Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa kuwania urais

Haelewekagi huyo,mara tume ina waislamu wengi mara oooh mgombea binafsi awepo mara asiwepo, mladi ubinafsi tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu,
Una hakika na ulichoandika hapa chini? Nchi kubwa na zenye demokrasia mfano USA na nchi zingine zina mgombea urais huru.

Rais inatakiwa awajibike kwa wananchi na sio kwa vyama.

True That... Tutakuwa ni NCHI PEKEE DUNIANI yenye MGOMBEA BINAFSI na hii ni kwasababu ya VIONGOZI waliobaki NCHINI hawakuwa VIONGOZi walipewa nafasi kuzijaza tuuu kwasababu ya UNYENYEKEVU na SIO UELEWA wa SIASA...

Sasa we ARE GOING TO PAY DEARLY...
 
Kwenye hili la wagombea huru ni lazima tuwe makini sana. Naamini sheria itawekwa vizuri ili kupunguza uwezekano wa kupata Rais kibaraka.

Nadhani tutahitaji pia kutizama tena definition ya "chama"/"chama cha siasa". Maana katika nafasi hiyo ya urais, uwezekano mkubwa ni kuwa mogombea huru atakuwa na kundi (sizable tu) ambalo lina muunga mkono au kuunga mkono "sera" zake.

Lakini kwa vyovyote vile, uwepo wa route ya kushiriki uongozi wa nchi bila kulazimika kuwa na chama siasa ni demokrasia zaidi kuliko hali ilivyo sasa.
 
Wrong!! rais anachaguliwa na wananchi na anawajibika kwao tu, na siyo kwa vyama vya siasa. Haya mambo ya kamati kuu za vyama hayana maana.

usichokijua ni kuwa kutakuwa na mvurugano wa kisiasa.wanasiasa watatumia mbinu zozote za kujitafutia umaarufu ndani ya vyama vyao muwaone mashujaa then dakika za majeruhi wanajitoa kwenye vyama wasipoteuliwa na kusimama kama wagombea binafsi.hapo tutapata rais mwenye tamaa ya madaraka,mwenye visasi,chuki,atatengeneza baraza la mawaziri kwa kujuana na mwisho wa siku atakuwa huru kwa sababu alijileta mwenyewe na mkamchagua yeye so hakuna wa kumwajibisha.usinidanganye wananchi watamwajibisha coz hata huyu tuliyenaye kama hao wananchi wangekuwa na huo uthubutu wa kuwajibisha wangekuwa tayari wamemwajibisha kwa wanavyomlalamikia but coz ni mazezeta hawawezi.
 
Nilitoa maoni yangu kwamba Rais awe ni kiongozi wa chama cha siasa kilicho na sera zinazokubalika na pia wasaidizi wanaojulikana na kukubalika kwa wapiga kura. Wapiga kura wachague chama chenye sera na viongozi waadilifu, wazalendo na wenye kutaka kutuondoa katika lindi la umaskini.

Fisadi lililokwapua maliasili na rasilimali za umma na kuzificha katika akaunti za siri nje ya Tanzania, linaweza kuzirudisha na kuzitumia kununua kura na kuchakachua matokeo ya Uchaguzi Mkuu, ili lituongoze kama Rais wa kujitegemea. Likifaulu kuchaguliwa ndio tumekwisha!

Naamini pia tatizo la gesi Mtwara, ambalo naliona kama Janga la Kitaifa, lingeweza kuepukwa kama serikali za majimbo au wilaya zingepewa uwezo wa kutumia raslimali zao kwa maelewano na Serikali Kuu.

Nawasamehe wanaotumia lugha isiyokuwa na heshima kwa wazee kama mimi. Wamelelewa vibaya. Poleni sana.
 
Mzee Mtei,
" Shimboni shafoo...."

Tunayaheshimu sana maoni yako kwa mustakabli mwema wa nchii hii ILA na sisi tusioa na vyama tuna maoni yetu pia.. Tunahitaji Rais asiye na chama ila tu awe na sera za kutuambia atafanya nini tukimkabidhi ile nyuma pale Plot # 1 Magogoni hilo la kuwa Fisadi anaweza rudi kwa mgongo wa nyuma naamini Vetting itafanyika kabla ya kupewa bendera ya kuipeperusha...na atajulikana tu vyanzo vyake vya fedha !

Hakitaharibika kitu, I promise you !
 
Kauli aliyotoa mzee Mtei baada ya kuundwa kwa tume ya katiba imemshusha kabisa thamani kisiasa kiasi kwamba chama alichokiasisi kikajitenga na kauli ya muasisi huyo.

Mtei muda wake UMESHAPITA.
 
Mkuu Kiranga unaweza kutupa mifano ya nchi ambazo zinaongozwa na wagombea binafsi?

