donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,071
- 21,541
Mkuu umeelezea vizuri. By the way, Mimi ni mtwamvinaSijawahi kuona Uzi mbaya Kama huu,nimesoma kwa uchungu mpaka machozi yamenitoka.
Hatujawahi kumsema vibaya milambo na Wala mkwawa hakufanya kwa sifa kuwa anamzidi milambo. Sijajua popote Kama waliwahi kufundisha kuwa mkwawa Ni zaidi ya milambo Ila huwa wanafundisha mema yake tuu. Naona umeamua tuu kumtukana MTWA MKWAVINYIKA Mtu mwenye ardhi kubwa! Kwanza mkwawa ana muheshimu Sana Mirambo na walioleana watoto
Kwa heshima mbwa wewe ilipaswa hata kufuta thread yako.
Ngoja nikupe machache kunihusu MTWA MKWAVINYIKA ambaye alifanya makubwa kabla ya kufikisha hata miaka 50
-Baada ya kifo Cha Mtwa Munyigumba uhehe iliyokuwa ndogo Sana iligawanyika katika pande mbili, upande mmoja uliangushwa na himaya hii kuwa mikononi mwa jitu, Jitu haswa! Mpana wa mwili, nguvu, uchawi na mwerevu shujaa wa Vita Tena anatajwa kuwa Askari mwenye mbio zaidi Duniani!
Ntakupa historia fupi tuh kuwa mwishoni mkwawa aliunganisha vikosi na kumuangusha huyu mwamba katika Vita kubwa mno uhehe!
Namkubali Mtwa Milambo Ila Hakuishi wakati wa mashambulizi makali nikimaanisha baada ya Berlin 1884--- angepigwa tuu Kama mwamba wa wakati wote Samoli Toure!
- Mtwa mkwawa alikuwa na kiwanda Cha Magobole sio Mirambo pekee Kama ulivyoaminishwa. Alikuwa na kiwanda Cha uhunzi Cha kutengeneza Vifaa mbalimbali Kama vya kilimo
- Mkwawa alitengeneza mfumo wa biashara uliyoiingizia uhehe pesa mingi
- Mkwawa alitawala ardhi kubwa ya Iringa, kuanzia kitonga milimani mpaka mgololo karibu na makambako na kote alizurula saa kwa miguu. Ila hakuridhika alipiga himaya ya wabena, alimpiga msangu na kuweka mpaka wake karibu na mnyakyusa huku na safari ilikuwa inaendelea.
- Mtwa mkwawa alishuhudia mashambulio yasiyo pimika kutoka kwa mzungu na vipigo vyote hivyo aliweza kuwashinda, Kuna kipigo Cha Tosa maganga, Kuna kumbukumbu za kikatili eneo la Kitanzini... Wakati furani Gavana wa kijerumani aliniuliza huyu Mkwawa Ni Mtu, Mto au Kisiki?
- Best of all ni kuua Askari 3000 wa kijerumani wakiongozwa na kanali wa Vita mkongwe von Zelewisky pamoja na majenerali wengine wa Vita wakati huo.
- Kifo Cha Mkwawa kilitokana na kuchoka kwa Jeshi kwani amekuwa mtu wa Vita nyakati zote za utawala wake, kikubwa zaidi alisalitiwa na sub chiefs walio toa Siri kwa ahadi ya kupewa madaraka makubwa!
- Mtwa mkwawa aliulika akiwa katika Hali ya ugonjwa mno! Njaa isiyo kipimo akibakiwa na wadzungwa waaminifu watatu vijana wadogo
Kikubwa zaidi Je unaweza ukaamini Mtwa Mkwawa amefanya yote hayo kwa kipindi Cha si zaidi ya miaka 20 tuuu? Kuunganisha kabila, kulipa nguvu na kupambana na maadui jirani na wazungu ndani ya miaka 20 unaweza kuamini??
Nimeelekeza machache tuu kumuhusu Mkwawa ulivyoamua kumdogolesha imeniuma Sana, sijui mtu huyu angeishi nyakati nzuri Kama Milambo uhehe ingekuweje?