Ujinga mwingine unatisha sana,
Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.
Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.
Mwaka 1968 mshahara wa 4500 pesa nyingi sana alikuwa anatakiwa kulipwa 2500.
Tatizo sio hoja yako mrembo faiza tatizo ni chuki yako kwa Nyerere anyway sijui ni nini alichowafanyia wazazi wako maana wewe ni mtoto na utakua umesimuliwa tu na kujenga chuki. Yote kwa yote kua na moyo wa kusamehe. Sahahu yaliyopita tugange yaliyopo na yajayo. Makosa aliyofanya Nyerere wakati huo Tuyaache tufanye yetu mazuri kwa sasa. Muda bado upo
Uelewa wako unatia shaka. Mzee mtei anamlinganisha Nyerere katika nafasi yake na maraisi wengine wa siku hizi katika nafasi ile ile. Kama Nyerere hakuwa na shida ni vivyo hivyo kwa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Jakaya. Hata hawa wasipochukuwa mishahara yao haina tofauti na Marehemu Nyerere asingalichukua. Sasa kama vile haitoshi hawa viongozi wa sasa sio hawapunguzi mishahara kwa kuwahurumia masikini bali pia huwaibia zaidi masikini na kujilimbikizia wao wenyewe na jamaa zao. Inashangaza kama huelewi mantiki ya Mzee Mtei, basi una safari ndefu sana kuweza kuchambua mambo. Mtei hamlinganishi Marehemu Nyerere na mtu kama wewe anamlinganisha na viongozi walioshika au kupata kushika nafasi kama yake. Upo hapo? Ua umejianda kutetea tu jambo lolote ili mradi uonekane umechangia? Hivi kweli unaweza kulinganisha uadilifu wa Marehemu Nyerere na kiongozi yupi wa sasa Tanzania ya leo? Mtei ingawaje haikuwa dhamira yake kupunguza mshahara wake lakini kwa kuona Boss wake amepunguza alipunguza pia mshahara wake, ina maana Mzee Mtei aliona aibu Boss wake apunguze halafu yeye apate zaidi ya Boss wake. Angalao Mtei aliona aibu, viongozi wa sasa hata HAYA hawana.
FaizaFoxy kwani JK anapolipwa Milion 32 kwa mwezi hapati nyumba bure?Hapati chakula bure?Hapati matibabu bure?Hapati huduma zote bure?
Mpe Nyerere sifa zake!Sikubaliani na baadhi ya maamuzi ya Nyerere alipokuwa madarakani(hasa Azimio la Arusha)lkn kwenye uadilifu aliwashinda tena kwa mbali ma Rais wote waliokuja hasa Kikwete ambaye sio MWADILIFU kwenye pesa za UMMA!
Nyerere asingekubali kujitengea Bilion 50 za safari zake(JK kajitengea) huku bohari ya madawa kwa TZ nzima ikipewa Bilion 48 tu
Hapa ni sawa na Mzee Slaa kulipwa mshahara na marupurupu sawa na mbunge.
Hawa mafisadi!!! Thubutu!!! Mishahara yao mikubwa sana na haikatwi kodi na bado haiwatoshi hivyo wanaamua kufanya ufisadi wa matrilioni mwaka nenda mwaka rudi kisha kwenda kuzificha nchi za nje. Maslahi ya Tanzania na Watanzania hawa mafisadi hawayajali kabisa wanachojali ni matumbo yao.
Inaonekana una chuki kubwa sana na mwl nyerere
Tatizo sio hoja yako mrembo faiza tatizo ni chuki yako kwa Nyerere anyway sijui ni nini alichowafanyia wazazi wako maana wewe ni mtoto na utakua umesimuliwa tu na kujenga chuki. Yote kwa yote kua na moyo wa kusamehe. Sahahu yaliyopita tugange yaliyopo na yajayo. Makosa aliyofanya Nyerere wakati huo Tuyaache tufanye yetu mazuri kwa sasa. Muda bado upo
Tuanze na ruzuku ya chadema inayoishia makao makuu vp mgao umekaaje? Make katibu anakula sawa na mbunge na hiyo ni moja ya masharti yake.
Hapo ukienda kwa vingozi wengine wa chini yake bila kumsahau mwenyekiti utakuta hali ndo hizohizo hazjatofautiana sana.
Leo ni karibu miaka 22 hata ofisi mmeshindwa kujenga lakini mnajua kulipana mishahara mizuri... mikoani ofisi zimechoka alafu mnakuja na ngonjera za baba mwenyenyumba hayatola!!!
Usikimbilie kubandua banzi kwenye jicho la mwenzio wakati lako lina boriti.
Michango yako hasi dhidi ya Nyerere inakufanya uonekane una chuki binafsi na huyu mtu,ambaye kwa kauli yake alikiri kuwa hakuwa malaika kuna makosa aliyafanya na mazuri mengi pia.Ujinga mwingine unatisha sana,
Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.
Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.
Michango yako hasi dhidi ya Nyerere inakufanya uonekane una chuki binafsi na huyu mtu,ambaye kwa kauli yake alikiri kuwa hakuwa malaika kuna makosa aliyafanya na mazuri mengi pia.
Lakini aliwashangaa warithi wake kufauata mabaya aliyoyafanya na kuacha mazuri,wakati mwingine inaonekana ni kwa vile hakuwa wa hitikadi yako.
jengeni hoja za maana acheni porojo sasa ulitaka mkwewe akutafune wewe?
Kama unakiri kuwa Nyerere mwenyewe kakiri, kwa hiyo hutaki tuyaainishe makosa yake ili wengine wasirudie?
Huwa mnafikiri au mnabwabwaja tu?
Sifa ipi? uadilifu upi? kudhulumu watu mali na roho zao ndio uadilifu?
Unajuwa ni wangapi waliokufa kwenye hayo maamuzi ya "Azimio la Arusha" ambayo hukubalini nayo? hata idadi hawajulikani, watu walihamishwa vijiji vyao vya asili na kupelekwa kutupwa maporini, waliokufa kwa magonjwa haya, waliokufa kwa kuliwa na wanyama haya, waliokufa kwa kugongwa na nyoka haya.
Huo ndio uadilifu?
Nyerere HAIKUIGEUZA Ikulu kuwa pango la WANYANG'ANYI wala yy na FAMILIA yake HAWAKUITUMIA ikulu kwa faida zao bifasi!Sikupata kushuhudia WATOTO wa Nyerere wakija Mbeya kusomewa taarifa za mkoa kama nao wapo ndani ya uongozi wa dola!!
Kwenye maadili ya matumizi mazuri ya hela zetu Nyerere anamzidi JK tena kwa mbali sana,kwenye utawala wa sheria, KIDEMOKRASIA na kuvumiliana ndiyo sifa pekee ya JK anayomshinda Nyerere! FaizaFoxy usichanganye sifa hizo mbili!!
Kwahiyo unaanika ya utawala wa nyerere ila ya utawala wa sasa mwiko.
Huo ni upunguani wa hali ya juu, uwe wa miaka 100 iliyopita uwe wa leo, Rais ni Rais tu.
Kuna tofauti ipi ikiwa katiba na kanuni ya kuuendesha tasisi ya Urais ni hiyo hiyo au uliibadili wewe?
Huu ujinga mtauwacha lini Watanzania? hivi mshahara wa Nyerere au wa Kikwete unamsaidia nini Mtanzania? kuna Watanzania kibao wana mishahara mikubwa na kipato kikubwa kuliko Rais x 1000.
Mbona mnakuwa wajinga kiasi hiki?