Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Tofauti ya mtei na jussa ni ipi ktk hzi kauli zao,?
 
Mimi nadhani watu tunachanganya mambo kwenye kampen watu huwakilisha chama kwa jambo lolote kwan ndicho kilichomtuma, kwenye mijadala ya kitaifa wote tu watanzania na haki ni sawa. kumzua mtu kutoa mawazo yake ni kujenga woga kwa watu kusemea kasoro zinazojitokeza, Tuache malumbano.
 
ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu! Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?

Hatima ya mustakabali wa tanzania itaamuliwa na kakundi kadogo sana ka watu zaidi kidogo ya milioni moja dhidi ya milioni 44. Bado hatupo salama. ngoja mlazimishwe kufuga midevu!

Mzee Mtei has stated a fact kuwa katika tume ile waislam ni wengi kuliko wakristo, sasa bisheni kama hilo sio kweli! Mtu wenu anaeeneza udini mkweree mnaacha kumkalipia mnamsonga mtu mwenye ujasiri wa kusema ukweli; hii yote ni kwasababu nyie watu wa magamba mmezoea unafiki!

ZITTO, hana adabu, ukweli unamuuma? Zanzibar haina wakristo? Iweje wajumbe 15 wote wawe waislamu? Hakuna wakristo Zanzibar? Aliyefilisika ni Zitto au Mtei? Sisi tunamheshimu sana mzee Mtei, hivyo tuachie mzee wetu, wewe ukiona umechoka? Sepa! Mnafiki sana wewe.

namuunga mkono Mzee Mtei! Sabababu ni zifuatazo:
Kadri kundi moja linavyozid ndivyo na hoja za upande huo zitakapopitishwa kirahisi!
Leo hii tunaona ccm inavyoburuza bunge c ni kwasababu ya wingi wao?
Unategememea ije hoja ya mahakama ya Kadhi hapo mezani itapingwa kweli?
tuombe Mungu aingilie kat bila hivo katiba itakuwa ya mrengo mmoja!
Ninyi kaeni mjiridhishe kwa kutetea upuuzi.........
Wenye akili zao ndani ya CDM walikaa kama kamati na kutathimini tamko la huyu Babu na athari zake kwa chama na jamii....
Wakabaini lina mushkeri mkubwa sana usiofuata misingi yetu kama taifa ya kuangalia mambo kwa jicho la kidini na kikanda
Na hatimaye wakaja na tamko hili haraka sana kumnawa asihusishwe na chama kwa aliyoyatamka
JIULIZE..... ni lini umewahi kusikia CDM inatoa tamko kutaka alichotamka kiongozi wake kisihusishwe na chama.....zingatia kwamba Mtei ni muasisi na ana influence kubwa ndani ya chama lakini still viongozi wameona kuna haja ya kuipotezea kwa kutoa tamko rasmi dhidi ya maoni yake?

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwamba maoni binafsi ya viongozi na wanachama wasiokuwa na mamlaka kwa mujibu wa katiba, kanuni na itifaki ya chama kuwa wasemaji wakuu wa masuala ya chama katika ngazi husika yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

CHADEMA kinatoa taarifa hii kufuatia maoni binafsi ya muasisi na mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA juu ya wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba yanayoelezwa kutolewa katika mtandao wa jamii wa Jamii Forums kutafsiriwa kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

CHADEMA kinatoa mwito kwa wachangiaji katika mitandao ya kijamii na wananchi kwa ujumla kuzingatia kuwa CHADEMA bado haijatoa kauli juu ya wajumbe wa tume husika kwa kuwa bado CHADEMA inaendelea kufanya uchambuzi juu ya wasifu wa wajumbe wa tume husika na mchakato wa uteuzi wao kama tulivyoeleza kwenye taarifa kwa umma tuliyotoa tarehe 7 Aprili 2012.

