya haya utapunguza nusu ya gharama za nauli.
 
Back
Top Bottom