meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,832
Habari za jioni wadau wote wa Jf.
Swali hapo juu ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha majonzi mengine kwa Taifa.
Hoja yangu itajikita katika kuwarejesha nyuma ,tulipo na tunapotakiwa kufika kama Taifa.Lakini haswa haswa nitaiangazia Chadema katika safari yake ya kisiasa njia nzuri,ngumu na ambaya ilizopitia.
Nitajaribu kufupisha na kugusia mambo muhimu pekee.
Mosi
Chadema kilikuwa ni Chama imara sana hadi kukawa na tetesi kuwa Mwalimu Nyerere alikitabiria kuwa Chama bora .Hii ilikuwa ni ile Chadema iliyokuwa na influence kubwa au uongozi wa Mzee Mtei.
Chadema hii ilijijenga vizuri sana na hakuna kumbukumbu rasmi ya kujijenga kupitia maandamano ama vurugu.Nakumbuka kipindi hiko Kulikuwa na mshike mshike kati ya CCM,POLISI na CUF.
utulivu huu uliiifanya Chadema iwe kivutio mbadala cha kisiasa kwa wananchi wapenda amani na mabadiliko.
Pili
Chadema ilianza kubadilika zaidi kimkakati chini ya ukatibu wa Dr slaa,makamu mwenyekiti Chacha Wangwe na wabunge kama Zitto na Mnyika ambao waliichachafya vilivyo serikali bungeni kwa hoja nzito na hivyo kuwavutia wananchi na pia kuwaelimisha na kuhamasisha wananchi.
Tatu
Baadae Chadema ilianza siasa za kiuhanarakati lakini zikiwa na mikakati mizito ya kujijenga kama Chama katika level ya mtaa.Hii inatokana na ukweli kuwa CCM ilikuwa inawabana pengine kwa kutumia dola na pia ilikuwa inajivunia ukubwa wake kichama katika level ya nyumba kumikumi.
Tukumbuke hapa ndipo tulipoanza kushuhudia kamatakamata ,virungu,maandamano na mauaji ya hapa na pale .naweza kusema hadi mauaji ya wanachama wa chadema 2011 jijini Arusha yanaweza kuwekwa katika hatua hii.Ikumbukwe kuwa katika hatua hii CCM ilienda kisayansi kwa kujaribu kuivuruga Chadema from within.Hiki ndipo kipindi kulipoibuka usaliti na kutoaminiana ndani ya Chadema hadi kina Zitto,Kitila na wengine kuondolewa ndani ya Chama.
Nne
Hii ni hatua iliyokuwa na sifa ya overambition ambapo Chadema ilitaka kuharakisha ukuaji bila mkakati unaoeleweka zaidi ya tamaa.
Haya yalitokea mnamo mwaka 2015 na Chadema ikaingia mkenge wa kucheza karata au kamari za kumchukua lowassa ili wachukie dola.
Hatua hii ilikuwa ni very premature au ilikuwa sahihi lakini haikufuata mipango iliyopoangwa n Dr Slaa au hata Baregu na hivyo mwisho wa siku pakatokea mparanganyiko wa misimamo.
Inawezekana hatua hii ilikuja prematurely kwa sababu ya ubinafsi au maslahi binafsi ya Mbowe na baadhi ya wafuasi wake.
Hatua hii iliaacha chadema na makovu makubwa sana na hatimaye kutoa pumzi kwa CCM kupata fursa mpya ya kujitathmini na kujipanga.
Ni hatua iliyoidhoofisha CCM lakini ilitoa mwanya mpana wa CCM Kujipanga upya .
Tano
Hii ni hatua ngumu kwa Chadema iliyoshindwa katika kamari ya kisiasa 2015.Ni hatua iliyoiacha Chadema with confusion na wasijue wafanye nini tena.
Muhimu sana ni hatua hihi hihii ambapo CCM iliingia katika great recovery and great reforms.
Ccm Chini ya Magufuli ikaamua kujirudi,kuiga mazuri ya Chadema na kudhibiti vilivyo fursa walizopata chadema(ambazo walizitumia vibaya).
Hapa Chadema ilipoteza think tanks akiwemo katibu Dr Slaa na wafuasi wengi wenye weledi na kubakia na makapi ya CCM YA KIFISADI iliyokataliwa na wananchi.
Katika hatua hii ambayo ni sasa Chadema ilipoteza agenda na hivyo kubakia kwenye matukio au tuseme kurukiarukia matukio.
Bado Chadema inaendelea kupoteza wanachama wenye weledi kwa kuwa hakuna agenda au msimamo inayoeleweka.
Ni katika hatua hii ya tano tuna watu kama SUMAYE na LOWASA waliotegemewa kubadilisha hali ya mambo ndani ya Chadema wakionesha failure kubwa kiasi cha Mbowe na lissu kubaki na Ukiwa au wapambanaji wanaokosa ushauri wa mapambano.
Hatua hii inataka kumrudisha Mbowe na baadhi ya wafuasi wake nyuma katika uhanaharakati huku wakisahau kuwa CCM chini ya Magufuli sio ile ya JK.Pia inavyoonekana SUMAYE NA LOWASSA hawapo tayari kujiunga na Mbowe katika kurudi kwenye uhanaharakati na hivyo wamemuachia Mbowe ajaribu tena gia nyingine ya anga.
HITIMISHO
Nimejaribu kwa kadri iwezekanavyo kuchambua trend ya ukuaji wa kisiasa na muelekeo wa Chadema kwa kadri ninavyoifahamu.
Ninajaribu kuwashawishi Chadema warejee kwenye hatua muhimu kabla ya hatua ya tano (confusion state) wajitathmini na kujipanga upya.
Sijaona ni lini Chadema ilikaa kwa nia ya kujitathmini hasa baada ya maamuzi ya kumchukua lowassa ...maamuzi ambayo yamewayumbisha na kupoteza dira especially wakati huu wa CCM ya Magufuli.
Kwa maslahi ya Taifa kwenda mbele likiwa na amani Chadema lazima ikae chini na kujipanga upya hata kama ni kwa miaka 10 au 20 ijayo ili kuaminika na watanzania na hivyo kushika dola.
Plan ya Chadema isiwe kushika dola tu kwa namna yoyote bali kushika dola with a purpose na mikakati mbadala ya maendeleo.
Wananchi wanahitaji maendeleo na ustawi wa maisha yao na sio kuona mabadiliko ya viongozi tu katika nafasi za kisiasa.
wananchi wameamua kuwarudisha wabunge wa UKAWA waliojiuzulu kwa kuwa hawaamini katika chama kushika hatamu bali mtu mwenye sera zenye muelekeo wa wanayoyataka.
Kwa maoni yangu ni kuwa bado sana hatujafika kwenye stage ya vurugu na harakati za kweli za kisiasa yaani zile za afe refa afe kipa lazima tushinde.Bado hatujawaona wanaharakati na wafia chama wa CCM wakiamua kulianzisha ili ku-counteract Vyama pinzani .kinachoonekana ni juhudi na mipango za kutaka kupaint mambo yaliwahi kutokea hapo awali na kuyafanya ndio climax.
Nikirudi kwa watajwa hapo juu katika title ya thread nawaona kama vile wameshindwa kutumia uheshimiwa wao kujipanga na kumpanga Mbowe ili aweza au waweze kufikia lengo.
Hivyo natoa wito kwao kufanya juhudi zote kuiweka Chadema sawa for the good future of URT.
Kwa leo ni hayo tu.
N.B
Matusi na jazba tuweke kando !