MTEMI wa Tanzania (M.T) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MTEMI wa Tanzania (M.T)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Apr 6, 2012.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nimefikiria namna ya kurudisha moyo wa utaifa ndani ya jamii yetu na kuja na wazo dogo kuwa tuweke heshima maalum kwa mwaka kwa watu ambao wataonekana kuwa wamefanya jambo la maana sana kwa nchi hii na wapewe tuzo ninayopendekeza iitwe MTEMI wa Tanzania au kwa kifupi (M.T) na iwe ni tuzo yenye heshima sana ambayo mtu awe anajivunia kuitumia kwa kiswahili au kiingereza, kwa mfano iwapo Kichuguu akipewa heshima hiyo basi aitwe Mtemi Kichuguu (M.T.) au Chief Kichuguu (M.T).

  JamiiForums inaweza kuratibu utaratibu wa aina hiyo tukawa tuna-raise funds za kuendesha mchakato wa kupokea maoni na kuchambua wasifu wa wanaopendekezwa hadi kutayarisha hafla ya kuwatunuku washindi. Mshindi anaweza kuwa mfanya biashara, mkulima, msanii, mtumishi wa serikali, mwanablogu, mwandishi wa habari, mwanamichezo, mwandishi wa vitabu, mwalimu, mtangazaji, hakimu, mwanasheria, mhandisi, mganga, mcheza mazingaombwe, mwanasiasa, au mwanataaluma yeyote mradi tu ni Mtanzania.

  Nadhani itatia raha sana kuitwa Chief Kichuguu (M.T) kuliko kuitwa Mheshimiwa Kichuguu (Mb) au Dk Kichuguu (PWU).
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,524
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Fafanua zaidi nini itakufa faida ya hizo tuzo zako na mtu akiisha kuipata itakuwa na tofauti gani na mituzo mingine lukuki iliyojaa mitaani.
  Pata kufikiri tuzo alizonazo Mkweree, zipo ngapi na zimekuletea heshima gani wewe kama mtanzania, na zimemletea heshima gani yeye kama Mkweree.
  So, jipange tena uje tena hapa na faida ya hizo tuzo zako
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Poa kidogo; post yako ni ya mkato sana na nadhani hukufikria wazo hili kwa kina vya kutosha. Ni sawa kabisa na yule anayesema kuwa kwa vile mgombea fulani hajaninunulia pilau basi sintampa kura yangu leo, badala yake nitampa huyu aliyenipa pilau kwa kuwa amenipa shibe leo.

  Nimefikia jambo hili kwa kina na ninaona faida kubwa sana huko mbeleni kuliko leo hii mara moja.
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee Kichuguu hapo kwenye red huo ni utani mbaya sana ... LOL!

  Itabidi niwasiliane na TCU nimuulize Prof. Mayunga Nkunya kama ameishawahi kuona sifiketi yako ya PWU na ame-certify kwamba unastahili kuitwa Dokta Kichuguu (PhD - for political ujiko purpose, PWU).
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  (1) Lakini si ni kweli kuwa tuna viongozi wengi wa aina ya Dkt. Kichuguu (PWU)?

  (2) heshima ya MT itakuwa ni pekee isiyopatikana popole pale kirahisi ila kwa kui-earn kwa watanzania; ni karibu sawa na heshima ya Sir ambayo haipatikni kwingineko kokote kule ila kutoka kwa malkia wa waingereza tu, na ni heshima ya kiingereza tu. Nina imani kuwa heshima yenye identity ya kitanzania tu itakuwa na thamani kubwa sana machoni mwa watanzaniaq huko mbeleni.
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee Kichuguu wagombea Ubunge wa 2015 kupitia chama fulani, utakuta wengi ni ma-"Dokta", sasa hivi wanasoma PWU kwa njia ya mtandao, very soon wataipua PhD zao na kuziingiza sokoni tayari kwa kusaka ajira ya siasa kwa kuwalaghai wapiga kura kwamba nao ni wasomi waliobobea kumbe ni weupe kuliko hata wasomi waliomaliza Form 7.

  Hiyo M.T. ikishatambulika rasmi utaona jinsi wanavyokimbilia kuisaka kwa udi na uvumba na wako tayari kuinunua kwa bei yoyote ile, kasoro uhai wao wenyewe.

  Hujaona Ridhiwan alipewa uchifu kule unyakyusani, kwa kipi hasa alichokifanya mpaka awe chifu wa wanyakyusa?

  Lowassa ni Laigwanani Mkuu wa ukanda wa huko kwao, ajabu ni kwamba Lowassa ni mmeru kwa asili. Ukiuliza waliompa huo u-Laigwanani walitumia vigezo gani kumpa huo ukubwa huwezi kupata jibu la kueleweka? Maana kwa age ya kwake, ni rika la "makaa" na juu ya "makaa" kuna generations (rika) mbili ambazo bado ziko hai. Ina maana walio juu ya generations hizo mbili hawafai wote?
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Chifu wa Tanzania inatakiwa iwe ni hadhi pekee isiyotolewa kwa pesa wala ushabiki wa kisiasa. Nimepata bahati ya kufanya kazi kwenye panels mbalimbali za kimataifa katika kuchambua sifa za watu ili kuwapa tuzo husika bila kutumia hongo wala external pressure. Tunaweza kuwa na panel za namna hiyo ambayo itaogopwa na kuheshimiwa; kinachotakiwa ni commitment tu.

  hebu ona ambavyo Nobel prize inavyoheshimiwa leo!! Ni nini kitakachozuia MT isiheshimiwa kwa kiwango hicho iwapo tutaamua?
   
Loading...