Watu wengine tuna wasi wasi kama Mzee Mtei, lakini tukipata mifano hai iatatusaidia.
 
Fisadi lililokwapua maliasili na rasilimali za umma na kuzificha katika akaunti za siri nje ya Tanzania, linaweza kuzirudisha na kuzitumia kununua kura na kuchakachua matokeo ya Uchaguzi Mkuu, ili lituongoze kama Rais wa kujitegemea. Likifaulu kuchaguliwa ndio tumekwisha!

Kwani fisadi huyo anashindwa vipi kuanzisha chama cha siasa akanunua kura? Kwani kununua kura mpaka awe mgombea binafsi?

Kama wewe uliweza kuanzisha CHADEMA, fisadi huyo unayemuogopa atashindwa vipi kuanzisha CCJ?
 
Mkuu Kiranga unaweza kutupa mifano ya nchi ambazo zinaongozwa na wagombea binafsi?

Watu wengine tuna wasi wasi kama Mzee Mtei, lakini tukipata mifano hai iatatusaidia.
Kuwa na Rais binafsi na kuruhusu ni vitu viwili tofauti.

Marekani wanaruhusu wagombea binafsi na kila uchaguzi huwa kunakuwa na wagombea binafsi wa Urais.
 
ana HAKI YA KUTOA MAONI YAKE KAMA MTANZANIA SIDHANI KAMA KUNA TATIZO LOLOTE HAPO.
 
Nilitoa maoni yangu kwamba Rais awe ni kiongozi wa chama cha siasa kilicho na sera zinazokubalika na pia wasaidizi wanaojulikana na kukubalika kwa wapiga kura. Wapiga kura wachague chama chenye sera na viongozi waadilifu, wazalendo na wenye kutaka kutuondoa katika lindi la umaskini.

Fisadi lililokwapua maliasili na rasilimali za umma na kuzificha katika akaunti za siri nje ya Tanzania, linaweza kuzirudisha na kuzitumia kununua kura na kuchakachua matokeo ya Uchaguzi Mkuu, ili lituongoze kama Rais wa kujitegemea. Likifaulu kuchaguliwa ndio tumekwisha!

Naamini pia tatizo la gesi Mtwara, ambalo naliona kama Janga la Kitaifa, lingeweza kuepukwa kama serikali za majimbo au wilaya zingepewa uwezo wa kutumia raslimali zao kwa maelewano na Serikali Kuu.

Nawasamehe wanaotumia lugha isiyokuwa na heshima kwa wazee kama mimi. Wamelelewa vibaya. Poleni sana.

Shikamoo Mzee Mtei,

Mzee kwani vyama vya siasa hakuna mafisadi si tumeona chama chako kilitoa orodha ya mafisadi pale Temeke Mwembeyanga.

Sidhani kama Watanzania wote wanaweza kuamua kumchagua kiongozi fisadi.

Mzee hiyo kauli yako itakuwa inabaka demokrasia kwa wale wasiokuwa na vyama.
 
Kuwa na Rais binafsi na kuruhusu ni vitu viwili tofauti.

Marekani wanaruhusu wagombea binafsi na kila uchaguzi huwa kunakuwa na wagombea binafsi wa Urais.

Mkuu kwani kuna kosa gani kuuliza mifano hai?! Kama ipo si iwekwe hapa?
 
True That... Tutakuwa ni NCHI PEKEE DUNIANI yenye MGOMBEA BINAFSI na hii ni kwasababu ya VIONGOZI waliobaki NCHINI hawakuwa VIONGOZi walipewa nafasi kuzijaza tuuu kwasababu ya UNYENYEKEVU na SIO UELEWA wa SIASA...

Sasa we ARE GOING TO PAY DEARLY...

Mkuu kabla haujaandika jaribu kwanza kufanya utafiti japo kidogo Tanzania siyo ya kwanza kuruhusu mgombea binafsi.
 
Rais siyo wa chama cha siasa Rais ni wa Wananchi. Wananchi ndiyo wana haki ya kuchaguwa ni mtu wa gani ambae wanataka hawaongoze siyo lazima chama.

Mfano mdogo bungeni watu wapo kwa ajili ya vyama siyo Wananchi.

Mtei pumzika tu mzee wetu kwanza ulilalamika hii tume imejaa udini Waislam wengi.

Kuna watu hawataki mambo ya vyama vya siasa.

Kama kiongozi anawajibika kwa wananchi, kwanini rasimu inasema mbunge akifa achaguliwe mbadala toka chama chake na sio aliekuwa wa pili ktk uchaguzi!
 
Mzee Mtei, si kweli.
Mgombea binafsi ni haki ya mtu na haipaswi kufungwa na kuzuiwa na kikundi cha watu.
Kwanza, kama atachaguliwa kuwa rais hapo ni wananchi watakuwa wamemchagua kiongozi wanayedhani anawafaa.
Mtu atakayepata zaidi ya asilimia 50 tena akiwa biafsi huyo anafaa.