Hata hivyo, izingatiwe kwamba uchambuzi wa wasifu wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika unaoendelea kufanywa na CHADEMA hauhusu dini za wajumbe wa tume kwa kuwa CHADEMA hakiamini katika udini bali unahusu uwezo na uadilifu wa wajumbe husika na iwapo umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

Izingatiwe pia kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya 3B kifungu cha 3.1.9 ikiwa ni sehemu ya misingi iliyopo kwenye itikadi ya CHADEMA ya mrengo wa kati, CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola na na misingi mingine ya CHADEMA ya kujenga chama na taifa lenye kutoa fursa kwa kuzingatia uwezo na uadilifu bila kujali tofauti zingine.

Pamoja na kujulisha umma kwamba CHADEMA kinaendelea kufanya uchambuzi wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika, tulieleza kuwa CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Tunasisitiza umuhimu wa Serikali kutoa kauli kwa umma kuhusu ratiba ya marekebisho ya awamu nyingine ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 kwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Bunge imetangaza kuwa Mkutano wa Bunge utaanza tarehe 10 Aprili 2012 bila marekebisho ya sheria ya katiba kuwa sehemu ya orodha ya miswada ya sheria inayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa saba wa Bunge.

Tunarejea kuutarifu umma kuwa Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 itafanya kikao chake karibuni mara baada ya uchambuzi kukamilika kupitia taarifa ya uchambuzi unaofanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

Imetolewa tarehe 09 Aprili 2012 na:

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Kama ni Jambo leo wala siumizi kichwa,labda yaandike magazeti mengine yasiyo ya magamba.
 
kamanikweli mh.zitto umesema hivyo sawa, ila kumbuka siyolazima usemeekilajambo ilikulinda haibayako mambomengine yanyamazie.NAKUHESHIMU SANA
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Kama alichosema Mzee Mtei ni wingi wa waislam katika tume nafikiri hiyo ni FACT. Kwa vile mtoa mada na Zitto hawajaongelea so what napata shida kuona usahihi wa tamko la Zitto hasa nianapoangalia nafasizao katika cham kimoja cha CDM i would the it is un called for - what was he Zitto trying to achieve?
 
Huyu bwana mdogo anachonifurahisha ni kwamba hajui kumun'gunya maneno, na hicho ndicho kinachowatoa watu roho. Inawezekana kweli kasema hivyo, au pia yawezekana mwandishi kaweka vile alivyoona inampendeza.
Mzee Mtei kweli anazeeka vibaya, maswali yake ya udini hayana tija. Rais alizingatia taratibu? Jibu ni NDIO. Tukianza kuulizana uwiano wa wakristu na waislam mbona sisi wakristu tutaumbuka! Lakini ni kwa ajili tunakuwa tunafit kuwa tulipo, sasa vidole vya nini? Hebu tuache uchochezi wa kidini. Maendeleo yenyewe hatuna, halafu tunataka kuongeza matatizo yasiyo na tija.

Haya ndio mambo hatukuyataka toka awali! rasimu ya muswaada wa mabadiliko ya katiba haikuletwa kwa wananchi waijadili, ndio maana unakimbilia kuuliza kama rais alizingatia taratibu au la. hauhoji uzuri wa taratibu hizo, ama zilivyowekwa. Utaratibu huu tayari unaonyesha ghilba imetumika. Hivi nani anawawakilisha wapagani kwenye hiyo tume, TUTARAJIE KUPATA KATIBA ITAKAYOKATALIWA NA WANANCHI!!!!!
 
Sasa mlivyokuwa mnalalamika CCM inawatukana kumbe ni Mwigulu na Lusinde yalikuwa mawazo yao binafsi.
Yaani we ukichanjwa inatoka damu ya kijani tu!!!! pole sana kwa huo ugonjwa wa kijanijani...
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

CDM inabidi ichukue maamuzi magumu, Mzee wa watu alikuwa very clear nashangaa watu wanavyokuza kauli yake. Ni ukweli mtupu kwamba hata serikali ya JK imeelemea upande huo kwani we angalia viongozi wakuu wa nchi wa kuteuliwa.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Mimi nadhani watu tunachanganya mambo kwenye kampen watu huwakilisha chama kwa jambo lolote kwan ndicho kilichomtuma, kwenye mijadala ya kitaifa wote tu watanzania na haki ni sawa. kumzua mtu kutoa mawazo yake ni kujenga woga kwa watu kusemea kasoro zinazojitokeza, Tuache malumbano.
Kama alichosema Mzee Mtei ni wingi wa waislam katika tume nafikiri hiyo ni FACT. Kwa vile mtoa mada na Zitto hawajaongelea so what napata shida kuona usahihi wa tamko la Zitto hasa nianapoangalia nafasizao katika cham kimoja cha CDM i would the it is un called for - what was he Zitto trying to achieve?
Kwani mzee mtei kasema uongo ? M naona kasema kwel kabisa