Mzee Mtei lazima atambue kuwa uwepo wa mgombea binafsi hauna maana ya kutoa rais tu. Unatoa nafasi hiyo kwa wabunge hadi madiwani. Kwa wenzetu mgombea binafsi ni alternative kama vyama vitaleta wendawazimu na wehu katika chaguzi.

Nafasi ya mgombe binafsi inaleta uwajibikaji wa dhati ndani ya vyama na hivyo uwezekano wa kupata wagombea wazuri kutoka katika vyama unakuwa mkubwa. Mizengwe inapungua kwa maneno mengine.

Halafu mzee Mtei anashangilia viti maalum. Tumekataa viti maalumu kwasababu ni mzigo tu usio na manufaa,
Tunaamini mwanamke au mwanaume mwenye uwezo atachagiuliwa kwa uwezo wake na syo surali au gauni.

Hakuna sababu ya kuwa na mgombea mwanamke halafu mgombea mwanaume.
Yaani jimbo moja wabunge 2. Huu ni upuuzi kweli kweli, huko kwenye haki za binadamu hawafanyi upuuzi huo sisi tunaupata wapi?
 
Nilitoa maoni yangu kwamba Rais awe ni kiongozi wa chama cha siasa kilicho na sera zinazokubalika na pia wasaidizi wanaojulikana na kukubalika kwa wapiga kura. Wapiga kura wachague chama chenye sera na viongozi waadilifu, wazalendo na wenye kutaka kutuondoa katika lindi la umaskini.

Fisadi lililokwapua maliasili na rasilimali za umma na kuzificha katika akaunti za siri nje ya Tanzania, linaweza kuzirudisha na kuzitumia kununua kura na kuchakachua matokeo ya Uchaguzi Mkuu, ili lituongoze kama Rais wa kujitegemea. Likifaulu kuchaguliwa ndio tumekwisha!

Naamini pia tatizo la gesi Mtwara, ambalo naliona kama Janga la Kitaifa, lingeweza kuepukwa kama serikali za majimbo au wilaya zingepewa uwezo wa kutumia raslimali zao kwa maelewano na Serikali Kuu.

Nawasamehe wanaotumia lugha isiyokuwa na heshima kwa wazee kama mimi. Wamelelewa vibaya. Poleni sana.

Mzee mtei with all due respect mawazo yako yaheshimiwe lakini ukweli utabaki palepale kwamba kwa dunia ya sasa yamepitwa na wakati

Ulianza kwa kuiangalia tume hii kwajicho wanalotumia akina shekh ponda, jicho la udini kitendo ambacho hakikubaliki kabisa dunia ya leo na wameprove kwamba ulikuwa wrong kwa kuja na rasmu ambayo haina punje la udini ndani yake

Sasa unakuja na madai ya mgombea binafsi hafai kwa urais, why?
Kigezo cha ufisadi hakina mshiko.
Rais haongozi kutokana chama au kundi linalo mzunguka tu, anaongoza kutokana na taratibu na sheria
Hatuwezi kuzuia mgombea binafsi ambao wapo wengi na wanasifa kwa kuogopa mafisadi, hii ni sawa na kukataa kufanya jambo jema kwakuwa kunamabaya huwa yanajitokeza ndani yake
Cha umuhimu kama taifa ni kuweka misingi ambayo haitawapa nafasi mafisadi kujipenyeza maana hata humu kwenye vyama vyenu wamejaa tele

Ushauri wangu kwako ni kuwa muangalifu sana na kauli zako ambazo naomba niamini zinaendana na umri wako vinginevyo unazidi kuififisha hekma na maono yako uluojijengea
 
usichokijua ni kuwa kutakuwa na mvurugano wa kisiasa.wanasiasa watatumia mbinu zozote za kujitafutia umaarufu ndani ya vyama vyao muwaone mashujaa then dakika za majeruhi wanajitoa kwenye vyama wasipoteuliwa na kusimama kama wagombea binafsi.hapo tutapata rais mwenye tamaa ya madaraka,mwenye visasi,chuki,atatengeneza baraza la mawaziri kwa kujuana na mwisho wa siku atakuwa huru kwa sababu alijileta mwenyewe na mkamchagua yeye so hakuna wa kumwajibisha.usinidanganye wananchi watamwajibisha coz hata huyu tuliyenaye kama hao wananchi wangekuwa na huo uthubutu wa kuwajibisha wangekuwa tayari wamemwajibisha kwa wanavyomlalamikia but coz ni mazezeta hawawezi.
Ndiyo maana ya demokrasia ...
 
Back
Top Bottom