Mkuu tatizo hapa sio kumzuia mtu kutoa maoni yake....HAPANA
Tatizo hapa ni aina ya maoni unayotoa.

Unadhani akina shekh Ponda na basaleh huwa hawatoi maoni yao wanaposema wanataka
uwiano sawa mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu, wakuu wa idara, mabalozi, ajira serikalini,
uwiano sawa wa billions tunazopewa taasisi za kikristo kuendesha hospital na mashule

Unajua tunacho wajibu humu.........ni zaidi ya matusi
So why not Mtei?
 
zito acha upumbavu wako.tamaa yako ya urais inakusumbua.wewe ni kibaraka magamba.mzee mtei ni zaidi ya unavyofikiri.kuna mambo ya msingi ya kufikiria,ukiondoa masuala ya udini,lazima tujifikirie sisi watanganyika nafasi iko wapi ktk suala la katiba.
 
Ninyi kaeni mjiridhishe kwa kutetea upuuzi.........
Wenye akili zao ndani ya CDM walikaa kama kamati na kutathimini tamko la huyu Babu na athari zake kwa chama na jamii....
Wakabaini lina mushkeri mkubwa sana usiofuata misingi yetu kama taifa ya kuangalia mambo kwa jicho la kidini na kikanda
Na hatimaye wakaja na tamko hili haraka sana kumnawa asihusishwe na chama kwa aliyoyatamka
JIULIZE..... ni lini umewahi kusikia CDM inatoa tamko kutaka alichotamka kiongozi wake kisihusishwe na chama.....zingatia kwamba Mtei ni muasisi na ana influence kubwa ndani ya chama lakini still viongozi wameona kuna haja ya kuipotezea kwa kutoa tamko rasmi dhidi ya maoni yake?

Kitu kizuri pekee naweza kukwambia ni kuwa subiri uje kushurutishwa kufuga midevu ndipo ujue nani mpuuzi kati yako na hii tume!!!
 
Kumbe jambo leo, limerudi mtaani. Tangu Arumeru Mashariki sijalisikia.
 
Maoni ya mtei c ya chadema hivi lusinde alivyotukana ccm ndo wametukana.
 
Mh Zito kweli wewe ni kiboko kwa mustakabali wa taifa hili hasa pale kunapo ibuka mambo ambayo yana hatarisha upendo baina yetu wadanganyika. Napenda unijibu maswali haya:
1. Ulitoa mawazo gani pale mbaguzi Jussa aliposema kuwa CUF imeshindwa jimbo la Uzini kwa sababu wakristo (wabara) ni wengi pande hizo???????
2. Unakumbuka kampeni za mwaka 2010!!!! Moja kati ya mambo yaliyo kuwepo kwenye manifesto ya CCM ni suala la mchakato wa mahakama ya KADHI, naamini unaisoma na kuielewa vizuri katiba yetu kuhusu masuala ya dini.Ni mh Serukamba pekee aliye tamka wazi bungeni kuwa CCM imewatongoza waislamu ili wakipigie kura kwa gear ya mahakama ya kadhi. Je ulitoa tamko????
3. Wakati wa kampeni Dk Slaa aliitwa mdini ataendeleza mfumo Kristo, je ulitoa tamko???
Mheshimiwa sana ni mpumbavu tu ambaye anaweza kuibomoa nyumba yake akiamini kuwa anajenga. Kila mtu anauhuru wa kutoa mawazo yake lakini je unajenga, unamnufaisha nani? Kumbuka mnasafari ndefu 2015 mtafika kwa style hii? Soma habari ya Nuhu na mwanae aliye mcheka baada ya kubaki utupu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom